Utata wa magoli ya SIMBA na YANGA mtaani

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
Mechi ya jana isingeonyeshwa watu wangevunjana meno mtaani. Cheki stori za mtaani watu ambao wamesikia kwenye radio tu huku kwetu kusikokuwa na umeme.

'' unajua nini ile ngoma imegonga mwamba ikatoka nje....refa akasema sio goli...laizi meni akamwita akaingiza mkono mfukoni..akampa dola mia tatu...halafu refa akarudi akishangilia akasema mpira uwekwe kati.... kapewa kitu yule...lile sio goli''

'' Hamna lile ni goli, unajua nini...mpira uliingia ukagonga nyavu na kurudi uwanjani''

'' Unajua ile penati sio penati ile....kwa sababu Mwape amekatwa katikati ya uwanja halafu refa akasema ipigwe penati...mi nimeona kabisa kwenye redio.

'' Acha wewe mbona Mgosi alikuwa ameotea kabla hajafunga....mi nimeona kabisa Mgosi peke yake na golikipa na kibendera kiko juu...nimeona kabisa kwenye redio.

'' Ndio hivyo kwanza ule mpira ulimgonga kipa ukarudi uwanjani na refa akaudaka akasema ni goli.
 
Back
Top Bottom