Utapeli mpya waibuka Dar

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
POLISI Kanda Dar es Salaam imewatahadharisha wananchi, makampuni, taasisi mbalimbali nchini kujihadhari na wimbi la utapeli lililoibuka hivi karibuni la matapeli kutumia majina ya viongozi wa Serikali, mawaziri kujipatia fedha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova amesema kumezuka wimbi la utapeli wa kupiga simu na kutapeli mamilioni ya fedha kwenye taasisi mbalimbali wakijifanya ni mawaziri.

Amesema kuwa watu hao hupiga simu na kujifanya wao ni waziri fulani na hata kuiga sauti ya waziri huyo na kusema na kuamuru apewe kiasi Fulani cha fedha kw kujifanya ana shida ya fedha kwa ajili ya ada, safari au hata matumizi mengine.

Amesema wakishaambiwa wazifuate, matapeli hao huwatuma madereva wenye magari ya serikali, yenye namba za bandia za STK na SU na kujifanya ni madereva wa mawaziri hao na wanafata fedha hizo.

Na baadae wakijaribu kuwasiliana na viongozi hao hushangaa na kukiri hawajatuma mtu yeyote kuchukua fedha.

Amesema kuwa wimbi hilo limeibuka sasa katika jiji la Dar es Salaam na matukio kadhaa yamesharipotiwa polisi na kuwataka wananchi wafanyabiashara kuwa makini sana.

Na Pilly Kigome, Dar
Source: NIFAHAMISHE
 
Amesema kuwa watu hao hupiga simu na kujifanya wao ni waziri fulani na hata kuiga sauti ya waziri huyo na kusema na kuamuru apewe kiasi Fulani cha fedha kw kujifanya ana shida ya fedha kwa ajili ya ada, safari au hata matumizi mengine.

Ndio professional way ya transaction kwa mawaziri wetu? ndio maana hata utapeli unakuwepo?-vimemox2
 
Ni utaratibu gani wa kupigiwa simu tu na mtu, hata akiwa waziri gani, apewe hela bila utaratibu hivyo?
Hii si ndo mambo ya Posho mbilimbili?

Kama kuna taasisi imeibiwa kwa njia hiyo, basi ni VIZURI SANA, mi nimependa, maana hata hizo taasisi zina`intertain uzembe, zina harufu ya Rushwa!
 
Ya very ryt mkuu
 
Back
Top Bottom