Utetezi wa Kwanza wa MwanaKijiji - Tanzania Kama Wazo

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Utetezi wa kwanza: Tanzania kama wazo​

M. M. Mwanakijiji

Mola nakuabudia
Sifa nakurudishia
U peke nakuinamia
Jinalo natukuzia

Kalamu naishikia
Wazo naliandikia
Linahusu Tanzania
Mama nampigania.

Ndugu zangu, Tanzania kama wazo. Ni wazo ambalo uhai wake hautegemei uwepo wa Muungano, uhalisia wake hautegemei nani yuko madarakani, na uwepo wake hautokani na nani analitaka au hataki. Naam, uwepo wa Tanzania kama wazo hautegemei Zanzibar wanafanya nini, au bara wanafanya nini; haujalishi kama CCM wanaboronga au CUF wanatawala.

Kutokuelewa Wazo hili yaani Tanzania - kunasababisha watu wengi kutokuelewa nchi iitwayo Tanzania. Tumetimiza miaka 47 ya Muungano wetu na kwa kiasi kubwa tumeenda mbali sana na wazo la Tanzania na sasa tumebakia kutafuta namna ya kuokoa Muungano. Watawala wetu waliposhindwa kulisimamia wazo la Tanzania walibakia kuhangaika na mambo ya nchi ya Tanzania yaani yale yanayosumbua watawala kwa iliyokuwa nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika.

Huwezi kuiokoa nchi ya Tanzania bila kurudia wazo la Tanzania. Yawezekana kwa wengine naonekana nazungumza kama kwa kitendawili. Labda nijaribu kuelezea kidogo juu ya hiki ninachokiita kuwa ni “Tanzania kama wazo” au kwa kimombo Tanzania as an idea.

Sehemu kubwa ya nchi ya Marekani ambayo tunaiona leo hii na kuiita “Marekani” ilikuwa ni koloni la Mwingereza na sehemu nyingine zilikuwa ni makoloni ya Ufaransa (Sehemu kubwa ya Jimbo la Lousianna), sehemu ya nchi ya Mexico (California na New Mexico kwa mfano) na Alaska (toka kwa Urusi). Lakini majimbo 13 ya kwanza (the Original Thirteen) ambayo yaliunda United States of America yote yalikuwa ni makoloni ya Uingereza.

Walipotangaza uhuru wao makoloni hayo 13 yalitangaza nia vile vile ya kutaka kuwa na taifa la namna gani wanalolitaka. Hili limeelezwa vizuri katika Tangazo la Uhuru la mwaka 1776 kwa kuelezea manung’uniko au kero mbalimbali ambazo makoloni hayo yaliziona kutoka kwa utawala wa Mfalme George wa III.

Malalamiko yao yalihusiana na masuala ya kodi, utawala, kujitegemea na kutosikilizwa. Na vita ya mapinduzi ilipoanza mwaka mmoja kabla Wamarekani hao wa mwanzo walijua kabisa kuwa hawakutaka nchi ya namna gani.

Yaani, kuna mambo ambayo waliyaona katika utawala wa Mwingereza na ambayo wao wenyewe wasingependa kuyaona yakiendelea na ni katika kubuni mfumo wao wa utawala ndipo walipoanza kufanya majadiliano ya kuandika Katiba mpya ambayo itawaelekeza kwenye nchi ambayo wanaitaka.

Hivyo vita yao haikuwa kwa ajili ya nchi waliyokuwa nayo tayari bali kwa ajili ya nchi waliyotaka kuwa nayo. Kimsingi walipigania wazo la mbali, njozi tunaweza kusema - ambayo waliweza kuiona ikiwaka katika mioyo yao na walikuwa tayari kufa ili hata kama wao wasingeweza kuiona njozi hiyo basi watoto wao waje kuifurahia.

Hivyo, vita yao ya mapinduzi ya kukataa utawala wa Mwingereza iliongozwa na wazo la nchi waliyokuwa wanaitaka. Na Azimio la Uhuru ilikuwa ni kama ramani ya kusema wapi wanataka kwenda na walipoandika Katiba yao miaka kumi baada ya vita

Wamarekani waliweza kuweka katika maandishi namna ya utawala wanaoutaka na kuanzia wakati ule wamekuwa wakijaribu kurudi kwanza kwenye roho ya Azimio na mara zote kwenye Katiba ile ya kwanza kabisa. Kwa sababu vyote viwili Azimio la Uhuru na

Katiba viliwakilisha na kubeba ndani yake matamanio ya Wamarekani.

Hivyo, kwa Wamarekani taifa lao ni zaidi ya nchi ya kijiografia. Kwao Marekani ni wazo vile vile na ni wazo ambalo wamejitahidi kulifikia na kulilinda kwa gharama yoyote ile. Walipoliandika wazo hilo Marekani haikuwa kamilifu. Bado kulikuwepo na watumwa, wanawake walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura, watu weusi bado walikuwa wanaonekana duni na mambo mengine mengi tu ambayo hayakuendana na roho ya Azimio la Uhuru.

Lakini kwa kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo walivyoibuka watu mbalimbali ambao walikuwa wanajitahidi kuwakumbusha Wamarekani wenzao juu ya ‘wazo’ la Taifa walilolipigania. Kina W.E. B. Dubois, kina Ab Lincoln, na kina Martin Luther King Jr., wote katika Ujumbe wa zamu yao na kwa watu wa zama zao waliwakumbusha Wamarekani juu ya tunu za wazo la taifa lao ambalo wazee wao walilipigania.

Hao walitangulia
Wazo walipigania
La nchi waliyotakia
Njozi waliyoitamania.

Hivyo, nchi hii ya Marekani, ya leo imetokana na wazo na Wamarekani karibu wote wanalielewa vizuri sana wazo hili na kwamba wako tayari kumtosa mtu yeyote bila kujali uwezo wake, cheo chake wala nafasi yake yoyote ile kama mtu huyo ni kikwako au anatishia kuendelea kudhihirika kwa lile wazo – yaani Marekani.

Walipambana na vikundi vya Mafia, walikuta tayari kumfikisha Marekani Rais wao, wamewafunga majaji, maseneta, wabunge, mapadri, mashehe, walimu, wa mama wa nyumbani matajiri wa kutupwa, maskini n.k Kwao hakuna mtu yeyote ambaye yuko juu ya wazo yaani Marekani.

Ni kutokana na ukweli huo Marekani iliweza kukua na kufikia majimbo 50 ya sasa na kutoka na na hilo imeweza kusimama na kuwa taifa lenye nguvu zaidi. Wengi wanafikiria nguvu ya Marekani inatokana na utajiri wake au uwezo wa jeshi lake. Ndugu zangu hivi vyote vimekuja kutokana na Wamarekani kujitambua wao ni nani na wazee walitaka kuwa na taifa gani na hilo limewafanya Wamarekani kuwa na hisia fulani juu yao wenyewe.

Wanajitambua kuwa wako katika zamu yao leo hii na wanajua kila mmoja wao jukumu lake ni kuwaachia kizazi kijacho cha Wamarekani, taifa lililo bora zaidi na ambalo bado linaakisi lile wazo ambalo lilisababisha kutaka kuwa huru.

Kuna nchi chache sana duniani ambazo zimetokana na wazo kwanza. Marekani ni mojawapo na Tanzania ni nyingine. Taifa la Tanzania limetokana na wazo ambalo lilipaswa kutuongoza tunapojadili Muungano na matatizo yetu mbalimbali kama taifa. Bahati mbaya sana wazo hilo la Tanzania limekufa na sasa watu wanaaminishwa kuwa Tanzania nchi tu ambayo unaweza kuivunja na ikafa.

Na ni bahati mbaya sana katika Taifa letu leo hii hatuna wasomi wala wanasiasa wenye uwezo wakutetea Tanzania kama wazo kwa sababu wao wenyewe hawalijui wazo hilo au kulikumbuka. Si Rais Kikwete, si Pinda, si Makinda, si Karume, siyo Seif, siyo Nassor Moyo, si Pengo, siyo Kakobe wala siyo maprofesa wetu wa vyuo vyetu vikuu. Hadi hivi sasa hajatokea mtu ambaye anaweza kuitetea Tanzania kama wazo ambalo tunalipigania.

Ndiyo maana nimesema huu ni utetezi wa kwanza wa Tanzania kama wazo.
Wazo letu la Tanzania liliandikwa katika kile tunachokifahamu kama Azimio la Arusha. Azimio la Arusha lilikuwa ni jaribio la kwanza kabisa katika bara la Afrika niko tayari kusahihishwa katika hilo ambapo jamii ya watu weusi waliweza kuainisha kwa maandishi kanuni za maisha mahusiano kati yao na kati ya watawala wao na wao.

Azimio la Arusha lilikuwa ni tangazo la nchi ambayo tunaitaka. Watu wengi wanafikiria Azimio la Arusha lilikuwa ni kutangaza “ujamaa” tu na kunyang’anya mali za binafsi. La hasha, AR ina sehemu ndogo tu ya mambo ya kutaifisha mali bali sehemu yake kubwa ni ufafanuzi wa taifa ambalo tulitaka kulijenga.

Lakini Azimio ilikuwa ni kuandikwa tu kile ambacho wazee wetu walikuwa wameshaanza kukizungumzia. Wazee wa Dar wa miaka ya 40 na 50 ambao walianza mapema kuupinga utawala wa kikoloni walifanya hivyo mioyoni mwao wakifikiria taifa walilokuwa wakilitaka.

Na hata Nyerere alipofika Dar na kukutana na wazee hawa kina Sykes na wengine alijikuta yuko miongoni mwa wenzake hasa kwani walijikuta wanakubaliana kuwa ukoloni ulikuwa hautakiwi tena na tulitaka kuwa huru kujenga taifa letu wenyewe.

Hii ilikuwa pia kweli kwa wazee wa Kilimanjaro na sehemu nyingine nchini ambao nao mioyoni mwao walitambua adha ya kutawala. Na mbegu hii ya kukataa kutawaliwa na wageni haikuanzia Dar peke yake bali hata wazee wetu katika Vita ya Maji Maji walipigana kuonyesha kuwa hawakuwa tayari kuendelea kutawaliwa tu bila kuwa na sauti katika serikali hiyo.

Hivyo, upinzani wote wa kile ambacho tunakitambua kama “Harakati za Uhuru” ulitokana na wazee wetu kutamani kitu bora zaidi ambacho kitakuwa chao.

Hivyo, ujio wa Azimio la Arusha na siasa za mwanzo za Taifa letu viliweka msingi wa nchi tunayoitaka. Havikutupatia nchi yenyewe. Wengi siku hizi wanazungumzia ati Tanzania ilikuwa nchi ya kijamaa si kweli Tanzania haijawahi kuwa nchi ya kijamaa hata siku moja. Bali ni nchi iliyojaribu kujenga ujamaa wake na mambo yote ya kujenga mfumo huo hayakufanyika.

Katika hotuba yake ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Augusti 5, 1967 (miezi michache tu tangu kutangazwa kwa Azimio la Arusha) Nyerere alisema hivi kutukumbusha kuwa Azimio lilikuwa ni lengo –wazo.

“Azimio la Arusha ni azimio la shabaha tu, basi. Azimio hilo linatamka lengo TANU itakakowaongoza watu wa Tanzania, na linaweka shabaha za maendeleo. Tanzania haikuwa nchi ya Ujamaa ghafla siku ile ile ya tarehe 5 Februari, au siku yoyote tokea hapo wala kwa sababu hiyo tu Tanzania haijawa nchi yenye kujitegemea, au nchi iliyoendelea.

Azimio la Arusha lisingeweza kufanya mambo hayo siku hiyo hiyo wala isingewezekana hata kama watu wangekuwa na ari na nguvu kiasi gani, kutimiza shabaha hizo katika miezi michache hii tangu Azimio lipitishwe na TANU.” Na akasema hapo hapo kuwa
“Azimio ndio mwanzo, si mwisho, wa safari ndefu sana ambayo bila shaka itakuwa na matatizo mengi”.

Hivyo waasisi wetu walitambua hivyo. Ndiyo maana wengine tunashangaa kuwa watu wale wale ambao waliunga mkono Azimio leo hii hata kulitamka kwenye midomo yao wanashindwa. Hakuna watetezi wa Azimio. Ni kama Wamarekani watokee leo hii na kuanza kubeza msingi wa taifa lao yaani Azimio lao la Uhuru. Jamani, Azimio la Uhuru la Wamarekani lilisema “Binadamu wote ni sawa”. Lakini wakati huo huo Marekani ilikuwa na watumwa na wanawake walikuwa haruhusiwi kupiga kura. Usawa uko wapi?

Lakini hawakutokea Wamarekani waliodai Azimio lao litupiliwe mbali kwa sababu ati haliendani na “hali halisi” au kwamba “limepitwa na wakati”. La hasha, bali walijitokeza watu waliojaribu kulikumbusha taifa hilo misingi yake. Watu waliotaka wenzao warudi na kuliangalia lile wazo lililounda taifa hilo. Hadi leo Wamarekani wakubwa na wadogo wanawashwa mioyo yao kwa kusoma Azimio hilo.

Hivyo ndugu zangu – hatuwezi kuielewa Tanzania bila kuelewa wazo liliounda nchi inayoitwa Tanzania. Kuna vitu vilivyoifanya Tanzania kuwa Tanzania na Muungano ni sehemu yake ndogo sana.

Tanzania ni wazo la watu ambao walitaka kuwa pamoja na kujenga aina fulani ya maisha. Hatuwezi na tunachezeana kufikiri kuwa tunaweza kupiga hatua ya haraka ya maendeleo kama Watanzania bila kurudia misingi yetu iliyotufanya tuwe Watanzania.

Ninaposikia ati Watanzania wanaogopa Kuungana na Wakenya ninashangaa, tangu lini? Ninaposikia ati kuna Watanzania wanasema kwa haraka tu “vunjeni Muungano yaishe” najiuliza wameingiwa na kitu gani? Ninaposikia ati kuna Watanzania wanasema “yule asipewe nafasi fulani kwa sababu ni dini fulani au Kabila fulani” najiuliza watu wangu wamepatwa na tatizo gani?

Azimio la Arusha lilisema haya (kati ya mengine mengi). Binadamu wote ni sawa, leo tunaangalia Watanzania wanachukua sheria mikononi mwao kwa kuwapiga na kuwaua Watanzania wenzao kule Tegeta kana kwamba wao ni Watanzania zaidi kuliko wale waliouawa!

Kila mtu anastahili heshima, leo hii kuna watu wengine wamekuwa majaji wa nani anastahili heshima na nani hastahili. Yaani, hata katika sehemu ya tofauti zetu za kisiasa wapo ambao wamefikia mahali pa kutengeneza uadui na dharau isiyo kifani wakiamini kuwa wao wanastahili heshima zaidi!

Raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili wan chi hii ukiwa kama dhamana kwa vizazi vijavyo – leo hii kufuatilia utajiri wetu tunaambiwa tunapenda sana ujamaa. Ati leo uwekezaji unatakiwa uwe ni ufunguo wa kuwanyang’anya Watanzania umiliki wa utajiri wao ambao ni dhamana yao. Jamani, wanataka kuuza urithi wetu na hawataki waulizwe!

Ndugu zangu hatuwezi kwenda mbali tunakotaka bila kurudia misingi yetu, kuisahihisha mengine na kuiboresha mingine lakini kuna misingi ambayo ilifanya Tanzania kuwa Tanzania na hiyo ilitangalia hii nchi tunayoita Tanzania. Wale wanaobeza Ujamaa ni kwa sababu hawajawahi kuusoma na kuulewa.

Hata watu wanaozungumzia ujamaa wengine wanadanganya wakifikiri tunazungumzia kitu kile kile. Ni kwa sababu hiyo ni muhimu kuanza kurudi nyuma na kuelewa Tanzania kama wazo kwani ni hapo tu ndipo tutaweza naamini kufikiria ni namna gani tunaweza kujenga taifa la kisasa kwa haraka zaidi.

Bila wazo la kutuongoza au shabaha watawala wetu watakuja na maneno mengi ya hadaa na kujaribu kutuburuza.

Turudi kwenye msingi. Tuelewe kwanza Tanzania kama wazo. Je, ilikuwa ina maana gani kuitwa Mtanzania? Je, Tanzania ilijitofautisha vipi na mataifa mengine ya Afrika?

Kwanini ilikuwa ni fahari kubwa kuitwa Mtanzania? Nasubiri kwa hamu kuona mdahalo wa kisomi ambao utajaribu kugusia mambo haya na kutukumbusha jinsi Utanzania ulivyokuwa tunu ya kututofautisha na watu wa mataifa mengine.

Niandikie: Mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mola nakuabudia
Sifa nakurudishia
U peke nakuinamia
Jinalo natukuzia

Kalamu naishikia
Wazo naliandikia
Linahusu Tanzania
Mama nampigania.

Ndugu zangu, Tanzania kama wazo. Ni wazo ambalo uhai wake hautegemei uwepo wa Muungano, uhalisia wake hautegemei nani yuko madarakani, na uwepo wake hautokani na nani analitaka au hataki. Naam, uwepo wa Tanzania kama wazo hautegemei Zanzibar wanafanya nini, au bara wanafanya nini; haujalishi kama CCM wanaboronga au CUF wanatawala.

Kutokuelewa Wazo hili yaani Tanzania - kunasababisha watu wengi kutokuelewa nchi iitwayo Tanzania. Tumetimiza miaka 47 ya Muungano wetu na kwa kiasi kubwa tumeenda mbali sana na wazo la Tanzania na sasa tumebakia kutafuta namna ya kuokoa Muungano. Watawala wetu waliposhindwa kulisimamia wazo la Tanzania walibakia kuhangaika na mambo ya nchi ya Tanzania yaani yale yanayosumbua watawala kwa iliyokuwa nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika.

Huwezi kuiokoa nchi ya Tanzania bila kurudia wazo la Tanzania. Yawezekana kwa wengine naonekana nazungumza kama kwa kitendawili. Labda nijaribu kuelezea kidogo juu ya hiki ninachokiita kuwa ni “Tanzania kama wazo” au kwa kimombo Tanzania as an idea.

Sehemu kubwa ya nchi ya Marekani ambayo tunaiona leo hii na kuiita “Marekani” ilikuwa ni koloni la Mwingereza na sehemu nyingine zilikuwa ni makoloni ya Ufaransa (Sehemu kubwa ya Jimbo la Lousianna), sehemu ya nchi ya Mexico (California na New Mexico kwa mfano) na Alaska (toka kwa Urusi). Lakini majimbo 13 ya kwanza (the Original Thirteen) ambayo yaliunda United States of America yote yalikuwa ni makoloni ya Uingereza.

Walipotangaza uhuru wao makoloni hayo 13 yalitangaza nia vile vile ya kutaka kuwa na taifa la namna gani wanalolitaka. Hili limeelezwa vizuri katika Tangazo la Uhuru la mwaka 1776 kwa kuelezea manung’uniko au kero mbalimbali ambazo makoloni hayo yaliziona kutoka kwa utawala wa Mfalme George wa III.
Malalamiko yao yalihusiana na masuala ya kodi, utawala, kujitegemea na kutosikilizwa. Na vita ya mapinduzi ilipoanza mwaka mmoja kabla Wamarekani hao wa mwanzo walijua kabisa kuwa hawakutaka nchi ya namna gani.

Yaani, kuna mambo ambayo waliyaona katika utawala wa Mwingereza na ambayo wao wenyewe wasingependa kuyaona yakiendelea na ni katika kubuni mfumo wao wa utawala ndipo walipoanza kufanya majadiliano ya kuandika Katiba mpya ambayo itawaelekeza kwenye nchi ambayo wanaitaka.

Hivyo vita yao haikuwa kwa ajili ya nchi waliyokuwa nayo tayari bali kwa ajili ya nchi waliyotaka kuwa nayo. Kimsingi walipigania wazo la mbali, njozi tunaweza kusema - ambayo waliweza kuiona ikiwaka katika mioyo yao na walikuwa tayari kufa ili hata kama wao wasingeweza kuiona njozi hiyo basi watoto wao waje kuifurahia.

Hivyo, vita yao ya mapinduzi ya kukataa utawala wa Mwingereza iliongozwa na wazo la nchi waliyokuwa wanaitaka. Na Azimio la Uhuru ilikuwa ni kama ramani ya kusema wapi wanataka kwenda na walipoandika Katiba yao miaka kumi baada ya vita Wamarekani waliweza kuweka katika maandishi namna ya utawala wanaoutaka na kuanzia wakati ule wamekuwa wakijaribu kurudi kwanza kwenye roho ya Azimio na mara zote kwenye Katiba ile ya kwanza kabisa. Kwa sababu vyote viwili Azimio la Uhuru na Katiba viliwakilisha na kubeba ndani yake matamanio ya Wamarekani.
Hivyo, kwa Wamarekani taifa lao ni zaidi ya nchi ya kijiografia. Kwao Marekani ni wazo vile vile na ni wazo ambalo wamejitahidi kulifikia na kulilinda kwa gharama yoyote ile. Walipoliandika wazo hilo Marekani haikuwa kamilifu. Bado kulikuwepo na watumwa, wanawake walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura, watu weusi bado walikuwa wanaonekana duni na mambo mengine mengi tu ambayo hayakuendana na roho ya Azimio la Uhuru.

Lakini kwa kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo walivyoibuka watu mbalimbali ambao walikuwa wanajitahidi kuwakumbusha Wamarekani wenzao juu ya ‘wazo’ la Taifa walilolipigania. Kina W.E. B. Dubois, kina Ab Lincoln, na kina Martin Luther King Jr., wote katika Ujumbe wa zamu yao na kwa watu wa zama zao waliwakumbusha Wamarekani juu ya tunu za wazo la taifa lao ambalo wazee wao walilipigania.

Hao walitangulia
Wazo walipigania
La nchi waliyotakia
Njozi waliyoitamania.

Hivyo, nchi hii ya Marekani, ya leo imetokana na wazo na Wamarekani karibu wote wanalielewa vizuri sana wazo hili na kwamba wako tayari kumtosa mtu yeyote bila kujali uwezo wake, cheo chake wala nafasi yake yoyote ile kama mtu huyo ni kikwako au anatishia kuendelea kudhihirika kwa lile wazo – yaani Marekani.
Walipambana na vikundi vya Mafia, walikuta tayari kumfikisha Marekani Rais wao, wamewafunga majaji, maseneta, wabunge, mapadri, mashehe, walimu, wa mama wa nyumbani matajiri wa kutupwa, maskini n.k Kwao hakuna mtu yeyote ambaye yuko juu ya wazo yaani Marekani.

Ni kutokana na ukweli huo Marekani iliweza kukua na kufikia majimbo 50 ya sasa na kutoka na na hilo imeweza kusimama na kuwa taifa lenye nguvu zaidi. Wengi wanafikiria nguvu ya Marekani inatokana na utajiri wake au uwezo wa jeshi lake. Ndugu zangu hivi vyote vimekuja kutokana na Wamarekani kujitambua wao ni nani na wazee walitaka kuwa na taifa gani na hilo limewafanya Wamarekani kuwa na hisia fulani juu yao wenyewe.

Wanajitambua kuwa wako katika zamu yao leo hii na wanajua kila mmoja wao jukumu lake ni kuwaachia kizazi kijacho cha Wamarekani, taifa lililo bora zaidi na ambalo bado linaakisi lile wazo ambalo lilisababisha kutaka kuwa huru.

Kuna nchi chache sana duniani ambazo zimetokana na wazo kwanza. Marekani ni mojawapo na Tanzania ni nyingine. Taifa la Tanzania limetokana na wazo ambalo lilipaswa kutuongoza tunapojadili Muungano na matatizo yetu mbalimbali kama taifa. Bahati mbaya sana wazo hilo la Tanzania limekufa na sasa watu wanaaminishwa kuwa Tanzania nchi tu ambayo unaweza kuivunja na ikafa.

Na ni bahati mbaya sana katika Taifa letu leo hii hatuna wasomi wala wanasiasa wenye uwezo wakutetea Tanzania kama wazo kwa sababu wao wenyewe hawalijui wazo hilo au kulikumbuka. Si Rais Kikwete, si Pinda, si Makinda, si Karume, siyo Seif, siyo Nassor Moyo, si Pengo, siyo Kakobe wala siyo maprofesa wetu wa vyuo vyetu vikuu. Hadi hivi sasa hajatokea mtu ambaye anaweza kuitetea Tanzania kama wazo ambalo tunalipigania.

Ndiyo maana nimesema huu ni utetezi wa kwanza wa Tanzania kama wazo.
Wazo letu la Tanzania liliandikwa katika kile tunachokifahamu kama Azimio la Arusha. Azimio la Arusha lilikuwa ni jaribio la kwanza kabisa katika bara la Afrika niko tayari kusahihishwa katika hilo ambapo jamii ya watu weusi waliweza kuainisha kwa maandishi kanuni za maisha mahusiano kati yao na kati ya watawala wao na wao.

Azimio la Arusha lilikuwa ni tangazo la nchi ambayo tunaitaka. Watu wengi wanafikiria Azimio la Arusha lilikuwa ni kutangaza “ujamaa” tu na kunyang’anya mali za binafsi. La hasha, AR ina sehemu ndogo tu ya mambo ya kutaifisha mali bali sehemu yake kubwa ni ufafanuzi wa taifa ambalo tulitaka kulijenga.

Lakini Azimio ilikuwa ni kuandikwa tu kile ambacho wazee wetu walikuwa wameshaanza kukizungumzia. Wazee wa Dar wa miaka ya 40 na 50 ambao walianza mapema kuupinga utawala wa kikoloni walifanya hivyo mioyoni mwao wakifikiria taifa walilokuwa wakilitaka. Na hata Nyerere alipofika Dar na kukutana na wazee hawa kina Sykes na wengine alijikuta yuko miongoni mwa wenzake hasa kwani walijikuta wanakubaliana kuwa ukoloni ulikuwa hautakiwi tena na tulitaka kuwa huru kujenga taifa letu wenyewe.

Hii ilikuwa pia kweli kwa wazee wa Kilimanjaro na sehemu nyingine nchini ambao nao mioyoni mwao walitambua adha ya kutawala. Na mbegu hii ya kukataa kutawaliwa na wageni haikuanzia Dar peke yake bali hata wazee wetu katika Vita ya Maji Maji walipigana kuonyesha kuwa hawakuwa tayari kuendelea kutawaliwa tu bila kuwa na sauti katika serikali hiyo. Hivyo, upinzani wote wa kile ambacho tunakitambua kama “Harakati za Uhuru” ulitokana na wazee wetu kutamani kitu bora zaidi ambacho kitakuwa chao.

Hivyo, ujio wa Azimio la Arusha na siasa za mwanzo za Taifa letu viliweka msingi wa nchi tunayoitaka. Havikutupatia nchi yenyewe. Wengi siku hizi wanazungumzia ati Tanzania ilikuwa nchi ya kijamaa si kweli Tanzania haijawahi kuwa nchi ya kijamaa hata siku moja. Bali ni nchi iliyojaribu kujenga ujamaa wake na mambo yote ya kujenga mfumo huo hayakufanyika.

Katika hotuba yake ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Augusti 5, 1967 (miezi michache tu tangu kutangazwa kwa Azimio la Arusha) Nyerere alisema hivi kutukumbusha kuwa Azimio lilikuwa ni lengo –wazo.

“Azimio la Arusha ni azimio la shabaha tu, basi. Azimio hilo linatamka lengo TANU itakakowaongoza watu wa Tanzania, na linaweka shabaha za maendeleo. Tanzania haikuwa nchi ya Ujamaa ghafla siku ile ile ya tarehe 5 Februari, au siku yoyote tokea hapo wala kwa sababu hiyo tu Tanzania haijawa nchi yenye kujitegemea, au nchi iliyoendelea.

"Azimio la Arusha lisingeweza kufanya mambo hayo siku hiyo hiyo wala isingewezekana hata kama watu wangekuwa na ari na nguvu kiasi gani, kutimiza shabaha hizo katika miezi michache hii tangu Azimio lipitishwe na TANU.” Na akasema hapo hapo kuwa “Azimio ndio mwanzo, si mwisho, wa safari ndefu sana ambayo bila shaka itakuwa na matatizo mengi”.

Hivyo waasisi wetu walitambua hivyo. Ndiyo maana wengine tunashangaa kuwa watu wale wale ambao waliunga mkono Azimio leo hii hata kulitamka kwenye midomo yao wanashindwa. Hakuna watetezi wa Azimio.

Ni kama Wamarekani watokee leo hii na kuanza kubeza msingi wa taifa lao yaani Azimio lao la Uhuru. Jamani, Azimio la Uhuru la Wamarekani lilisema “Binadamu wote ni sawa”. Lakini wakati huo huo Marekani ilikuwa na watumwa na wanawake walikuwa haruhusiwi kupiga kura. Usawa uko wapi?

Lakini hawakutokea Wamarekani waliodai Azimio lao litupiliwe mbali kwa sababu ati haliendani na “hali halisi” au kwamba “limepitwa na wakati”. La hasha, bali walijitokeza watu waliojaribu kulikumbusha taifa hilo misingi yake. Watu waliotaka wenzao warudi na kuliangalia lile wazo lililounda taifa hilo. Hadi leo Wamarekani wakubwa na wadogo wanawashwa mioyo yao kwa kusoma Azimio hilo.

Hivyo ndugu zangu – hatuwezi kuielewa Tanzania bila kuelewa wazo liliounda nchi inayoitwa Tanzania. Kuna vitu vilivyoifanya Tanzania kuwa Tanzania na Muungano ni sehemu yake ndogo sana.

Tanzania ni wazo la watu ambao walitaka kuwa pamoja na kujenga aina fulani ya maisha. Hatuwezi na tunachezeana kufikiri kuwa tunaweza kupiga hatua ya haraka ya maendeleo kama Watanzania bila kurudia misingi yetu iliyotufanya tuwe Watanzania.

Ninaposikia ati Watanzania wanaogopa Kuungana na Wakenya ninashangaa, tangu lini? Ninaposikia ati kuna Watanzania wanasema kwa haraka tu “vunjeni Muungano yaishe” najiuliza wameingiwa na kitu gani? Ninaposikia ati kuna Watanzania wanasema “yule asipewe nafasi fulani kwa sababu ni dini fulani au Kabila fulani” najiuliza watu wangu wamepatwa na tatizo gani?

Azimio la Arusha lilisema haya (kati ya mengine mengi).

Binadamu wote ni sawa, leo tunaangalia Watanzania wanachukua sheria mikononi mwao kwa kuwapiga na kuwaua Watanzania wenzao kule Tegeta kana kwamba wao ni Watanzania zaidi kuliko wale waliouawa!

Kila mtu anastahili heshima, leo hii kuna watu wengine wamekuwa majaji wa nani anastahili heshima na nani hastahili. Yaani, hata katika sehemu ya tofauti zetu za kisiasa wapo ambao wamefikia mahali pa kutengeneza uadui na dharau isiyo kifani wakiamini kuwa wao wanastahili heshima zaidi!

Raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili wan chi hii ukiwa kama dhamana kwa vizazi vijavyo – leo hii kufuatilia utajiri wetu tunaambiwa tunapenda sana ujamaa. Ati leo uwekezaji unatakiwa uwe ni ufunguo wa kuwanyang’anya Watanzania umiliki wa utajiri wao ambao ni dhamana yao. Jamani, wanataka kuuza urithi wetu na hawataki waulizwe!

Ndugu zangu hatuwezi kwenda mbali tunakotaka bila kurudia misingi yetu, kuisahihisha mengine na kuiboresha mingine lakini kuna misingi ambayo ilifanya Tanzania kuwa Tanzania na hiyo ilitangulia hii nchi tunayoita Tanzania. Wale wanaobeza Ujamaa ni kwa sababu hawajawahi kuusoma na kuulewa. Hata watu wanaozungumzia ujamaa wengine wanadanganya wakifikiri tunazungumzia kitu kile kile.

Ni kwa sababu hiyo ni muhimu kuanza kurudi nyuma na kuelewa Tanzania kama wazo kwani ni hapo tu ndipo tutaweza naamini kufikiria ni namna gani tunaweza kujenga taifa la kisasa kwa haraka zaidi. Bila wazo la kutuongoza au shabaha watawala wetu watakuja na maneno mengi ya hadaa na kujaribu kutuburuza.

Turudi kwenye msingi.
Tuelewe kwanza Tanzania kama wazo. Je, ilikuwa ina maana gani kuitwa Mtanzania? Je, Tanzania ilijitofautisha vipi na mataifa mengine ya Afrika? Kwanini ilikuwa ni fahari kubwa kuitwa Mtanzania?

Nasubiri kwa hamu kuona mdahalo wa kisomi ambao utajaribu kugusia mambo haya na kutukumbusha jinsi Utanzania ulivyokuwa tunu ya kututofautisha na watu wa mataifa mengine.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndugu hii thread na ile nyingine ya Tanzania kama wazo mbona naona ni moja. Mzee ungeondoa hii tukachangia kwenye ile ya MMM
 
Ahhhhhh......jamani mimaandishi yote hiyo!...mnataka tusifanye kazi zingine?....
 
Mzee nashukuru kwakuleta utetezi wa Tanzania kwenye mahakama ya wana wa tanzania ambao ndiyo wenye hatima ya mwisho kuamua kuishi kama watanzania tofauti na mataifa mengine yeyote mazuri na mabaya kwa mtizamo wa kila mmoja wetu; lakini utanzania wetu ni upi? Swali zuri ulilouliza kwetu sote nasi tuamue kama tumeamua kuuza utu wetu kama taifa na hivyo kukosa sura itakayotutambulisha sisi kama sisi kwa jina tulilojipa la Tanzania.

Binadamu yeyote asiyejitambua huishi kwakuangalia sura za wengine na mara nyingi kuishi kwakujilinganisha na wenzie bila kufahamu kuwa duniani kila mtu aliumbwa kwa sura na mfano wake huku sote tukifanana na kwa sura na mfano wa Mungu; kwamba hatufanani kwa monekano lakini bado sote tunaungana katika mambo ya msingi moja likiwa hitaji la kupenda na kupendwa; kuwa hai (hii ina maana kubwa lakini kwa uelewa wa wengi, lakini tunaweza kuvijumuisha katika kula japo vyakula vitatofautiana; kulala japo vitanda na nyumba zitatofautiana; Kuvaa ili kujisitiri kwa baridi na vimelea vya magonjwa na pia aibu ambayo jamii husika imetengeneza kwa utamaduni wake vyote hivi vikikazia maana ya UHAI) na la mwisho uwezo wa kuumba (Ubongo na viungo vya uzazi) yaani ubongo unaweza ukaumba vitu vya kutumia na kurahisisha maisha kwajinsi mbalimbali na pia kuumba mfumo wa utawala ambapo kila mmoja atakuwa na sehemu ya kuwajibika ili kusitokee migongano katika maisha na hivyo kuwa na utaratibu rasmi unaokubalika kwa faida ya kila mmoja. Mfumo wakwanza ukiwa familia yenye baba mama na watoto ambapo hii tulipewa kama mfano wa jinsi ya kutumia ubongo na viungo vyetu vya uzazi katika mfumo wa kwanza kabisa kuwepo tangu kuanza kwa dunia. So utaona japo sisi tutofauti sana katika sura na pia katika utendaji ambao unaonyeshwa na matokeo ya maisha bado tuna fanana na Muumba wote tukiwa na sifa tatu upendo; Uhai na uwezo wa kuumba.

Kama vidole finger print inavyoonyesha hatuwezi kufanana hata siku moja na hivyo hakuna siku hata moja Ame atafanana na Mzee mwanakijiji hata akijitahidi vipi kumuiga na kuisahau sura yake ya asili. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa familia zote duniani hakuna hata moja inafanana na nyingine kwakila hali kila moja ina watoto wenye sura tofauti; zingine zina wake na waume wengi etc etc. huu ukiwa ukweli wa institution yakwanza katika maendeleo ya mwanadamu sijui kama itaingia akilini kuwa Tanzania kama nchi na hivyo institution (State) itakaa ifanane na nyingine yeyote duniani na kama hili ndilo jibu je sisi sura yetu inafananaje? Je dunia itatutambuaje tukitaka kuhesabiwa ama kuitwa katika mambo ya dunia? Tunaweza badili jina kwa herufi zake lakini sisi kama kundi la watu tuliojikuta katika sehemu moja ya dunia tusipoamua kuwa na jina litakalotutambulisha kila mmoja wetu kila tuendako tutakuwa tumeamua kujiua katika sura ya dunia nakubakia misukule isiyoelewa chakufanya zaidi ya kupelekeshwa na wale walioamua kutufanya misukule.

Ni vyema sasa kama taifa tukatambua kuwa jukumu la kuji identify si la mtu yeyote nje ya wale tuliojikuta kwakupenda ama kutopenda kuitwa watanzania katika ramani ya dunia. Njia pekee ya kufanya hivi ni kutambua kuwa tuna sifa hizi tatu tulizopewa bure na mwenyezi Mungu/Nature AKILI/Ubongo UHAI na ili tusigeuke kuwa Wanyama Upendo ambao unatutofautisha na hao. Tukiweza kuvitumia hivi vitatu kwakuwa kila mtu na hivyo kundi kilipewa kwa kipimo chake basi hatimaye tutajenga taifa litakalo kuwa na Jina tena jina litakalotambuliwa na kila mmoja duniani. Lakini kinyume chake pia tutakuwa na jina ambalo pengine halitatufurahisha ila ndivyo jinsi tutakavyokuwa yaani kama baba wa Taifa alivyotabiri wanyama ndani ya Zoo inayoitwa Tanzania na watalii toka sehemu na sehemu watatamani kuja kutuona kwajinsi tutakavyokuwa tunaishi katika sehemu hii ya dunia.
 
Kuzaliwa kwa taifa aina maana watu wote waliopo ndani ya hilo taifa lazima waone kutumia the same ideology. Ndio maana kuna siasa ndani ya taifa hili viongozi wa- represent hayo makundi yenye tofauti hiwe namna ya uchumi unavyoendeshwa, dini, utamaduni na mengineo.

Kusema kwamba Azimio la Arusha ni msingi wetu kama watanzania wote is just simple and portrays authoritarian thinking. You give the 'majority voice' a chance to implement (not to forget during the birth of Azimio la Arusha most of Tanzanian didn't have any voice nor choice) lakini that doesnt imply it is a permanent voice. The world as moved on since the birth of Azimio la Arusha, science has developed and socialism as proved to be a system of failure beyond any reasonable doubt on its own.

People are not equal in many aspects, people vary in choices, production can not be dictated by few as it proved to be impracticle on maintaining production efficiency and allocating resources. In the long run you either over produce or under produce.

The sooner we realize ujamaa or whatever it is we want to label it, like many before us who had attempted to implement the mode or theorize it and had coined their own terms for it, is a system bound for failure.
 
Hivi wakati ule mtu aliposema mimi ni "MTANZANIA" iliendana na vitu gani? Je Watanzania walikuwa na tofauti gani kimtazamo na Waafrika wengine?
 
mao.jpg
Tanzania naigawa katika vipindi vitatu!
1.1964-1966:
Uhuru wetu hauwezi kuwa safi mpaka africa yote imekuwa huru,pan-africanism bila kujali ni mfumo gani wa kiuchumi nchi nyingine za kiafrica zinaufuata,tulitaka muungano wa nchi za kiafrica(since our independence).China na ujerumani mashariki walikuwa na interst kubwa na zanzibar na waliitaka iwe nchi ya kikomunisti na waliwaunga mkono Hanga na Babu(umma party).
2.1966-1991:
Baada ya kutembelea China,mwalimu alivutiwa sana na mfumo wao wa kiuchumi.Mwalimu alivutiwa na mawazo ya mao na akaamini kuwa tanzania inaweza kufanikiwa ikifuata mfumo wa uchumi wa kijamaa kama wa China,hapo ndio ujamaa ulipoanzishwa.
1991-todate:
Kwa sababu malimbali,mfumo wa kijamaa kama wa china haukuwezekana.Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mfumo holela wa kiuchumi.
Kuhusu muungano,uchumi wetu mbovu unatufanya tuangalie options nyingine kama vile kuuvunja au kufufua nchi ya Tanganyika.Ni umasikini,ubinafsi na uroho ndio unatufanya tuuhoji muungano.
 
MM Mwanakijiji

natanguliza heshima za dhati kwako wewe, kwa ufahamu wako, uelewa wako mkubwa na uwezo wako mkubwa wa kufikiria, kuchambua na kuainisha mambo, na mwisho kuandika kwa ufasaha na upembuzi yakinufu sana. hakika wewe ni mkali.

Kwa great thinkesr wa ukweli, nasema kwamba makala yako inatosha sana kumpa mtu urais na inatosha sana kumuwezesha kutengeneza nchi yake na kuipatia maendeleo makubwa sana kiuchumi na kitechnolojia kama dunia ya leo inavyotaka na zaid ya hapo, kwa maana ya kule kunapokuja ambapo kwa sasa ni kwa kufikirika (imaginatory).

unajua Mwanakijiji, FUTURE ni wazo, ni ndoto, si kwa nchi tu, bali hata mtu binafsi ( an individual). FUTURE ni malengo thabiti ya muda mrefu na hufikiwa tu kama ufuatiliaji na utendaji wa malengo yale ya msingi unafuatwa bila kuyumba, kukata tamaa, na bila kubadilishwa badiliswa hovyo. Unajua Mwanakijiji, kUBADILIBADILI MAWAZO MARA KWA MARA kwangu mimi NIKUSHINDWA, sisi mpaka sasa tumeshindwa, au niseme viongozi wetu mpaka sasa wameshindwa, wamepoteza uelekeo, wazo la msingi hawalikumbuki, aidha ni kwa sababu wako shallow kwenye hilo, au wamedandia treni kwa mbele au la hamana nia thabiti.

Lakini kwa watanzania ninavyowajua, si watu makini sana kwenye mambo ya msingi, si watu wanaopenda kusoma, si watu wanopenda kazi, na watu wa juu ju sana, na hili ndio tatizo kubwa sana. Kinachotakiwa hapa kwetu, ni kubalisha fikira za watu, kubadilisha tabia za watu, kubadilisha mienendo ya watu na imani zao. Wakati nachangia makala yako hii hapa, nilisema tu makala yako ni ndefu, mtu mmoja alietaka kujua unazungumzia nini akasema nisimtumie yeye huwa hasomi makala ndefu, umeliona hili.

Mwanakijiji, ni muda sasa nasoma makala tofauti tofauti za wana jimii fourums na namna wanavyochangia makala zinazoanzishwa humu, naweza kusema hivi, jamiiforums haina GREAT THINKERS KAMA SLOGAN YENYEWE INAVYOSEMA, the only GREAT HINKER HUMU NDANI NI WEWE, naomba pia utumie uwezo wako huo kuwabadili wanajaimii forum wenzangu ili wawe GREAT THINKERS WAUKWELI ili na wakawabadili watanzania wengine, MUNGU ATASAIDIA TUTAFANIKIWA.

Umeomba tuchangie katika wazo la msingi,mimi sio mtu wa art, sikusoma sana historia darasani, na sehemu nyingine pia, sina data za kutosha za kuchangia, ila kwa makala yako, nitaongeza sana spidi ya kupitia vitabu kuanzia sasa, ahsante sana.
 
Back
Top Bottom