Utekelezaji wa ahadi za CHADEMA waanza rasmi huko Arumeru

sio nguvu ya soda?nakumbuka Mnyika alivyoanza sasa anaanza kupotea
 
Arusha itakuwa chachu ya kuikomboa na kuleta mabadiliko chanya ktk Tz. Hongera Nassari, hongera Chadema, hongera wananchi wa Arumeru East!
 
Dar kubadilika Itachukua muda sana siina waswahili na waswahili ni watu hawafikirii mbali
 
Hakuna blah blah tuko nyuma sana imagine 50 years of uhuru bado twaongelea madawati,mgao wa umeme,maji safi na salama,dawa za 5billion zimexpire zikiwa bandarini kusubili procedures za kuzitoa etc
Wakati wenzetu wanatembea inabidi sisi sio tuu tukimbie bali kukodi treni ya umeme ya kutufikisha tunakotakiwa kuwa
 
.....ila inafaa kutoa elimu kuhusu kazi ya Mbunge, ndio maana watu wanaona bora kuchagua mafisadi wakidhani kuwa watatumia fedha zao binafsi kutatua matatizo yao ya kila siku. Wanaamka mapema kupanga foleni ya kuomba misaada, wanatoa magari kwenye misiba na ubani ndio yanaishia hapo, akina Abood, Mohd Dewji, Lowassa, Chenge et al....
upo sahihi kabisa ndugu.siku moja nilikuwa dodoma kwenye msiba mmoja nikawasikia wababa watatu wakisema eti wabunge wote wangekuwa kama mhe. fulani basi tanzania ingekuwa na maendeleo sana na kwamba wanatamani kama mhe. huyo angekuja kugombea kwenye jimbo lao (dodoma mjini)eti kisa tuu huyo mhe. alitoa mabasi yake mawili hapo msibani.kwa hali hii kweli tutafika jamani!!???
 
katika hali inayotafsiriwa kuwa chadema wamejipanga katika kuleta mabadiliko katika jimbo la arumeru mashariki,utekelezaji wa ahadi za mbunge mteule kutoka cdm bw. Joshua nassari umeanza rasmi hata kabla ya kuapishwa kwake.
Taarifa zilizonifikia kutoka kwa wakazi wa meru ni kuwa visima vya maji vimeanza kuchimbwa.

Nadhani nape nnauye anahitaji kupata taarifa hii kutokana na ushauri alioutoa kwa cdm.

Hongera josh nassari!
Vingapi mkuu?
 
Vingapi mkuu?


Idadi itakusaidia nini? Unatakiwa ujue kuwa visima vimeanza kuchimbwa Arumeru Masharikia. Hii ni Aibu kwa serikali ya ccm ambayo imekuwa madarakani kwa miaka 50 lakini hawakuwa na hiyo idea ya kuwasaidia wana Arumeru. ccm yao ni kupiga makofi kwa kuwapongeza walowezi waliokwapua ardhi ya wazalendo.

Mwulize Kikwete kuwa walikuwa wapi na kwanini hawakuchimba visima?
 
Nadhani roho hii iendelee milele..tusiwape nafasi Chama Cha Matusi aka CCM ya kuongea.
 
Pro-Chdema mbona mnaporomosha matusi yaani mie kuuliza visima vingapi mnachimba limekuwa kosa!
 
Idadi itakusaidia nini? Unatakiwa ujue kuwa visima vimeanza kuchimbwa Arumeru Masharikia. Hii ni Aibu kwa serikali ya ccm ambayo imekuwa madarakani kwa miaka 50 lakini hawakuwa na hiyo idea ya kuwasaidia wana Arumeru. ccm yao ni kupiga makofi kwa kuwapongeza walowezi waliokwapua ardhi ya wazalendo.

Mwulize Kikwete kuwa walikuwa wapi na kwanini hawakuchimba visima?

Mungi,
Wanaotakiwa kujua idadi ya visima vitakavyochimbwa ni Chadema peke yao?
 
Hatimaye ritz aweka heshma kwenye pipoz pawa,magamba hamia pipoz pawa upate uhondo,chadema ni 8 by 8 by 6,but nyie magamba ni 2 by 2 by 4 hamuuwez mzk wetu sisi n mwendo mdundo kaka!,ona aru mash tumeshaanza kutekeleza ahadi kwa vitendo tofaut na nyie wachumia tumbo na maneno(matusi)majukwaani.Hongera mhe. Nassari kwa kuchimba visima!
 
dhamira ya dhati ya kiongozi ni kuwatumikia wananchi wake,dhamira ya dhati ya fisadi ni kuwanyonya wananchi mpaka damu ya mwisho.Hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya watu hawa wawili.Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Mafarisayo wana wezo mkubwa wa kuongoza lakini hawapendi ,wanapenda muda wao mwingi kuutumia kushughulika na falsafa.Aina hii ya mafarisayo tunao wengi lakini mfumo wa kimangimeza ndiyo usiopenda kuwapa nafasi watu hawa kuonyesha uwezo wao wa kuongoza.Kuongoza ni kuonyesha njia ikiwa watu wana zaidi ya miaka hamsini hawakuweza kuonyesha njia leo ndani ya miaka michache kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 wataweza nini kama si kutafuta pensheni kwa ajili ya kuja kuwahonga wananchi 2015 ili wachaguliwe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom