Utata wa Tanganyika na Tanzania

Nashukuru sana mtanganyika mwenzangu kwa kuwakumbusha watanganyika wasio elewa utaifa wao. Na pia nina mashaka na wale watu wazima wanao simama mbele za majukwaa na kusema ni uhuru wa tanzania sin ahakika kama akili zao ziko active. Hakika nakwambia mi ntakufa naitambua tanganyika
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?
Nadhani hujaelewa mada kwani hata huko ulaya ulisikia UJERUMANI ikiitwa EU MAGHARIBI au UINGEREZA kuitwa EU KISIWANI au POLAND kuitwa EU MASHARIKI ?????????? Mbona zinaendelea kuitwa kwa majina yao na bado zote zimeungana ktk EU kwa nn Tanganyika ife ndani ya muungano lkn Zanzibar ibakie PANA KANENO HAPO !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:A S 465:
:A S 465:
 
Tulikubaliana tuwauwe mama zetu, mie nikamuua mama yangu Tg! Nilipo gundua mwenzangu mama yake zenj hakumuua bali kamficha! Nikamshauri kuwa lazima amuue mama yake ili wote tuwe yatima, au nami nimfufue mama yangu!
Nilipata jibu la kifedhuli kwamba; "Aliye kufa amekufa usimfufue utahatarisha uhusiano wetu! na mama yangu zenj piga ua hafi mtu! Jibu hata wewe unalo.
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?
mimi sioni faida ya huu muungano naomba nipe mifano na faida zake

mimi sioni faida ya huu muungano naomba nipe mifano na faida zake

Faida ya Muungano kwa ujumla wake haipo. Wazanzibari ndio pekee wenye kufaidika na muungano huu. Huenda mmojawapo atakujibu. Wazazibari ndio wenye haki ya kujiita Watanzania. Wao wana uwezo wa kupata kila wakitakacho Bara na Visiwani. Wanachukua ardhi popote, wanapata madaraka (Mawaziri, wakurugenzi, mameneja n.k.) huku Bara. Wanakuwa na madaraka katika mambo yasiyo ya muungano. Wamejazana katika Bunge la muungano na kushiriki kikamilifu katika mijadala ya yale yasiyo ya muungano. Kule Visiwani (Pemba na Unguja) Mtanzania bara (Mtanganyika) huna chako. Huwezi kuingia Baraza la Wawakilishi, huwezi kuwa kiongozi wa Serikali yao, ardhi hupati, hata ukitaka kuoa huko utawekewa vikwazo utadhani uko uchina. Muungano wa sasa hautufai bila TANGANYIKA YETU. Watanganyika tuungane kupigania nchi yetu tukufu ya Tanganyika. Hakuna suluhu bila Tanganyika. Hakuna nchi iitwayo Tanzania Bara iliyopata Uhuru miaka 50 iliyopita. Tanganyika ndiyo inayoadhimisha miaka 50 ya uhuru!! Hivi viongozi wa nchi hii hawaoni aibu kutukuza nchi ya kufikirika na kuacha nchi yao halisi Tanganyika?
 
Utata wa Tanganyika na Tanzania.

Edson Kamukara

SINA muda wa kupoteza leo isipokuwa naomba tujivue unafiki na kisha kila mmoja wetu ajihoji Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea Uhuru wa miaka 50 ya taifa lipi? Nahitaji jibu la moja kwa moja si siasa za upotoshaji, anayejibu swali hili anapaswa kujiweka katika nafasi ya mtoto mdogo anayepaswa kujua jambo fulani kiundani.

Desemba 9, mwaka 1961, kulikuwa nchi yetu inaitwa Tanganyika ambayo ilipata uhuru wake. Ilipofika mwaka 1964 Rais wa Tanganyika Julius Nyerere na mwenzake wa Zanzibar Abeid Amani Karume, waliona ipo haja ya mataifa hayo kuunga.
Muungano ni kuunda umoja na ushirika wa pamoja lakini nje ya hapo kila mtu anabakia kuwa kama alivyokuwa awali. Hii kwa bahati mbaya sivyo ilivyokuwa kwa huu muungano wetu.

Baada ya Muungano kufanikiwa na kuundwa Tanzania, nchi moja ya Tanganyika ilinyongwa na ikabakia Zanzibar. Na ndani yake zikaletwa siasa za Tanzania Bara na Tanzania Visiawani.

Hivi mtoto wa kizazi cha leo anapohoji kujua ilipo Tanganyika tunaweza kumweleza nini mbali na siasa? Zanzibar ipo Tanganyika ilikufa ikazaliwa Tanzania Bara ambayo kimsingi ndiyo hiyo hiyo Tanzania.

Hii ndiyo historia ya nchi yetu, na tunathubutu kutembea kifua mbele tukijiaminisha kuwa tumekomaa kifikra vya kutosha wakati tunapotosha ukweli kuhusu Taifa letu?

Leo watoto, vijana, watu wazima na mbaya zaidi viongozi kila mmoja anaimba kuwa Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ( Hii ni nchi ipi?).

Zanzibar wana vielelezo vya utambulisho wao kama taifa, wana wimbo wa taifa, bendera, katiba yao, Bunge lao na mengineyo. Nchi inayoitwa Tanzania Bara haina bendera, wimbo wa taifa, Bunge badala yake wanatumia vielelezo vya taifa la Tanzania lililotokana na muungano wa (Tanganyika na Zanzibar).
Hivyo, hata Desema 9 mwaka huu, kinachosherehekewa si miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Maana siku hiyo utaimbwa wimbo wa taifa wa Tanzania, itapeperushwa bendara ya Tanzania, Rais atakuwa wa Muungano, sasa hapa tutasemaje ni uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara kama tunavyojidanganya)?

Hivi ndivyo tumeendelea kujidanganya kwa miaka yote. Tumekuwa na Bunge la Muungano ambalo linawashirikisha wabunge kutoka Zanzibar, kimsingi linapaswa kujadili mambo yale yanayohusu muungano tu.

Lakini kutokana na udhaifu wa muundo wa muungano wetu hata kwenye mijadala ya mambo yasiyo ya Muungano wabunge wa Zanzibar wanaendelea kuwemo wanashiriki kutuamulia wakati kule kwao wana Baraza la Wawakilishi ambalo linajadili mambo yao pekee.
Huu mfumo wa muungano wetu lazima tukubaliane kuwa una kasoro hata kama hatutaki kuambiwa ukweli. Ni bora kujitathmini kuanzia hapa ili itafutwe suluhu ya kuondosha upotoshwaji wa historia ya nchi yetu ya Tanganyika badala ya kuendelea kuzika vichwa mchangani kama kanga tukidhani tumejificha hakuna shida.
Mfano mdogo wa mkorogano huu unajitokeza kwenye michezo hasa kwenye mashirikisho yanayotutambua kama nchi mbili. Kwa sasa hapa Tanzania yanaendelea mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika michuano hiyo Zanzibar wameingia kama nchi, wanatambulika kwa timu yao ya Zanzibar Heroes wakiwa na bendera ya taifa lao na wimbo wao wa taifa halafu eti sisi tumejibadilisha kutoka Taifa Stars tunajiita Kilimanjaro Stars.

Lakini kinachofanyika kwenye timu ya Kilimanjaro Stars ni kile kile cha Taifa Stars, kwani wimbo na bendera wanavyotumia ni vile vile vya Tanzania. Na hata kocha kabadilishwa tu mwaka huu baada ya Wazanzibari kuhoji maana huyo huyo wa Taifa Stars ndiye alikuwa anafanywa wa Kilimanjaro Stars.
Mimi ni mmoja wa waumini nisiyeona aibu kusema kuwa tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, lakini siku hiyo ya Desemba 9 mwaka huu, sitasherehekea maana hakutakuwa na bendera ya Tanganyika wala wimbo wa Tanganyika ili kuniletea hisia za kumbukumbu ya kuachana na ukoloni.

Naogopa sana unafiki na uongo wa kujidanganya kushiriki kuimba wimbo wa Mungu ibariki Tanzania wakati huo bendera ya rangi nne ya Tanzania ikipeperuka halafu nijiaminishe kuwa nimesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Tafakari!
edkamukara@yahoo.com/ 0714717115/ 0788452350

Ufisadi mpaka kwenye Historia ya nchi. Wataendelea kudanganya mpaka lini.

Kamwe hawawezi kushinda, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua.
 
Faida ya Muungano kwa ujumla wake haipo. Wazanzibari ndio pekee wenye kufaidika na muungano huu. Huenda mmojawapo atakujibu. Wazazibari ndio wenye haki ya kujiita Watanzania. Wao wana uwezo wa kupata kila wakitakacho Bara na Visiwani. Wanachukua ardhi popote, wanapata madaraka (Mawaziri, wakurugenzi, mameneja n.k.) huku Bara. Wanakuwa na madaraka katika mambo yasiyo ya muungano. Wamejazana katika Bunge la muungano na kushiriki kikamilifu katika mijadala ya yale yasiyo ya muungano. Kule Visiwani (Pemba na Unguja) Mtanzania bara (Mtanganyika) huna chako. Huwezi kuingia Baraza la Wawakilishi, huwezi kuwa kiongozi wa Serikali yao, ardhi hupati, hata ukitaka kuoa huko utawekewa vikwazo utadhani uko uchina. Muungano wa sasa hautufai bila TANGANYIKA YETU. Watanganyika tuungane kupigania nchi yetu tukufu ya Tanganyika. Hakuna suluhu bila Tanganyika. Hakuna nchi iitwayo Tanzania Bara iliyopata Uhuru miaka 50 iliyopita. Tanganyika ndiyo inayoadhimisha miaka 50 ya uhuru!! Hivi viongozi wa nchi hii hawaoni aibu kutukuza nchi ya kufikirika na kuacha nchi yao halisi Tanganyika?

ahaa, ndio sababu wanapenda muungano huu wa serk2! Yaani Tg wameifanya koloni lao au kama nchi waliorithishwa na babu zao!
 
Ki ukweli tunapotoshwa sana na viongozi wetu ambao wanaupigia debe uhuru wa Tanzania,kwani nchi inayoitwa Tanzania ilitawaliwa na nani? Mwl.Nyerere alipigania upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika,sasa hawa wanaodai miaka hamsini ya uhuru wa tz ni kwa mba hata kuhesabu hawajui?
 
Napenda kujuzwa hivi wanzanzibar nao wanasherekea miaka 50 ya uhuru wa tanzania? Ebu warudi ktk historia yao ya uhuru wa unguja
 
Huu uhuru wa tarehe 9 Desemba 1964 ni uhuru wa Tanganyika. Sehemu inayoitwa Tanzania bara ilianza mwaka 1964 mara baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mpaka sasa haijafikisha miaka 50 toka imeanza.
 
Back
Top Bottom