Utapeli wa Majembe Auction Mart - A true Story

Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,604
3,163
Wana JF,

Nina leta taarifa hii kwenu ili kama kuna wahusika watasoma hapa basi wachukue hatua zinazostahili. Mchana huu nilipaki gari maeneo ya immigration karibu na jengo la UNDP la zamani. Ilinichukua kama dakika 15 kurudi na kukuta gari limefungwa chuma kwa maana ya kwamba nilipaki vibaya. Nikawauliza what is next wakaniambia lazima twende kwenye ofisi yao kule keko nikalipie faini ya Tshs. 28,000. Nikawakubalia na mmoja wao akapanda kwenye gari tukaelekea keko. Kufika Keko kwenye yadi yao story ikabadirika. Nikaambiwa inabidi nilipe hizo pesa hapo, halafu niache gari nirudi town centre kwenda kulipia faini jiji Tshs. 50,000.00. Alternatively, ili kurahisisha mambo nikaambiwa waniandikie gate pass, halafu nikalipe Tshs. 60,000 kwa mlinzi wao pale getini ili niachane nao.

Nilikuwa tayari nimechelewa kukutana na mtu na hivyo ni opt kulipia hizo Tshs. 60,000 bila risiti. Maamuzi hayo yalizingatia ukweli kwamba ningelazimika kukodi taxi kwenda ofisi za jiji mjini na kurudi na hiyo isingenigharimu chini ya Tshs. 30,000 halafu na muda ambao ningepoteza hapo njiani kwenda na kurudi Keko. Wanasema ukiisha kuja na risiti ya kulipia jiji ndipo
wanakuruhusu kuchukua gari yako.

Huu ni mpango wa makusudi kabisa wa kupata pesa za bure na kuliacha jiji bila mapato yake. Kwangu mimi yafuatayo yangeweza kufanyika kurahisisha process ya kulipia faini;

1. Waliponikamata nilikuwa hapo hapo jiji, ilikuwa ni rahisi kuniambia nilipie gharama ya jiji kwanza kabla ya kwenda huko Keko.

2. Hawa watu badala ya kumtaka mtu aliyefanya kosa kwenda kulipia sehemu mbili tofauti, pesa zote zingekuwa zinalipwa jiji kama ilivyokuwa zamani, na majembe wanapata % yao kutokana na makusanyo.

Sina uhakika kama uongozi wa jiji unaujua uozo huu unaofanywa na hawa maagenti wao. Napendekeza jiji litangaze utaratibu wa kulipia faini na kiwango kijulikane kwa kila mtu kuliko mtindo wa sasa ambapo unajikuta unalazimika kufanya wanachikitaka hawa majembe bila kujua kama hivyo ndivyo ilivyo.

Je haya yameisha mkuta mtu mwingine? Tufanyeje kukomesha tabia hii.

Tiba
 
Magufuli angekusikia wewe ungevuka kivuko kwa alfu kumi walai
 
wewe ndio ujnalikosesha jiji mapato, kwanini utoe rushwa?

Mkuu,

I am always against bribing anyone for anything. Ningekuwa mpenda rushwa nisingekubali kwenda mpaka huko Keko, tungemalizana pale pale mjini. Lakini kwa kuwa nilitaka nilipe hiyo faini kama inavyostahili, nilikubali kwenda Keko. Lakini baadae nilikuja gundua nimeingizwa kwenye mtego wa kutoa rushwa kwani huo mzunguko ungenigharimu zaidi ya hizo pesa nilizopashwa kulipa kihalali pamoja na muda. Nafikiri umenielewa. Swala ni je utaratibu wa kulipa faini ulio sahihi ni upi? Kwa nini hauwekwi wazi?

Tiba
 
huwa majembe ni matapeli toka alipokuwepo yule mzee wa kihehe ambaye ndio mmoja wa founders wa majembe..

Sasa unashauri kipi kifanyike kukomesha huo utapeli? For sure we need to do something!!!!

Tiba
 
ukikutana na hao jamaa watakudai hadi breakdown towing fee wakati gari umeenda ukiendesha wewe mwenyewe.kibaya zaidi ni huo mlolongo wa nenda JIJI kalipe leseni,nenda TRA kalipie stampduty mara releas ukirudi kwao wanakuchelewesha wanakuambia umechelewa njoo kesho ili ulipie storage...shida tu kwa mlipa kodi halafu zinatafunwa
 
Eneo lao hatari wanakotega ni pale ofisi za tigo(kituo cha gold star), na mbele ya nbc corprate posta ya zamani usiache gari pale kabisa watakulamba bila huruma.....
 
Hata ulalamike vp hao wanakula na wakubwa
kwa uonevu na rushwa za wazi wazi hawawezi chukuliwa hatua yoyote chini ya serikali hii ambayo si sikivu
 
Hivi Majembe ni ya nani? Kwani polic na migambo hawawezikufanya hizo kazi wanazofanya majembe? Kwani nao wanazijua sheria za barabarani maana siku hizi nawaona hata kwenye kusimamia magari kama trafic. Au niya kigogo flani anajikusanyia hela za serikali
 
Majembe ni ya Seith Mwamoto wanatokea iringa.
 
ukikutana na hao jamaa watakudai hadi breakdown towing fee wakati gari umeenda ukiendesha wewe mwenyewe.kibaya zaidi ni huo mlolongo wa nenda JIJI kalipe leseni,nenda TRA kalipie stampduty mara releas ukirudi kwao wanakuchelewesha wanakuambia umechelewa njoo kesho ili ulipie storage...shida tu kwa mlipa kodi halafu zinatafunwa

Sasa mkuu kipi kifanyike ili kuachana na utapeli huu?

Tiba
 
Hata ulalamike vp hao wanakula na wakubwa
kwa uonevu na rushwa za wazi wazi hawawezi chukuliwa hatua yoyote chini ya serikali hii ambayo si sikivu

Mkuu,

Kwa hiyo una conclude kwamba nothing can be done? No we need to do something, hatuwezi kuiacha hali hii iendelee.

Tiba
 
Mkuu,

I am always against bribing anyone for anything. Ningekuwa mpenda rushwa nisingekubali kwenda mpaka huko Keko, tungemalizana pale pale mjini. Lakini kwa kuwa nilitaka nilipe hiyo faini kama inavyostahili, nilikubali kwenda Keko. Lakini baadae nilikuja gundua nimeingizwa kwenye mtego wa kutoa rushwa kwani huo mzunguko ungenigharimu zaidi ya hizo pesa nilizopashwa kulipa kihalali pamoja na muda. Nafikiri umenielewa. Swala ni je utaratibu wa kulipa faini ulio sahihi ni upi? Kwa nini hauwekwi wazi?

Tiba

Mkuu pole sana....
Hii ndo bongo tambarare....
Jamaa wanakua wanajua kabisa kwamba watu wana mambo mengi ya kufanya na muda ni mdogo...then wanatumia sheria mbovu kukuchelewesha, ila uone njia pekee ni kutoa rushwa....
Isingekua jambo la ajabu kama pia ungeenda hadi jiji kukuta mhasibu 'katoka kidogo'...then ukaambiwa uende kesho asubuhi....na ukienda kesho...kule majembe wanakudai ulipie gharama za maogesho...!
 
Jamaa hakutoa rushwa bali alikuwa na haraka zake ndipo majembe wakampatia kwa ufisadi wao wakamtoza pesa za jiji bila stakabadhi.
 
Aliyewapa tenda ya kukamata magari ndio anayewaongoza kufanya hivyo. Hiyo hata ukalalamike kwa nani majibu yake hutayapenda. Nchi imeuzwa hii kaka.
 
Hivi majembe bado wapo! Na wale wa kukamata magari barabarani walikuwa ni haohao au yono?
 
Back
Top Bottom