CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,920
Kuna gogo la muanga, njiani limeanguka
Waja mafundi kuchonga, kibanzi kutobanjika
Watu wavunjika nyonga, kwa kupanda na kushuka
Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala
Waja wenye mbinu zao, hupanda wakadunguka
Waja na wavamiao, kwa papara na haraka
Wako pia waliao, gogo lipo lawacheka
Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala
Letu sote gogo hili, kilitaka lakutaka
Afanyae hatambuli, mja huyo asumbuka
Thamani yake ni ghali, wala hili si dhihaka
Kula ajaye na shoka, katu hawi seremala
Hili gogo madhubuti, si rahisi kukatika
Tukishindwa tukaketi, bandu mwisho hubanduka
Tukikosa jizatiti, gogo litaja anguka
Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala
Bandu humaliza gogo, hilo sheti kukumbuka
Tusijitie mikogo, kudharau kila shoka
Tusilikimbie zogo, pembeni jema kuweka