Mungu Mweusi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 1,474
- 1,077
Kama una GPA ya 2.3 ulienda chuo kufanya nini? Wewe ndy wa kutandika viboko maana umechezea kodi yetu, na hiyo ni laana labda urudi kulima kwenu SITIMBI.
Shukrani mkuu, wengine wanasema daktari aliye ufanyia postimatamu mwili wa sokoine alisema kua mwili ulikuwa na tundu la risasi mgongoni pia hakuna ndugu wa marehemu aliye ruhusiwa kushiriki kuuandaa mwili wa marehemu,nazidi kuchanganyikiwa hapa.
huyo kijana anaonekana kachoka kachakaa hana hata mia mfukoni hiwezi kumfananisha na riz1 kiuchumi hata kidogo.
Kaka alikufa saa 7 kasoro mchana kweupe nikiwa na miaka 13. Serikali ilitangaza kifo saa 10 jioni mochwari ya morogoro. Maiti ililetwa na land rover 109
Nina uhakika shaka hii iliyopo juu ya kifo cha Moringe Sokoine inathibitisha usemi wa wenye hekima kuwa "PENYE UKWELI UONGO HUJITENGA"
Aliyeanzisha mada hii amefanya vizuri. Ila tu ikiwa lengo ni kupata ukweli utakaolisaidia taifa la sasa na vizazi vijavyo. Dunia ya leo ujanja ujanja hauna nafasi sawa na enzi za ujinga miaka ile ya fikra za mwenyekiti. Ifike mahali ukweli na uwazi uwe ni kitu cha kawaida maana wengi walio na hila na uovu hasa wa kuvuja mali za umma huugopa sana ukweli. Watafanya kila wawezalo kuufunika lakini hilo haliwezekani.
Ukifuatilia utaona hata huu wizi wa fedha za umma BOT tena unaojirudia ni zao la kukwamishwa juhudi alizoanzisha Sokoine. Hii itakuja kuisha ingawa itachukua miaka mingi ijayo. Lakini historia inaonyesha hatua za maendeleo ya kweli na thabiti wakati mwingine hupigwa kwa gharama ya watu kujitolea hata kufa, hasa kwa nchi zilizo gizani huku Afrika.
R.I.P: Sokoine, Korimba, Kombe, Dr. Omary Ally Juma, Dr. Mvungi, Amina Chifupa, kighoma Malima, Karume...loading please wait...
Mkuu mbona ktk RIP zako Mwalimu hayupo!
Mmmhhh so nini pia kilichomuua Horace Kolimba?
Anapatikana wapi leo huyu ProfSababu za Dr Prof Shaba kuwa mlevi wa kutupwa baada ya postmotem.
Huyu Prof Shaba inasemekana hakua mlevi ila baada ya tukio hili alikua kama TBL
Mbona haukuweka huo utata ambao wewe ndio ulibaini?.
Waulize Dr Kashimba alie na Siri aina ya majeraha ambayo hata Familia ilikataliwa kuona, pia Muulize Mzee Kizota yule mwenye Bar viwanja vya Saba Saba, alikuwa bodi gadi yake, wakimbizi waliokuwepo maeneo ya karibu na ajali wanadai kuona bodi gadi huyo akifyatua risasi, muda mfupi tu baada ya mheshimiwa kutoka nje ta gari kujaribu kukimbia. Muulize Mwalimu Nyerere aliekuwa Rahisi wa Tanzania
nilikua bado mdogo sana,ila nakumbuka kipindi wanatangaza ndo nilikua natoka RTC kununua sukari ,ndo nikasikia ulikua mshituko na hudhuni sana tulifuatilia mazishi live kupitia RTD.
Kisha nikiwa sec miaka ya 90 tukawa na urafiki na mtoto wa mmoja wa mkuu wa majeshi ambae pia kwao ni butiama karibu kabisa na kwa jk,akawa anatuambia ni siri kubwa ila mwili wa sokoine ulikutwa na jeraha la risasi mgongoni.
Ila sikuwahi kuamini asee.
Mkuu Head teacher, umenikumbusha. Mimi nilikuwa darasa la 5, shule ya msingi Katwe, kule Karagwe - Kagera. Pia siku hiyo tulikuwa na ugeni shuleni wa viongozi wa CCM kutoka mkoani, namkumbuka Mzee Pius Ngeze (Mwenyekiti wa mkoa) na Bonifas Njohole ambaye alikuwa katibu wa CCM mkoa wa Kagera. Yaani enzi hizo viongozi wa CCM mkoa walikuwa na nguvu kuliko mkuu wa mkoa. Habari za msiba zilijulikana mida ya saana 7 mpaka 8, hakika yalikuwa ni majonzi makubwa sana.
Mengine yote sawa lakini muda alipofariki si 11:30 jioni bali muda wa kati ya saa tano na sita mchana maana nilkuwepo Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu wakati mwili wa Hayati Sokoine unaletwa pale alafu muda kati ya saa saba na saa nane mchana wimbo wa taifa ulipigwa na kufuata sauti ya Mwalimu ikitangaza kifo cha Hayati Sokoine. Hiyo saa 11:30 nadhani mwili wake ulikwa umeshawasili Dar ulichukuliwa kwa ndege ya Jeshi pale Ngerengere.Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar Es Salaam
Picha hapo chini ikimuonyesha Baba wa Taifa ambaye naye ni marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa aliyekuwa rafiki yake kipenzi Waziri Edward Sokoine ukiwa umelala milele.
Sokoine alifariki kwa ajali ya gari Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha!
Hayo mengine ni maswali ya hisia tu ambayo kila mwenye hisia zake moyoni hana budi kujiuliza bt all in all apumzike kwa amani milele!
Duuh hii nayo kali aisee kwa hiyo kachukuliwa msukule? ha ha ha!