KWELI MUUNGANO WETU ULILETWA NA CHZI na unaendeshwa kichizi!
Mkuu Mwita, masuala ya Muungano yamenichosha, ujadiliwe upya.
Nikitafakari sana mambo ya Muungano huwa kichwa kinaniuma. Cha ajabu wanaoufaidi sana Muungano ndo wanaoongoza kuupinga. Wanaoumizwa ndo wanautetea. Binafsi sijawahi ona faida ya Muungano. Lord have mercy on me...
Asprin
Nina uhakika watanganyika wengi hawanufaiki na muungano na hawauhitaji lakini kitu cha ajabu ni kwamba hawalalamiki hadharani kama wanavyofanya wazanzibari.
Nina uhakika ikiitishwa kura ya maoni juu ya muungano mapendekezo yatakuwa ni either serikali tatu ama kuuvunja.
Na kwa kulitambua hilo unaona viongozi wa nchi hawataki muungano uguswe katika mjadala wa katiba mpya.
Dr. Hussein Mwinyi ambaye ni mbunge wa Kwahani Zanzibar, ameteuliwa kuongoza wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba Masuala ya Afya si ya muungano na SUK Zanzibar wanaye waziri wa afya Juma Duni Haji.
Wizara zinazohusika na mambo ya muungano ni pamoja na Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Ulinzi na JKT, Fedha, Habari, Vijana na Michezo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naomba ufafanuzi toka kwa mtu mwenye taarifa zaidi juu ya hili. Thanks!
tunataka kazi...awe znz au mtanganyika...sisi tunataka kazi!!!!
Nafikiri suala la muungano halikuzingatiwa hapa ila kilichoangaliwa zaidi ni taaluma aliyonayo Dr Mwinyi na mhe President anaamini atafit zaid katika wizara hiyo ya afya kuliko ile ya ulinzi so suala la muungano halihusiki kwa hapo.
wabongo bana mmeshaanza mambo yenu..dk hussein mwinyi he is a doctor by proffn so itakuwa rahisi kuongoza jahazi kuliko lile Li mponda lenu hata halijui kuwa panadol ni brand name...
Unaweza kukubaliana na mimi sasa kuwa watanganyika tumelogwa na sasa karibia wote tumekuwa mazezeta? Watu takribani milioni 40 tutakubalije kuufyata kwa watu wasiozidi 100?
wabongo bana mmeshaanza mambo yenu..dk hussein mwinyi he is a doctor by proffn so itakuwa rahisi kuongoza jahazi kuliko lile Li mponda lenu hata halijui kuwa panadol ni brand name...
huyu si alikuwepo 2005? Ni huyu na anna walileta siasa pale starlight na mgomo ukaendelea? Nanusa harufu ya mgomo utakaosababishwa na huyu jamaa kwa chuki zake binafsi.
Seriously, members wengine wanatuangusha! Ishu hapa sio ubaguzi wala hamna anaye-question integrity ya elimu yake. Swali ni utaratibu gani umetumika kumpa yeye uongozi wa mambo yasiyomhusu?
Keshamteua na anajua hatuna la kufanya