Utapeli mpya facebook kwa watumiaji wa tigo

viz

Member
Jul 18, 2012
21
2
kuweni makini na watumiaji wa tigo kuna style mpya ya wizi kwenye mtandao wa kijamii facebook: hebu ingia kwenye hii link Salama Jabir | Facebook huyu jamaa anajiita kama Salama Jabir yule mtangazaji wa kipindi cha mkasi EATV

Kwenye wall yake kuna tangazo kama lifuatalo:

"TIGO MXSHARE PIGA SIMU BURE KWENDA MITANDAO YOTE BILA MALIPO:

Hi, kwa wale wote wanao ulizia huduma ya tigo mxshare. Technician bado anaendelea kuunganisha huduma ya Mxshare kwa bei nafuu Tshs.3500, ukiunganishiwa unakua na uwezo wa kupiga simu bure kwenda mitandao yote Tanzania bila malipo ya vocha na ukishaunganishiwa huduma haina kikomo na ukishalipia 3500 ukaunganishiwa hautolipia tena pesa na hautohtaj kuunganshwa tena huduma ni yamoja kwa moja.

KAMA UNAHITAJI TAFADHALI NITUMIE NAMBA YAKO YA SIMU INBOX SASA HIVI ILI NIMPATIE TECHNICIAN WA TIGO AIUNGANISHE KATIKA SYSTEM KISHA UTALIPIA Tshs.3500 ILI TUKUPE PIN NUMBER YAKUJIUNGA.

KUMBUKA: Hatuhitaj mtu awe na hofu na kuhisi anatapeliwa maana mjini hapa na sio wote mnao amini, ila tuna uhakika na huduma hii na wengi tumewaunganishia. HATUCHUKUI PESA KWANZA MPAKA UTUPE NAMBA YAKO IUNGANISHWE KTK SYSTEM KISHA UTAHAKIKISHA JE, NIKWELI KUNA HUDUMA IITWAYO MXSHARE? KISHA NDIO UTALIPIA TUKUPE NAMBA YA SIRI YAKUJIUNGA."

Nawakilisha
 
Wabongo bwana! wanapenda kula bata bla kutoka jasho kama vp akawaunganishie wabunge wanaoish dar wapigie raia majimbon
 
3500 simu bila kikomo kwenda mitandao yote hapa nchini,Kampuni ingefungwa hii
 
Back
Top Bottom