Utaratibu Wa Kuandaa/kuandika Katiba Mpya ya Tanzania

Nenetwa

Member
Jan 16, 2011
14
0
:thinking:Kwa maoni yangu napendekeza utaratibu ufuatao katika kuandaa/kuandika Katiba Mpya ya Tanzania.

Hatua 1:Kubainisha udhaifu/mapungufu yaliyomo katika Katiba ya sasa.Mapungufu hayo yawekwe wazi hadharani na katika maandishi.Watu binafsi,taasisi,asasi,mashirika,wanazuoni,washikadau wote na wananchi wote wapate fursa ya kuyaweka bayana mapungufu hayo kupitia midahalo ya wazi ili wadau na wananchi wengi washiriki.

Hatua 2:Wananchi kupendekeza mambo mapya wanayoyataka yawekwe katika Katiba yao Mpya. Maoni kutoka nchi nzima yaliyotolewa na wananchi wenyewe yazingatiwe.

Hatua 3:Kuundwa kwa Tume Huru ya Wataalamu kutoka kila kona ya Washika dau, itakayofanya uchambuzi,tathmini na majumuisho ya maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wananchi wote. Wataalamu kutoka Vyama vya Siasa, Vyombo vya habari, taasisi na asasi za Kiraia, wanasheria, wanazuoni, vyama vya wafanyakazi, wawakilishi wa wananchi wa kawaida, kwa kifupi namaanisha kila kona itoe mwakilishi/wawakilishi wake katika kuunda Tume hiyo ya Katiba Mpya.Kupitia maoni hayo ya wananchi,Tume hii itaandika/itaandaa Muundo wa Mfano wa Katiba Mpya.

Hatua 4
Kurudisha Muundo wa Mfano wa Katiba kwa Wananchi, ili wausome,wauelewe,waujadili na wajiridhishe kuwa yale yaliyoandikwa ni yale waliyoyataka yaandikwe katika Katiba hiyo Mpya. Kama kuna mapungufu watoe maoni tena, na kama kuna makosa yafanyiwe marekebisho. Wakiridhika basi Mfano huo wa Katiba urudishwe kwenye ile Tume iliyoundwa Mwanzo Kwa ajili ya maboresho,marekebisho,masahihisho. Yote haya yazingatie matakwa ya wananchi.

Hatua ya 5:
Kuandika/Kuandaa Katiba Mpya. Baada ya masahihisho, maboresho,marekebisho ya ule mfano wa Katiba, mchakato wa kuiandaa na kuiandika Katiba Mpya iliyosheheni Matakwa ya Wananchi wote ufanyike.

Hatua 6: Katiba mpya itakayoandaliwa/kuandikwa ichapishwe kwa wingi na igawiwe bure kwa wananchi,angalau kila kaya iwe na nakala moja ya hiyo Katiba Mpya.Ili kila mwananchi wa rika zote aweze kujua sheria mama ( Katiba) inayomuongoza.

Nimesisitiza ushirikishwaji wa Wananchi wote katika kila hatua ili kuondoa uwezekano wa kundi la watu wachache kujihodhisha, kujimilikisha vipengere ndani ya Katiba Mpya,vitakavyowalinda na vitakavyowafanya watetee maslahi yao ya wachache yasiyo na manufaa kwa wengi na kupuuza ya Wananchi walio wengi.

Haya ni maoni yangu kuhusu utaratibu wa kuandaa Katiba mpya ya Tanzania. Jisikie Huru kunikosoa,kuongeza pale nilipoonesha mapungufu na kutoa maoni yako juu ya utaratibu mwingine bora wa kuandaa Katiba Mpya ya Tanzania yenye kushirikisha, kutetea na kusimamia maslahi ya wananchi wote.

KARIBU!
 
Back
Top Bottom