utendaji katika sekta ya umma ni wa maagizo zaidi

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,368
3,814
Nime 'observe' kwa muda sasa na kugundua kuwa ndani ya sekta ya umma hasa katika ngazi za maamuzi utendaji unazingatia zaidi maagizo;
hakuna new innovation. mfano katika ngazi za mtaa/vijiji, kata tarafa na hata wilaya viongozi husubiri maagizo kutoka ngazi za juu ndipo utaona wakikurupukia walioko ngazi za chini. fanya hiki, fanya kile. pia utendaji ni mtindo wa dharura. utona kipindi kirefu kinaweza kupita mabo yametulia tu mra utaona ghafla msukumo wa kufanya jambo fulani ambalo msingi wake ni maagizo toka juu.
tukitaka kuendelea haraka ni lazima kila kiongozi katika ngazi yake awe na vision na mikakati ya kufikia hiyo visio akishirikiana na wale anaowaongoza. vision na mikakati ni lazima viendane na sera za taifa kama vision 2025 na malengo ya milenia.
ushahidi wa yangu ni mfano ha harakati mbalimbali kaama operesheni usafi, ondoa kipindupindu n.k mfano akitokea mkuu wa mkoa ambaye anasisitiza usafi utaona walioko chini wanvyohangaika. akihamishwa na mikakati inahama. karibu idara nyingi za serikali katika ngazi mbalimbali zinafanya kazi kwa mtindo huu
hapa dar es salaam kwa mfano katika shule za msingi kuna mamia ya walimu wenye stashahada shahada ya kwanza na ya pili akini wakurugenzi na maafisa elimu wako kimpya hawajui hata wawafanye nini walimu hawa wakati shule za sekondari hazina walimu wa kutosha wenye sifa. kwa nini wasiwe majasiri wakafanyan internal reallocation? kwani si wanabaki katika halmashauri hiyo hiyo? wanasubiiri maagizo kutoka wapi? tutafanya kazi kwa maagizo pekee mpaka lini? ikiwa raisi atakuwa hivo je itabidi asuburi maagizo kutoka wapi, mbunguni au? Acheni kuwachosha viongozi wa kitaifa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom