Utapeli wa Majembe Auction Mart - A true Story

Mkuu pole sana....
Hii ndo bongo tambarare....
Jamaa wanakua wanajua kabisa kwamba watu wana mambo mengi ya kufanya na muda ni mdogo...then wanatumia sheria mbovu kukuchelewesha, ila uone njia pekee ni kutoa rushwa....
Isingekua jambo la ajabu kama pia ungeenda hadi jiji kukuta mhasibu 'katoka kidogo'...then ukaambiwa uende kesho asubuhi....na ukienda kesho...kule majembe wanakudai ulipie gharama za maogesho...!

Mkuu, hiyo ni kweli kabisa na ndio maana nasisitiza taratibu za ukamataji na utoaji faini uwekwe wazi ili kuondoa mchezo mchafu namna hii. Hawachelewi kukwambia muda wa kazi umeisha njoo kesho na hiyo kesho unadaiwa hela ya za maegesho na ulinzi!!! Kwa kweli wanaohusika inabidi waiangalie hali hii na kurekebisha la sivyo tutakuja kusikia mtu amefumuliwa kichwa kwa risasi kwa sababu ya ujinga wa namna hii.

Tiba
 
Inaudhi sana, ni dalili ya serikali kuishiwa,haiingii akilini serikali yenye vyombo vyote kufikia hatua ya kutumia madalali (Majembe na Yono zote asili yake Iringa) kusimamia/enforce sheria za serikali kuu,jiji,mamlaka ya mapato nk. Luhanjo nn at work maana kama huyo Kevela owner wa Yono wanatoka wote Wangingómbe
 
Inaudhi sana, ni dalili ya serikali kuishiwa,haiingii akilini serikali yenye vyombo vyote kufikia hatua ya kutumia madalali (Majembe na Yono zote asili yake Iringa) kusimamia/enforce sheria za serikali kuu,jiji,mamlaka ya mapato nk. Luhanjo nn at work maana kama huyo Kevela owner wa Yono wanatoka wote Wangingómbe

Mkuu,

Ni jana tu nilifanyiwa huu upuuzi. Next time wakiingia kwenye anga zangu I will teach them a reason na ninachofikiria kukifanya kitaifanya serikali nzima kushtuka na ku-revise huu upuuzi. Hatuwezi kufanywa watumwa wa mafisadi kwenye nchi yetu wenyewe. Enough is enough!!!!!

Tiba
 
Mkuu,

Ni jana tu nilifanyiwa huu upuuzi. Next time wakiingia kwenye anga zangu I will teach them a reason na ninachofikiria kukifanya kitaifanya serikali nzima kushtuka na ku-revise huu upuuzi. Hatuwezi kufanywa watumwa wa mafisadi kwenye nchi yetu wenyewe. Enough is enough!!!!!

Tiba

mbona pale mwenge wamefunga, jamaa bado wapo kweli? mia
 
Mkuu hii sirikali yetu imeshashindwa kazi, hapa mkoani kilimanjaro hao majembe wamepewa kazi na TRA yakukamata bodaboda ambazo hazijalipiwa mapato. Wakikamata pikipiki wanapeleka ofisini kwao na si TRA. Ukienda ofisini kwao wanakwambia tukuandikie karatasi ukalipe TRA SH 75,000, au utulipe sisi sh 40000 tukuachie. Yaani haka kanchi watu wamegawana sehemu za kula, siku wakikamata bodaboda yangu ntaonesha mfano ndipo TRA watajifunza kuwa walichokifanya ni ujinga
 
Wana JF,

Nina leta taarifa hii kwenu ili kama kuna wahusika watasoma hapa basi wachukue hatua zinazostahili. Mchana huu nilipaki gari maeneo ya immigration karibu na jengo la UNDP la zamani. Ilinichukua kama dakika 15 kurudi na kukuta gari limefungwa chuma kwa maana ya kwamba nilipaki vibaya. Nikawauliza what is next wakaniambia lazima twende kwenye ofisi yao kule keko nikalipie faini ya Tshs. 28,000. Nikawakubalia na mmoja wao akapanda kwenye gari tukaelekea keko. Kufika Keko kwenye yadi yao story ikabadirika. Nikaambiwa inabidi nilipe hizo pesa hapo, halafu niache gari nirudi town centre kwenda kulipia faini jiji Tshs. 50,000.00. Alternatively, ili kurahisisha mambo nikaambiwa waniandikie gate pass, halafu nikalipe Tshs. 60,000 kwa mlinzi wao pale getini ili niachane nao.

Nilikuwa tayari nimechelewa kukutana na mtu na hivyo ni opt kulipia hizo Tshs. 60,000 bila risiti. Maamuzi hayo yalizingatia ukweli kwamba ningelazimika kukodi taxi kwenda ofisi za jiji mjini na kurudi na hiyo isingenigharimu chini ya Tshs. 30,000 halafu na muda ambao ningepoteza hapo njiani kwenda na kurudi Keko. Wanasema ukiisha kuja na risiti ya kulipia jiji ndipo
wanakuruhusu kuchukua gari yako.

Huu ni mpango wa makusudi kabisa wa kupata pesa za bure na kuliacha jiji bila mapato yake. Kwangu mimi yafuatayo yangeweza kufanyika kurahisisha process ya kulipia faini;

1. Waliponikamata nilikuwa hapo hapo jiji, ilikuwa ni rahisi kuniambia nilipie gharama ya jiji kwanza kabla ya kwenda huko Keko.

2. Hawa watu badala ya kumtaka mtu aliyefanya kosa kwenda kulipia sehemu mbili tofauti, pesa zote zingekuwa zinalipwa jiji kama ilivyokuwa zamani, na majembe wanapata % yao kutokana na makusanyo.

Sina uhakika kama uongozi wa jiji unaujua uozo huu unaofanywa na hawa maagenti wao. Napendekeza jiji litangaze utaratibu wa kulipia faini na kiwango kijulikane kwa kila mtu kuliko mtindo wa sasa ambapo unajikuta unalazimika kufanya wanachikitaka hawa majembe bila kujua kama hivyo ndivyo ilivyo.

Je haya yameisha mkuta mtu mwingine? Tufanyeje kukomesha tabia hii.

Tiba

Pole sana mkuu,naamini kweli unachukia rushwa kama mimi,uharaka ulikulazimisha kushiriki mchezo mchafu,naamini bado unanafasi ya kupeleka malalamiko yako JIJI na TAKUKURU pia.
Majembe na baadhi ya traffic wanapenda kulazimisha rushwa,nashukuru binafsi nimejikopmboa kutoka kwammoja wa trafic wapenda rushwa baada ya kuwa nimerecord mabishano yangu naye kwenye simu yangu,mabishano ya bei ya rushwa aliyotaka,baada ya kuwa nimepata mazungumzo nilimjulisha kuwa si tu kuwa simpi rushwa lakini napeleka kwa wakubwa wake waliomtuma kukusanya rushwa,aliniachia na nashukuru sana hata baada ya kunisimamisha mara 2 hajarejea hoja yake kuhusu crek kwenye kioo cha gari yangu cha mbele.
Kwa pamoja tunaweza kupambana na mafedhuli hawa...
 
Pole sana mkuu,naamini kweli unachukia rushwa kama mimi,uharaka ulikulazimisha kushiriki mchezo mchafu,naamini bado unanafasi ya kupeleka malalamiko yako JIJI na TAKUKURU pia...

Kesi ya nyani unampelekea Ngedere!!!!!
 
Back
Top Bottom