Uteuzi Mkurugenzi wa TBC, Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu

Clement Mshana, sio mtu muwazi na ambaye ataifanye TBC iwe kama Tiddo alivyofanya, kama mtakuwa na kumbukumbu nzuri huyu Clement Mshana ndie aliyezuia baadhi ya waandishi wa habari kuingia bungeni kurusha hotuba ya raisi mwaka jana, na mwandishi aliyezuiliwa alilalamika sana hata kwa kuandika makala kwenye gazeti.Huyu katumwa kuzima uhuru wote wa TBC
 
Ata vatican ilijilaumu sana kw a kuwapa Uaskofu akina Bishop Pius Ncube,Bishop Emmanuel Millingo na Bishop Koda wa Same.Ukurugenzi wa TBC umemzidi kimo Clemence Mshana
 
Tunaomba wasiwe na magamba maana muda wa kuyavua tena hawataupata
 
Leo naona mioyo saafi kabisa watu hawajalalamika dini. Aliteuliwa yule Prof wa Ardhi ilikuwa balaa. Ukweli huu ndio Utanzania, tuangalie qualifications na teuzi zifuatazo tujifunze kuhakiki uwezo badala ya kukimbilia dini.
 
Hongera bibi Mwamini I hope you still hold ujamaa na kujitegemea in your heart maana ni masiku mengi tumepotezana. May God the almighty direct your every step in your new position.
 
Woga wa uthubutu ndio ugonjwa wa Watanzania hatutaenda mbele kwa ugonjwa huu. tunahitaji watu wa msimamo na wenye maadili ili tutoke tulipo hivyo wote mlioteuliwa msiogope kufukuzwa kwa kutenda haki na kufuata kanuni. tanzania itajengwa na wenye moyo
 
Clement Mshana ni mtu makini sana. Hajui na hana siasa za maji taka. ataipeleka TBC na Nchi mbali sana. Mungu amjalie afya njema. nawapongeza wengine ingawa sina UHAKIKA sana na utendaji wao ila naamini sio "mashemeji".

Mshana ni Conservative,pro kikwete,pro ccm.alikua kaimu pale kabla ya Tido
 
Cha msingi ajira zooote nchizitangazwe magazetini na mashirika huru yafanyie watu usaili kama ilivyotokea kwa Katibu Mkuu FAT kuja TFF na Watanzania tukaona kweli uchapaji kazi ulivyokua.

Kwa njia ya ushindani kwa mfumo ule ule wa ki-soko huria inamaana hakuna kundi litakalolalamika kuonewa au kapendelewa yule. Hili ni swala la uamuzi tu wala hakuhitajiki fedha za misaada toka nje ya nchi kulitekeleza.

Leo naona mioyo saafi kabisa watu hawajalalamika dini. Aliteuliwa yule Prof wa Ardhi ilikuwa balaa. Ukweli huu ndio Utanzania, tuangalie qualifications na teuzi zifuatazo tujifunze kuhakiki uwezo badala ya kukimbilia dini.
 
Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.

huu uteuzi kichwa mafuta?? maji akafanye nini injinia huyu maskini???

Huyu Bashir Mrindoko alitajwa kwenye kamati ya Mwakyembe. Pamoja na Mrindoko watu wengine ambao alielekezwa JK awawajibishe ni Edward Hosea, Mary Kijo. Lakini hadi hii leo JK ameshindwa kuchukua hatua.

Halafu waTZ mnadanganyika na ghiriba za JK eti sasa ameamua kushughulikia ufisadi (read kujivua gamba) wakati anazidi kuwateua mafisadi wengine kushika nyadhifa kubwa.

Vyombo vya habari tafadhari wakumbusheni watanzania ni wasahaulifu kwamba huyu Mrindoko ni fisadi aliyetajwa kwenye tume ya Mwakyembe.

Hakuna cha kujivua gamba hapa ni changa la macho.
 
bashiri Mrindoko alitajwa kwenye ripoti ya mwakyembe kuhusu richmond na azimio Na. 14 lilisema:

AZIMIO NAMBA 14:

“Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni. Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.”

tusiwe warahisi kusahau jamani!!

kwa serikali ya CCM, hii ni moja ya hatua za kinidhamu. ni mara ngapi kiongozi akiboronga sehem A anahamishiwa sehemu B? cha muhimu aboronge in favour ya wateule wake!!
 
"Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli"

Kamati ya Mwakyembe ilimtaja hadi kwa jina na kushauri Rais amfukuze kazi kwa kusimamia vibaya mchakato haramu wa kuileta RICHMOND lkn badala yake leo tunaona anapandishwa cheo.
 
Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.

huu uteuzi kichwa mafuta?? maji akafanye nini injinia huyu maskini???

Bora kamtoa kampeleka huko, huyu jamaa alikua kikwazo sana kwenye maendeleo ya Nishati kwa ujumla. watakoma huko Maji.
 
Clement hana tofauti sana na yule mhariri mtendaji wa DailyNews. TBC sasa inarudi kule TvT na TBC(T) inarudi RTD ile ya akina Paul Sozigwa. Tutarajie vipindi kama mazungumzo baada ya habari vitarudi.
 
Nadahani imefika wakati Makatibu wakuu na manaibu wateuliwe kwa taaluma zao kwenda kuhudumu katika wizara husika kwa kuwa nafasi zao ni za kiutendaji zaidi hazihitaji propaganda, nadhani maendeleo yanachelewa nchini mwetu kwa kuwa sekta zinaongozwa na wasio wana sekta
 
Nilimjua mshana kupitia kipindi chake cha tuambie wakat wa tvt.lakini niseme kweli sikumkubali na mahojiano yake na watu waliokuwa anawaita kwani yalikuwa yana udhaifu kwa upande wa kuuliza maswali kwa wahusika.Kama mnafuatilia mahojiano ya Shaka Ssali wa VOA,mtakubaliana nami kuwa yale ndiyo mahojiano yanakidhi kiwango kwani anauliza swali bila kumwogopa mtu.
Katika hili naomba nijuzwe CV ya mshana.Binafsi ningependekeza angeteuliwa mtu wa pale pale tbc ingawa huyu naye alikuwepo pale.Ni maoni yangu jamani.
 
Back
Top Bottom