Utaratibu wa mpya wa kupanga Matokeo ya Sekondari

Kenneth Nzowa

New Member
Oct 30, 2013
3
0
Nichukue nafasi hii kuipongeza wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na serikali kwa ujumla kwa jitihada kubwa za kujaribu kufanya kila liwezekanalo ili kila mtanzania aipate elimu,pamoja na kuboresha elimu yetu kuanzia awali, msingi, sekondari hadi chuo kikuu. Mojawapo ya hatua hizi ni kuchambua na kuweka utaratibu wa kupanga matokeo ya mitihani ya sekondari. utaratibu huu utaweza kubainisha uwezo wa mwanafunzi kwa uwazi zaidi na kumpa nafasi zaidi ya kuendelea na masomo ya ngazi za juu. Mfano Mwanafunzi aliyepata alama 76 kwa 100 badala ya kuonekana B atakuwa na alama A ambayo ni ufaulu wa kujipambanua. Nionavyo mimi ni kwamba baada ya kufanya mabadiliko makubwa haya twende moja kwa moja kwenye michakato ya ufundishaji na ujifunzaji darasani. Hivi sasa hatuhitaji kuwaza kupunguza idadi ya wanafunzi darasani ili wawe 45 kwa mwalimu mmoja. gharama ya kufanya hivyo ni kubwa kuliko unavyo weza fikiria haraka na huenda isiwe na matokeo tarajiwa. Waalimu ni mashahidi, mara ngapi tumefundisha wanafunzi wachache kwenye tuition lakini wakawa na matokeo duni? Lililo mbele yetu ni kupewa kipaumbele kwa mafunzo ya walimu kazini. Ikiwezekana kuwe na sera maalumu ya mafunzo kazini kwa waalimu. Naamini WAALIMU BORA, watajituma, watatengeneza zana za kufundishia zilizokwenye mazingira yao na kwa ujumla watajipa motisha ya ndani(intrinsic motivation) badala ya kutemea motisha ya nje(extrinsic motivation). na watafanya kazi nzuri zaidi Hata kama hawatafundisha vizuri darasani watawafundisha vizuri sana ndugu zao na watoto wao ambao ni watanzania. Jedwali hili ni nukuu kutoka gazeti la Mwananchi la tarehe 1/11/2013
AlamaDarajaMaelezo
75-100Aufaulu wa kujipambanua
60-74B+ufaulu bora sana
50-59Bufaulu mzuri sana
40-49Cufaulu mzuri
30-39Dufaulu hafifu
20-29Eufaulu hafifu sana
0-19Fufaulu usioridhisha
 
Back
Top Bottom