UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

Mkuu, stop being a cheap advocate

Open your eyes and think.

Kesi inategemea ushahidi, hoja zako zimejikita katika kigezo cha umri na speculation kuwa amebakwa na kuacha hoja zote za msingi.

Subiri postmotem na results za mkemia mkuu na mawasiliano ya simu yote ndo urudi tena.

Cheza na kesi ya mauaji wewe . . .

Unarahisisha mambo kilahisi bila hoja za nguvu!

hoja zako zinanisaidia kuthibitisha ya kuwa DPP ni bomu.......ilkuwaje amkamate Lulu wakati kumbe hata post-mortem ripoti haijakamilka, kumbe kuna hata mawasiliano ya simu hayajulikani yanasema nini na taarifa ya mkema mkuu haijulikani? Sasa DPP akiwa hana vielelezo hivi alifikiaje kumtia nguvuni masikini mtoto wa watu na kumfungulia makosa ya jinai wakati hana hata chembe ya ushahidi?

kwa khali hii hata wewe DPP anaweza sasa hivi kukutia ndani na kukufungulia kesi ya hii ya mauaji kwa madai anasubiria vielelezo muhimu kutoka kampuni ya simu, post-mortem report na ripoti ya mkemia mkuu...............Am very sad with the way this nation is heading..................yaani haki za raia zinachezewa kama za kuku ambaye uhai wake na uhuru wake uko mikononi mwa mbabaishaji yoyote yule kama huyu DPP............

ni vyema tiukaanza kuangalia haki za mtuhumiwa..........2day it Lulu 2morrow could be you.....................na kwa bahati mbaya hutakuwa unahushishwa na mauaji ya celebrity or a self-proclaimed number one Bongo movie superstar like mwendazake.............
 
...................huhitaji kuwa mwanasheria kufikiria tatizo lenu mnafikir shule inakupa vipaji.............shule yaweza kuviendeleza vipaji lakini Ni Mwenyezi Mungu ndiyo anayekupa vipaji na waweza kuviendeleza bila ya hata siku moja kukaa darasani........usikubali kuwa mtumwa wa kutafuniwa darasani jifunze kutafuna mwenyewe..........meno....brain/ubongo umepewa wa nini?

Nadhani hili ni tatizo lako la kuzaliwa nalo, kujifanya mjuaji kumbe kichwani hakuna kitu.
Unaweza kuthibitisha ubakaji wa kanumba? we unafikiri lulu akishasema tu kwamba kanumba alitaka kumbaka basi jaji anatoa hukumu ya kutomtia hatiani? kama wewe umesoma sheria basi ni hasara kwako, kwa familia yako na taifa kwa ujumla. mwanasheria gani asiyeweza kushughulisha akili yake??

Hoja zimetolewa hapa badala ya kuzijibu unaanza kuleta nyodo, sasa wewe nae katika watu waliosoma unajiita msomi? mara ujiite political analyst, mara mwanasheria hata hueleweki mkuu au ndo kuishi kimjinimjini!! Bora mimi nisiyesoma sheria lakini siwezi kuandika utumbo kama huu unaoandika hapa huku ukijiita mwanasheria.

Na jambo la mwisho na la msingi, umeshaiona charge sheet ya lulu? au ndo mambo ya u-bush lawyer!!??
 
Mkuu, stop being a cheap advocate

Open your eyes and think.

Kesi inategemea ushahidi, hoja zako zimejikita katika kigezo cha umri na speculation kuwa amebakwa na kuacha hoja zote za msingi.

Subiri postmotem na results za mkemia mkuu na mawasiliano ya simu yote ndo urudi tena.

Cheza na kesi ya mauaji wewe . . .

Unarahisisha mambo kilahisi bila hoja za nguvu!
Kama Zombe alishinda na maushahidi yote yale sitegemei Lulu kuendelea kubakia kuhukumiwa kifungo hata cha siku moja. Pia wanasheria wetu wanazidi kujidhihirisha kutojua sheria pale wanapo file kosa la Murder badala ya Manslaughter kama ilivyokuwa kwa Zombe.
 
Mimi si mwanasheria ingawa ningeshauri kuwa tusiweke maneno yetu na utaalamu wa kisheria katika kinywa cha Lulu. Hakuna anayependa kuona Lulu anaadhibiwa endapo hana kosa lakini pia tusitumie utaalamu wa kisheria kutetea uozo katika jamii. Lulu amekiri kuwa na wapenzi wa umri zaidi ya Babake ..... na hao je wafanywe nini? Hili suala ni pana zaidi ya tunavyolifanya kuonekana. Kwa ujumla maadili yameporomoka katika jamii yetu na nitajifunza kutoka kwa wanaseria kwani inaionekana kuwa wao wanapopita kona kona huwa awali ya youe wanauliza umri na birth ceritificate za hao vidosho? Na kuwataka wakalete Original Birth Certificate .... Mmmmh!

Ati kubakwa ..... suala zima zima halina mazingira ya ubakaji. Ukweli wa Lulu ndio wa muhimu kuliko ubingwa wa sheria.
 
hoja zako zinanisaidia kuthibitisha ya kuwa DPP ni bomu.......ilkuwaje amkamate Lulu wakati kumbe hata post-mortem ripoti haijakamilka,

Usiendelee kuiaibisha taaluma ya sheria na wanasheria kwa u-bush lawyer wako, tumia akili yako japo kidogo tu utafahamu kwamba lulu alikamatwa na polisi, DPP hafanyi kazi ya kukamata watuhumiwa!!
 
lulu-top.jpg

Elizabeth Michael Kimemeta

Mkakati wa Lulu kujitoa kenye makucha ya hii dola kandamizi sasa umeanza kuchipuka pale ambapo mshitakiwa wa hii kesi ya mauaji alipokerwa pale mahakamani alipokuwa akisomewa mashtaka tajwa dhidi yake na hata kunyosha kidole na kutoa sahihisho ya kuwa umri wake ni miaka 17 na wala siyo 18. Kwa kawaida kwenye kesi za mauaji mara ya kwanza husomwa katika mahakama ya hakimu mkaazi na mshitakiwa anayo haki ya kukaa kimya kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo lakini Lulu aliona aanze kuweka utetezi wake vyema hata katika hatua hiyo ya awali...............

Athari za kisheria za umri wa miaka 17
.

Umri huo unamweka Mwendazake -Steven Kanumba- ambaye ana umri wa miaka 28 katika khali mbaya ya kitabia na mwenendo kulingana na sheria ya makosa ya kijinai katika kujamiana pamoja na ya kuwa kwa vile yeye ni marehemu hawezi kushitakiwa nayo lakini yanapunguza makali ya Lulu kuwa na kesi tajwa ya kujibu.

Umri wa miaka 17 ni binti mtoto na wala siyo mtu mzima hivyo kuwa na mapenzi naye hata kama alipenda iwe hivyo unamgeuzia kibao mwendazake kuwa alikuwa anakusudia au alikuwa akimbaka Lulu na hivyo kuweka kesi ya mauaji kuwa na utetezi wa "self-defence" kwa maana ya kuwa Lulu alifanya yoyote yale yaliyo ndani ya uwezo wake kujitetea dhidi ya mwanaumme mtu mzima tena mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa anamkamia kumbaka.

Vilevile umri tajwa unamwondolea Lulu adhabu ya kifo endapo mahakama kuu itamtia hatiani kwenye makosa ya mauaji (very unlikely, though- uwezekano wa kumtia hatiani ni mdogo sana) na pia kumpa haki ya kuondolewa kwenye lupango ya watu wazima jambo ambalo polisi wetu wameendelea kukiuka haki zake kwa kumchanganya na lupango ya watu wazima. Utetezi wa kiawali wa Lulu unakuwa hauna mashiko pale Lulu atakapolalamikia ya kuwa polisi walimlazimisha kumshikilia kwenye lupango ya watu wazima na hivyo kumfanya aghafilike kiakili na hivyo kushindwa kutoa ushahidi sahihi na hivyo kuilazimu mahakama kuutupilia mbali ushahidi wa kiawali na hivyo kumruhusu autoe ushahidi mpya ambao ndiyo huu ninaouchambua na kuuwakilisha hivi sasa.

Lakini kubwa zaidi ni utetezi wa kimazingira ambao Lulu atautoa mahakamani wa ya kuwa yeye ni kinda wa chini ya miaka 18 na hivyo utamweka mwendazake katika mazingira ya kiubakaji au kukusudia kumbaka na hivyo utetezi wa self-defence kuwa na uzito wa kipekee.

Haya ni baadhi tu ya dondoo ambazo Lulu aweza kuzitumia katika kujinasua katika makucha tajwa:-

a) Mwendazake ndiye aliyemwita kuwa ana mazungumzo naye ya haraka usiku wa tukio juu ya tasnia ya filamu. Hivyo yeye Lulu hakuwa na makusudio ya kwenda kwa Kanumba kwa minajili ya kumwuuwa. Kumbuka DPP ni lazima athibitishe nia ya kuua ili mahakama imtie hatiani Lulu lakini kama ni kanumba ndiye aliyemwita mtuhumiwa nia ya Lulu kwenda kwa mwendazake kwa nia tajwa itaota mbawa kuwa isingewezakana kuwa vivyo kama DPP anavyodai.

b) Marafiki wa Lulu watathibitisha ya kuwa wao ndiyo waliokuwa wakimpigia simu na kutaka kujua alikuwa wapi na kwa nini amechelewa. Ushahidi huu wa kimazingira utazidi kubomoa hoja ya polisi ya kuwa Lulu alikwenda kwa mwendazake kwa nia ya kumtoa roho.

c) Lulu atathibitisha mahakamani ya kuwa kanumba siye mpenzi wake na kwa hivyo hoja ya DPP kuwa kulikuwa na ugomvi wa mapenzi kukosa mwelekeo.

d) Lulu atajenga hoja ya kuwa Kanumba alitaka kumbaka na yeye alitumia nguzu za mikono yake kujihami na kutokana na umri wa miaka 17 mahakama lazima ikubaliane naye ukizingatia mazingira yenyewe: Yawaje mtu mzima amkaribishe binti mdogo wa chini ya miaka 18 chumbani mwake kama lengo siyo kumbaka? Yawaje Kanumba akutwe hana nguo kwa maana ya kuwa yuko uchi wa mnyama na binti mdogo hivyo tena chumbani kwake? Kwa hiyo, hata kama lulu alitumia silaha iliyokuwemo chumbani kujilinda, mahakama itampa manufaa ya "benefit of doubt" na hivyo kuukubali utetezi wake. Lulu hakutumia silaha yoyote kulingana na ushahidi uliopo mikononi mwa DPP.

e) Lulu atadai kilichomwangusha Kanumba chini na kukosa fahamu hakina uhusiano na yeye bali ni matatizo yake ya kiafya na atatumia taarifa ya madaktari wa Muhimbili kuthibitisha ya kuwa kilichomtoa roho mwendazake ni mshtuko mkubwa katika ubongo wake (Brain concussion) ambao haukusababishwa na majeraha ya mwilini mwake ambayo hata hivyo hayapo. Mwendazake hakuwa na jeraha lolote kuonyesha lingeweza kumsababishia mshtuko tajwa.

f) Lulu atadai mahakamani ya kuwa hakuna ushahidi wowote ule wa kitaalamu ya kuwa marehemu alikufa kwa lolote jinginelo na inashangaza hata DPP kumfungulia kesi ya mauaji na hivyo kumbughudhi na kumdhaliliisha mbele ya jamii na hivyo kuiomba mahakama iangalie namna ya kumfidia dhidi ya kubambikiziwa kesi ambayo hata haipo au "malicious prosecution".

g) Lulu atarejea ushahidi wa ndugu wa marehemu aitwaye Seth ambaye alidai Lulu ana mazoea ya kwenda pale na ya kuwa hakuona kama kuna ubaya wowote kwa hiyo alimkaribisha na ya kuwa kaka yake ndiye aliyeanzisha zengwe pale aliposikia mlio wa simu ya Lulu na kuhisi ya kuwa Lulu alikuwa anapigiwa simu na mwanaumme mwingine. Hapa lengo litakuwa kuonyesha ya kuwa kama kuna ugomvi marehemu ndiye aliyeuanzisha kwa minajili ya kumbaka kwa kumzuia asiendelee na safari zake. Vile vile mdogo wa marehemu- Seth- aliona Lulu siyo mtu wa shari na ndiyo maana hakumzuia kuingia ndani kutokana na kuwa mtu wa amani na siyo wa hata kuweza kutishia maisha ya nduguye..........

kwa ushahidi huu na mwingineo mwingi, hakuna Jaji ambaye atakubali kuchafua heshima yake kwenye jamii na kuhalalisha mabinti wadogo wafanyiwe unyama hata kama unyama huo unafanywa na aliyekuwa akijiita mwenyewe "mcheza filamu nambari moja hapa nchini".

Hivyo basi mahakama itaamua Lulu hana kesi ya kujibu na mwendazake ndiye aliyejenga mazingira kwa yote yaliyomkuta na hapaswi kumtupia lawama mtoto mdogo aliyechini ya miaka 18.......

FUNDISHO KWETU SOTE

Aidha ni jukumu la watu wazima kuwa mfano wa malezi ya watoto wadogo badala ya wao kuwarubuni na kuwafunza namna ya kuyaharibu maisha ya watoto hao kupitia makosa ya jinai ya ubakaji kwa kuwarubuni na kuwapa ajira njaa za hapa na pale.............
Mkuu Ruta ahsante saana kutoa ukweli huo hadharani, nilijaribu kusaport thread ya Watanzania kushabikia uzinzi ikahamishiwa sijui (cereblity)!!!! Lakini kwa hili ndio ukweli mwendazake alitumia dhiki ya mtoto huyo na kumuweka chini ya himaya yake eti mpenzi wake tena anataka kufunga naye ndoa???????? Baada ya kumfundisha uigizaji akamfundisha na ufuska, kitendo cha kulala na mtoto under age ni cha ubakaji, siri imeanza kufichuka!!!! Hata kama mtoto huyo alikubali lakini kwa akli za utu uzima alitakiwa kumsaidia kielimu na malezi mema ansubilie akomae kiakili aingize gia zake baadae!!! Hivyo ushahidi wa umri unamtia mwendazake matatani, ikionyesha dhahili hakukuwa na penzi kati yao ila ni ubakaji!!!!!Tusishabikie wabakaji mwisho wa siku watoto wetu wataingia kwenye kundi hilo dhalimu wakifuata fadhila!!!!!

Jamani hii hoja ya kutaka kubakwa kwa Lulu inatoka wapi?
Mbona tulisikia kuwa Marehemu alimsikia Lulu akipokea simu na hivyo akahisi anaongea na mwanaume mwingine?
Hiyo inahusiana nini na kutaka kubakwa??:???
  1. Nadhani marehemu alitaka kumuadabisha Lulu.
  2. Lulu akajitetea kwa namna fulani.
  3. On the process marehemu alianguka.
  4. Labda alisukumwa kama ilivyosemwa, au aliteleza na kuanguka.

  • Nasema kuteleza kwa kuwa tumesikia kuwa marehemu alikuwa bafuni anaoga, huenda kwa kuw amelowa maji ni rahisi kuteleza sakafuni (Tiles).

Sasa basi kama kifo kimetokana na kuanguka, issue ya kubaka haipo na issue ya umri haina msingi hapo, maana Criminal liability kwa mtu yeyote ni inaanzia above 10yrs, Labda wakati wa hukumu ya kuua kwa kukusudia ndio umri wa Lulu unaweza kujadiliwa hapo.
Kwasasa umri sio issue kabisa.
 
Pitia tena hoja zako Allen naona zina migongano mikubwa..............mwanzo ulisema mwendazake mchumba wake alikuwa Donata.............baada ye unamgeuzia Lulu............hivi mwendazake alikuwa ana wa chumba wangapi kwa wakati mmoja?.........ingawaje utetezi wa kubakwa au kukusudiwa kubakwa haupanguliwi na uchumba au hata ndoa na kinda wa chini ya miaka 18........

Unajichanganya mwenyewe, Allien hajasema kwamba Dotnata alikuwa mchumba wa kanumba(mind you dotnata ni mke wa mtu). Alichosema Allien ni kwamba Dotnata ameshuhudia kwamba hawa watu walikuwa ni wachumba. Dotnata anathibitisha kwamba hawa watu walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita sasa.

Hata kama una mapenzi makubwa sana kwa lulu, usipotoshe watu mkuu, hakuna mwenye chuki na lulu, tunachotaka sisi ni ukweli ujulikane na lulku atendewe haki.
 
Mkuu andika full citation otherwise hizi sheria unazozisema zitakuwa ni za kwako binafsi.

CHAPTER 101
THE SEXUAL OFFENCES SPECIAL PROVISIONS ACT
[PRINCIPAL LEGISLATION]
ARRANGEMENT OF SECTIONS
Section
Title
PART I
PRELIMINARY PROVISIONS
1. Short title.
2. Interpretation.

PART II
AMENDMENT OF THE PENAL CODE
3.-20. [Amendment of Cap. 16.]

PART III
AMENDMENT OF THE CRIMINAL PROCEDURE ACT
21.-25. [Amendment of Cap. 20.]

PART IV
AMENDMENT OF THE EVIDENCE ACT
26. [Amendment of Cap. 6.]

PART V
AMENDMENT OF THE CHILDREN AND YOUNG PERSONS ACT
27. [Amendment of Cap. 13.]

PART VI
AMENDMENT OF THE MINIMUM SENTENCES ACT
28.-29. [Amendment of Cap. 90.]

CHAPTER 101
THE SEXUAL OFFENCES SPECIAL PROVISIONS ACT
An Act to amend several written laws, making special provisions in those laws with regard to sexual and other offences to further safeguard the personal integrity, dignity, liberty and security of women and children.
[1st July, 1998]
[s. 2]
Act No. 4 of 1998
PART I
PRELIMINARY PROVISIONS (ss 1-2)
[PCh101s1]1. Short title
This Act may be cited as the Sexual Offences Special Provisions Act.
[PCh101s2]2. Interpretation
In this Act, except where the context requires otherwise–
"boy" means a male person of the age of under eighteen years;
"girl" means a female person of the age of under eighteen years;
"gross indecency" means any sexual act that is more than ordinary but falls short of actual intercourse and may include masturbation and indecent physical contact or indecent behaviour without any physical contact;

soma kwenye hiyo nyekundu kwa uangalifu mkubwa sana.............hakuna makubaliano yoyote ya kutembea na msichana ambaye ni chini ya miaka 18............
 
Jamani hii hoja ya kutaka kubakwa kwa Lulu inatoka wapi?
Mbona tulisikia kuwa Marehemu alimsikia Lulu akipokea simu na hivyo akahisi anaongea na mwanaume mwingine?
Hiyo inahusiana nini na kutaka kubakwa??:???
  1. Nadhani marehemu alitaka kumuadabisha Lulu.
  2. Lulu akajitetea kwa namna fulani.
  3. On the process marehemu alianguka.
  4. Labda alisukumwa kama ilivyosemwa, au aliteleza na kuanguka.

  • Nasema kuteleza kwa kuwa tumesikia kuwa marehemu alikuwa bafuni anaoga, huenda kwa kuw amelowa maji ni rahisi kuteleza sakafuni (Tiles).

Sasa basi kama kifo kimetokana na kuanguka, issue ya kubaka haipo na issue ya umri haina msingi hapo, maana Criminal liability kwa mtu yeyote ni inaanzia above 10yrs, Labda wakati wa hukumu ya kuua kwa kukusudia ndio umri wa Lulu unaweza kujadiliwa hapo.
Kwasasa umri sio issue kabisa.

Kishoka, nimeipenda anaysis yako. Hawa wanasheria wanasoma notes bila kuangalia kwanza uhalisia pili na ushahidi wa kimazingira. Hapa bado uhalisia wa tukio anao Lulu, taarifa ya madaktari na pia afya ya Kanumba (ambayo Daktari wake anaweza kuielezea). Tuongelee ushahidi wa kimazingira .... Historia ya LULU ana wanaume wengi kwahiyo wote ni wabakaji. At least she has admitted that the misunderstanding was caused by the call she received from another Muzee!!! Baada ya tukio alikwenda Coco Beach na akaitwa na Daktari ambapo alikwenda akidhani Kanumba is back to his normal state .... akarudi ... ni kweli huyo alikuwa anabakwa?? Dotnata amekiri kuwa Kanumba alimpeleka Lulu kwake kumtambulisha kuwa anataka kumwoa.
 
Mkuu Ruta ahsante saana kutoa ukweli huo hadharani, nilijaribu kusaport thread ya Watanzania kushabikia uzinzi ikahamishiwa sijui (cereblity)!!!! Lakini kwa hili ndio ukweli mwendazake alitumia dhiki ya mtoto huyo na kumuweka chini ya himaya yake eti mpenzi wake tena anataka kufunga naye ndoa???????? Baada ya kumfundisha uigizaji akamfundisha na ufuska, kitendo cha kulala na mtoto under age ni cha ubakaji, siri imeanza kufichuka!!!! Hata kama mtoto huyo alikubali lakini kwa akli za utu uzima alitakiwa kumsaidia kielimu na malezi mema ansubilie akomae kiakili aingize gia zake baadae!!! Hivyo ushahidi wa umri unamtia mwendazake matatani, ikionyesha dhahili hakukuwa na penzi kati yao ila ni ubakaji!!!!!Tusishabikie wabakaji mwisho wa siku watoto wetu wataingia kwenye kundi hilo dhalimu wakifuata fadhila!!!!!

Mtumishi wetu,

Mkuu hapa hatuzungumzii uzinzi, hapa tunazungumzia kifo cha kanumba na kesi ya mauaji inayomkabili lulu.

umri wa lulu bado ni kizungumkuti, kwahiyo unapomhukumu mwenda zake basi unalazimika kututhibitishia umri halisi wa lulu, kwakuwa hapa kuna miaka 18, na kuna miaka 17. Kabla ya kutoa hukumu kwa mwendazake, thibitisha kwanza umri halisi wa lulu.
 
unajichanganya mwenyewe, allien hajasema kwamba dotnata alikuwa mchumba wa kanumba(mind you dotnata ni mke wa mtu). Alichosema allien ni kwamba dotnata ameshuhudia kwamba hawa watu walikuwa ni wachumba. Dotnata anathibitisha kwamba hawa watu walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita sasa.

Hata kama una mapenzi makubwa sana kwa lulu, usipotoshe watu mkuu, hakuna mwenye chuki na lulu, tunachotaka sisi ni ukweli ujulikane na lulku atendewe haki.

sioni hoja ya kisheria ya kuijibu hapa...........zaidi ya kuelezea ufahamu wake wa kihisia
 
Mtumishi wetu,

Mkuu hapa hatuzungumzii uzinzi, hapa tunazungumzia kifo cha kanumba na kesi ya mauaji inayomkabili lulu.

umri wa lulu bado ni kizungumkuti, kwahiyo unapomhukumu mwenda zake basi unalazimika kututhibitishia umri halisi wa lulu, kwakuwa hapa kuna miaka 18, na kuna miaka 17. Kabla ya kutoa hukumu kwa mwendazake, thibitisha kwanza umri halisi wa lulu.

ukikataa kuzungumzia uzinzi ina maana Lulu kamwe ushaidi wake hauwezi kusikilizwa.............watu hufa na wengi wetu tunakufa kwa sababu zetu wenyewe.......................kwa nini makimbilia kauwawa ....hivi yeye alikuwa siyo wa kufa kama wengine tunavyokufa?
 
soma kwenye hiyo nyekundu kwa uangalifu mkubwa sana.............hakuna makubaliano yoyote ya kutembea na msichana ambaye ni chini ya miaka 18............

Wakati tunaendelea kujisomea hiyo sheria na wewe thibitisha pasipo shaka kwamba umri wa lulu ni chini ya miaka 18.
 
ukikataa kuzungumzia uzinzi ina maana Lulu kamwe ushaidi wake hauwezi kusikilizwa.............watu hufa na wengi wetu tunakufa kwa sababu zetu wenyewe.......................kwa nini makimbilia kauwawa ....hivi yeye alikuwa siyo wa kufa kama wengine tunavyokufa?

Hakuna anayekataa kanumba kufa, hapa tunazungumzia mazingira na sababu za kifo chake, kama angejifia mwenyewe chumbani bila lulu kuwepo unadhani sasahivi tungekuwa tunayaandika haya??

Mashitaka yaliyoko mbele ya lulu ni mauaji ya kanumba, sasa kama unadhani huo utetezi wa kutaka kubakwa unaweza kuhalalisha kuua ama unaweza kumnasua na kesi ya mauaji, basi endelea kumtengenezea utetezi mkuu.
 
Kishoka, nimeipenda anaysis yako. Hawa wanasheria wanasoma notes bila kuangalia kwanza uhalisia pili na ushahidi wa kimazingira. Hapa bado uhalisia wa tukio anao Lulu, taarifa ya madaktari na pia afya ya Kanumba (ambayo Daktari wake anaweza kuielezea). Tuongelee ushahidi wa kimazingira .... Historia ya LULU ana wanaume wengi kwahiyo wote ni wabakaji. At least she has admitted that the misunderstanding was caused by the call she received from another Muzee!!! Baada ya tukio alikwenda Coco Beach na akaitwa na Daktari ambapo alikwenda akidhani Kanumba is back to his normal state .... akarudi ... ni kweli huyo alikuwa anabakwa?? Dotnata amekiri kuwa Kanumba alimpeleka Lulu kwake kumtambulisha kuwa anataka kumwoa.

nimeibandika sheria ya sexual offences act......................labda itasaidia kukutoa hizi tongotongo
 
nimeibandika sheria ya sexual offences act......................labda itasaidia kukutoa hizi tongotongo

Sheria haina tafsiri, ndio maana kukawepo mahakama kwaajili ya kazi ya tafsiri.
Sioni kama kuna issue ya kubaka katika sakata la kifo cha Marehemu Kanumba hapa.
Na hiyo uliyotoa hapo ni Definition of terms tu, itakusaidia katika kutafsiri vifungu vya sheria husika Ruta!.
 
Nadhani hili ni tatizo lako la kuzaliwa nalo, kujifanya mjuaji kumbe kichwani hakuna kitu.
Unaweza kuthibitisha ubakaji wa kanumba? we unafikiri lulu akishasema tu kwamba kanumba alitaka kumbaka basi jaji anatoa hukumu ya kutomtia hatiani? kama wewe umesoma sheria basi ni hasara kwako, kwa familia yako na taifa kwa ujumla. mwanasheria gani asiyeweza kushughulisha akili yake??

Hoja zimetolewa hapa badala ya kuzijibu unaanza kuleta nyodo, sasa wewe nae katika watu waliosoma unajiita msomi? mara ujiite political analyst, mara mwanasheria hata hueleweki mkuu au ndo kuishi kimjinimjini!! Bora mimi nisiyesoma sheria lakini siwezi kuandika utumbo kama huu unaoandika hapa huku ukijiita mwanasheria.

Na jambo la mwisho na la msingi, umeshaiona charge sheet ya lulu? au ndo mambo ya u-bush lawyer!!??

mwita learn to read between the lines...................ninachosema ni utetezi....mark my words........................hayo mengineyo hayaboreshi mjadala nijitie na hata nisipojitia.................haina maana jibu hoja ..........if you can or simply shut up..........
 
Back
Top Bottom