Bw mito (Balloteli) wewe mwenyewe hujajieleza vizuri huenda huyo Wakala akataka msaada wa kifedha kwani No. ya huyo mteja si bado anayo kwanini asimpigie kumueleza yaliyomsibu? Mimi nilichosikitika ni hiyo heading kuwa "utapeli tigo sasa unatisha!" mimi ni mtumiaji wa tigo sioni kosa lao km huyo wakala hataki kusema ukweli natakupa link ya tigo uwaarifu kwa msaada zaidi Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More hapo waeleze yote au ingia facebook na utafute Tigo Tanzania Huo ni msaada wa mwisho ambapo utajua nani ni mkweli Wakala au mwizi
Ukwaju husomi vizuri nduguuuuu ah! Ukizipitia posti za mtoa mada kashasahihisha kuwa sawa sio tigo pesa bali ni mtoaji na mpokeaji. Mi nilivoisoma tu mada yake nikawa nshajua nini alichokusudia, lakini wewe ukawa unatoa ushauri nje kabisa ya maudhui. Huwezi kumshauri eti aende tigo kupeleka malalamiko, kwanza jiulize, hao tigo watakusaidia vipi? Wao watakuwa na ushahidi gani km ni chuma ulete? Wewe binafsi ushahidi wako upi? Hata kama namba ya mteja unayo, yeye si alikukabidhi hela na ukazitia katika pochi? Na ukikubali ivo basi uzembe wako, sifikiri kama hata alokupa pesa atakubali na yeye kama chuma ulete! Fikiria, laki sita izo unafikiri uyo alozipokea ataziweka tu kwenye account? Si atatuoa line kabisa tu baada ya kuzitoa? Tusome mada jamani tusirukie tu kwa kusoma kichwa cha habari pekee yake!!