Utata Watawala SMS Za Simba Na Yanga

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20


Mwenyekiti wa Yanga Iman Madega
Thursday, September 24, 2009 3:13 PM
LICHA ya Kampuni ya Push Mobile Media Ltd kusema iko katika mchakato wa kuzilipa klabu za Simba na Yanga fedha zilizopatikana kutokana na huduma za ujumbe mfupi wa 'Fan Club' unaotoa taarifa mbalimbali za klabu hizo kongwe nchini, utata umelizunguka


Uchunguzi uliofanywa na gazeti moja la kila siku umebaini kuwa pamoja na mikataba kuingiwa, lakini bado kuna utata wa malipo kamili kwa fedha zilizopatikana.

Viongozi wa klabu hizo mbili kongwe nchibi, Simba na Yanga wamekuwa wakikwepa kulizungumzia hilo.

Kwa mujibu wa utaratibu huo, kila mwanachama au shabiki wa Simba au Yanga amekuwa wakikatwa sh150 kwa kila ujumbe anaopata.

Taarifa za awali zilisema kuwa, kutokana na mpango huo, klabu ya Simba imeingiza wanachama na mashabiki 30,000 wakati Yanga ni 14,000 waliojisajili.

Kwa utaratibu uliowekwa, Simba na Yanga wanapata sh50 kwa 'meseji' moja kati ya sh150 na sh 50 nyingine inakwenda kampuni ya simu ambayo mtandao wake umetumika na nyingine inaingia Push.

Mitandao ya simu ambayo imekuwa inatumika ni Zain, Vodacom, Tigo, TTCL, Sasatel huku wakiratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA.

Yanga inatarajia kuvuna sh. 700,000 endapo meseji zote 14,000 ziliwafikia mashabiki na wanachama wake waliojisajili katika huduma hiyo, lakini fedha hizo zitakuwa zaidi endapo wanachama na mashabiki hao 14,000 watatumiwa ujumbe mara nyingi .

Kwa upande wa Simba ambayo imepata wanachama na mashabiki 30,000 na kutokana na makato hayo kwa mtu mmoja na sms moja, Simba inaingiza shilingi milioni1.5 na pia itakuwa zaidi endapo watu hao watatumiwa ujumbe huo zaidi ya mara moja.

Hata hivyo, Afisa Mwandamizi wa Kampuni ya Push Mobile, Rahim Kangezi alisema kuwa mabadiliko ya uongozi wa timu hizo kubwa ndiyo kikwazo cha timu hizo kupata fedha hizo. Hata hivyo, hakukuwa na mabadiliko makubwa katika klabu hizo katika siku za karibuni.

Afisa huyo alikiri kusema kuwa wapo katika mchakato wa kuzilipa timu hizo kwani, malipo yake yanatatokana na idadi ya wanachama waliojisajili kwa ajili ya timu zao.

Alisema kuwa walifanya kikao na watendaji wapya wa klabu hizo na kukubaliana njia yakupata malipo yao ndani ya wiki moja.


</SPAN>
 
Back
Top Bottom