Utapeli wa serikali kwa watafiti nchini

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
katika kile ninachokiona kama utapeli uliokubuhu wa serikali ya CCM kwa vile hawana kitu cha ukweli cha kushikia na ni maisha waliyoyazoea kudanganya....hivi karibuni ilitoa waraka kwa vituo na taasisi za utafiti juu ya maboresho ya mishahara ya watumishi wa kada ya utafiti. waraka huo unasema unaanza kutumika Julai mosi,2010. Kutokana na utafiti nilioufanya kutoka reliable sources za wizara ya kilimo na mifugo ambazo ndio zina watafiti wengi, hii ni changa la macho...ni siasa tupu.

Inasemekana wanaopata mshahara huo mpya ni kama robo tu ya wanaostahili-wengi wao wakiwa wale vingunge yaani maafsa ngazi za juu sana kama vile Principals na Seniors Research Officers. Vijana wengi wa chini wanaonekana wakilandalanda kila leo kwa maafisa utumishi wizarani mwao na ofisi ya rais-utumishi au hazina kuulizia bila majibu ya kuridhisha.

inasemekana baada ya maboresho hayo, maafisa wa juu wa wizara zenye watafiti, walijaribu kuchomeka ndugu na watoto zao katika post za watafiti hata kufanya zoezi hili kuvurugika. Habari nilizopata jana zinasema kwamba ile ni danganya toto watu wapate kuchota pesa za kampeni ili hesabu hazina i-balance kwamba kiasi fulani kimeenda kwenye mishahara hii mipya!!!
 

Attachments

  • WARAKA MPYA UTAFITI[1].doc
    205.5 KB · Views: 61
Back
Top Bottom