Makyomwango
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 322
- 79
Wanabodi, tumeshuhudia na kujionea wenyewe mawaziri wakichukua maamuzi mbalimbali dhidi ya watendaji wakuu wa mashirika yaliyo chini ya wizara husika. Alianza Mwakyembe ATCL, akaja Kigoda na TBS, akafuata Profesor Mhogo na TANESCO na sasa tena Mwakyembe na Bandari.
Kwa wakati wote huo mawaziri hawa wamwkua wakichukua maamuzi mazito dhid ya watendaji wakuu huku wajumbe wa bodi wa taasis husika wakiachwa na kuendelea na majumu yao. Nijuavyo mimi, taasisi za umma hukabidhiwa kwa bodi za uongozi ambazo pamoja na mambo mengine zinatakiwa kufanya yafuatayo
Haya ni majukumu makubwa sana kwa bodi hizo na hivyo ufisadi unapotokea katika taasisi, ni wazi kuwa wajumbe wa bodi hizo wanakuwa hawajatekekeleza majukumu yao ipasavyo. Naamini kwamba kama tungekuwa na wajumbe wa bodi za uongozi wazalendo, walio makini na wenye uchungu na taasis hizo kamwe ufisida usingejipenyeza kwenye taasisi.
My Take
Kuchukua maamuzi magumu dhidi ya watendaji wakuu wa taasisi zilizovulunda na kuwaacha wajumbe wa bodi za uongozi kuendelea na majukumu yao waliyoyashindwa kuyatekeleza ni kuendeleza uozo ndani ya taasisi husika. Ni vyema bodi hizo zikavunjwa na ikiwezekana sheria zinazounda taasis hizo zirekebibishwe ili wajumbe wa bodi hizo nao waweze kuwajibishwa taasisi zao zinapovurunda.

- Kutunga na kusimamia sers za taasisi
- Kusimamia uongozi wa taaasisi na kuhakiki kuwa mipango mikakati ya taasis hizo inaandaliwa na kutekelezwa kwa ufanisi wha hali ya juu
- Kuudhibi uongozi wa taasisi pamoja na mali za taasis
- Kuteua watendaji wakuu wa taasis husika