Utaratibu wa Watanzania wanaoishi Ughaibuni kushiriki kutoa maoni ya Katiba Mpya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI YAO KUHUSU UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA.

Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

1. 1. MAMBO YA KUZINGATIA
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:

Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tzThis e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ), nukushi + 255-22-2133442
na +255-224-2230769

(ii)Utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.

Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.

(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:
Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).

Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.

Kwa maelezo zaidi bofya: http://www.katiba.go.tz/index.php/maoni-nje-ya-nchi
 
Wanabodi,

Nimekutana na hii taarifa kwenye mtandao wa wenzetu uitwao "wanamabadiliko"

Wakuu,
Tafadhali tembeleeni link kupata mwongozo:

Mwongozo Kwa Watakaotoa Maoni nje ya nchi

MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA
WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI
YAO KUHUSU UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA
_________________________

Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni www.katiba.go.tz

Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

  1. 1. MAMBO YA KUZINGATIA

Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:

(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.

(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:

Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)Utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.

(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:

Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.

Rgds
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800,
Website: Tume ya Mabadiliko ya Katiba

MY TAKE:-

Wenzetu mlio ughaibuni, tumieni hii fursa kwa kuleta maoni yenu ambayo yatakuwa na exposure nzuri ya huko mlipo, ili na`si tupate katiba nzuri kama za huko kwetu wenzetu.

Angalizo: Maoni yanatakiwa kuletwa na Watanzania tuu ambao bado wameuretain Utanzania wao, hii inamaanisha, wale Watanzania kiuhalisia, ambao wamepoteza Utanzania wao kwa sababu zozote zile, hawaruhusiwi kutoa maoni yao kwa kisingizio maoni haya yanatakiwa kutolewa na raia wa Tanzania pekee!.

Kwa maoni yangu, this is not fair, kwa vile serikali ilishaonyesha nia ya kuelekea kwenye dual citizenship, tungeitumia fursa hii kufungua milango kwa kila Mtanzania halisi, regardless ya uraia wake, kutoa maoni kuhusu katiba ya nchi yake bila vikwazo vyovyote au abaguzi wa aina yoyote ili kutowanyima haki hii ya msingi, waTanzania wenzetu ambao wamepoteza uraia wao wa Tanzania, bali mioyo, mawazo na mapenzi yao ni kwa nchi yao halisi ya Tanzania.

Ila pia kwa wale wenzetu ambao mnajijua mna michango muhimu kuhusu katiba mpya, na mmepoteza uraia wenu wa Tanzania, tunaombeni sana, tumeni maoni yenu kupitia ndugu, jamaa na marafiki zenu wenye uraia ili hayo mawazo yenu muhimu, tuyapate!.

Natanguliza Shukrani.

Pasco.
 
Attachments

  • Mwongozo kuhusu Utaratibu wa Watanzania kuishi Ughaibuni.pdf
    219.5 KB · Views: 76
safi sana hii imekaa vizuri...jamani tutoe mawazo yetu tupate katiba nzuri..[SUB][/SUB]
 
Mpokea na mtoa rushwa wapate adhabu ya kifo! thank you!! huio ndio mchango wangu kwa hii katiba mupya.
 
Back
Top Bottom