Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #101
Kama umepata kazi ya upishi, inapita miezi na hata miaka kadhaa hujapika chakula chochote na bado unapata mshahara, inabidi ujiulize kama bado unastahili hiyo nafasi. Ngereja anastahili kuwajibika yeye mwenyewe kwa kushindwa kufikia matazamio ya nafasi aliyopewa.
hili halina shaka lakini Ngeleja anacho kile tu ambaco amepewa. Kumuwekea mtu malengo ya kufikia kitu fulani halafu humpi nyenzo za kufikia malengo hayo kunawanyima waliompa malengo hayo kumdai kwanini hajayatimiza. Lakini vile vile wale wanaoweka malengo wanamuwekea malengo ya namna gani? Huwezi kumwambia Ngeleja atatue tatizo la umeme wakati uhuru wa kufanya hivyo unaamuliwa na Baraza la Mawaziri.