Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Waulize Dr Kashimba alie na Siri aina ya majeraha ambayo hata Familia ilikataliwa kuona, pia Muulize Mzee Kizota yule mwenye Bar viwanja vya Saba Saba, alikuwa bodi gadi yake, wakimbizi waliokuwepo maeneo ya karibu na ajali wanadai kuona bodi gadi huyo akifyatua risasi, muda mfupi tu baada ya mheshimiwa kutoka nje ta gari kujaribu kukimbia. Muulize Mwalimu Nyerere aliekuwa Rahisi wa Tanzania
Mhhh aise mbona hatari
 
Kitu kinazidi kunichanganya ni kua safari za kiongozi kama waziri mkuu kunakua na msafara wa magari kibao yakiwamo ya polisi na TISS unakuta magari mengine yanazuiwa barabarani kupisha msafara sasa kwa huyu sokoine ilikuaje hiyo gark ilimgonga sokoine isizuiliwe kupisha msafara wa mkubwa waziri? au enzi hizo safari za viongozi hazikua na ving'ora? kichwa kinauma.
Tukipata jibu lake mzizi wa fitna utaisha
 
nilikua bado mdogo sana,ila nakumbuka kipindi wanatangaza ndo nilikua natoka RTC kununua sukari ,ndo nikasikia ulikua mshituko na hudhuni sana tulifuatilia mazishi live kupitia RTD.

Kisha nikiwa sec miaka ya 90 tukawa na urafiki na mtoto wa mmoja wa mkuu wa majeshi ambae pia kwao ni butiama karibu kabisa na kwa jk,akawa anatuambia ni siri kubwa ila mwili wa sokoine ulikutwa na jeraha la risasi mgongoni.
Ila sikuwahi kuamini asee.
Daah
 
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati Sokoine kwa vile alipofariki nilikua bado sijazaliwa, nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1. Ajali iliyosababisha kifo cha Sokoine ilikuwa ya aina gani? Kupinduka kwa gari, kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2. Katika hiyo ajali hayati Sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3. Kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4. Kama wako hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4. Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5. Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6. Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7. KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

Kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.
acha kufukua makaburi. JPM atakuzingua
 
Hizo nyingine hisia za watu tu, Sokoine alikufa kwa ajali ya gari full stop.Baadae utakuja na kusema kuna utata na kifo cha amina chifupa ,,,acha mambo hizo.
 
Tunaulizia sokoine lkn kifo cha juzijuzi tu cha balali mpaka leo ni utata .......watu hadi familia yake haikupewa uhuru ktk msiba....
Serikali ilikosa pesa za kumsafirisha kutoka marekani ili azikwe tz
 
Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam

sokoine.jpg


Picha hapo chini ikimuonyesha Baba wa Taifa ambaye naye ni marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa aliyekuwa rafiki yake kipenzi Waziri Edward Sokoine ukiwa umelala milele.

soko.jpg


Sokoine alifariki kwa ajali ya gari Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha!
Hayo mengine ni maswali ya hisia tu ambayo kila mwenye hisia zake moyoni hana budi kujiuliza bt all in all apumzike kwa amani milele!
Alifariki mchana kwenye saa saba hivi. Tangazo rasmi likatolewa na Nyerere jioni kuanzia saa kumi.
 
Nakumbuka ilikuwa ni jumapili ya tarehe 15 April 1984 nikiwa Arusha. tulikuwa kanisani kwenye ibada ya jumapili katika kanisa lilo kando ya barabara ya uhuru ( kwasasa karibu na shoprite) waumini wote tulitoka nje ya kanisa kuangalia mwili wa Sokoine ukipitishwa kuelekea Munduli kwa Maziko, nakumbuka jinsi watu walivyokuwa na simanzi wakati huo
Calvary Temple Assemblies of God
 
images
images

Hapo ndipo kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Moringe Edward Sokoine
Kweli baada ya Kikao cha Bunge kumalizika alikua aondoke na ndege ya Serikali kwenda Dar-es-salaam
Marehemu Sokoine akachagua atatumia Barabara
Heresay: alikuwa kochi la nyuma peke yake na hakufunga mkanda
ajali ilipotokea alirushwa hadi kioo cha mbele na aliummia kifuani sana (km ni headrest ya abiria wa mbele au dreva vilitoboa haya)
Kitu nisichokiamini ni kuwa walimpiga risasi na kumuita Dube eti alipondeponde hilo gari M-Benz mpaka lichakae NO- BIG- NO
Ninachokumbuka nilikuwa Chuoni siku hiyo na tifu ni kuuendeleza msako wake wa WALANGUZI ambao sasa utawavaa viongozi wa juu, wakatihuo alishakatazw kwani alimkamata Waziri Barongo akitaka aswekwe ndani Marehemu Julius Nyerere akamwambia sasa unaifanya kazi visivyo Barongo Mfungulie
Sokoine alikufa kwa ajali ingawa aliuwa na maadui wengi hasa Viongozi wenzake na wale walioupitia Uwaziri mkuu wakiwemo Msuya na Kawawa

sokoine.jpg
Wewe pia umesimuliwa. Kama ni kweli ulikuwa chuo mwaka huo ungekumbuka kuwa hakukuwa na waziri aliyeitwa Barongo. Edward Barongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na ni miongoni mwa waliokamatwa katika sakata la uhujumu uchumi, akawekwa mahabusu na kushitakiwa. Sokoine alipofariki Barongo alikuwa anasota mahabusu. Jamaa za Barongo na watu wengine waliokuwa kwenye list ya uhujumu walishangilia sana waliposikia Sokoine kafa.
 
Back
Top Bottom