Utapeli mkubwa DSM: Beware

Kumbe waliotapeliwa ni wengi? Tatizo la watz walio wengi wanapenda njia za mkato! Ndio maana ofisi zetu za serikali kuna ufisadi mdogomdogo mwingi, zinaitwa dili! Mtu akionekana mwadilifu atapigwa vita mpaka anaweza kuacha kazi! Hawa waliotapeliwa wote ni wapenda njia za mkato na kama wameajiriwa wako likely kuwa wanafanya ufisadi!
 
Sisi tumelizwa 1,300,000/= kwa njia hiyo hiyo uliyoelezea Mjasiliamali. Tena siyo waswahili kama unavyodhani kwani rugha wanayoongea ni kiingereza ambao ni watu weupe tena waliyoenda shule.

Story hii ni kweli kabisa. Katika ofisi niliyomo tuna biashara mbali mbali ikiwemo ya fumigation. Mnamo February 09 meneja wa kitengo cha fumigation alipigiwa simu akaambiwa kwamba kuna dawa zinatakiwa kwenda Sudan ya Kusini kwa ajili ya kuifadhi chakula cha UNHCR. Kwamba mtu anayezichukua dawa hizo atatokea UNHCR Ngara mara tu itakapodhibitika kwamba dawa zipo atapanda charter toka Ngara hadi Dar Es Salaam nawakutane airport.

Mimi binafis nilihusika kuzungumza kiingereza na mzungu (mwenzangu hajui kimombo vizuiri) aliyejifanya yuko Ngara na aliniambia tukipeleka madawa hayo airport atatulipa cash hapo hapo na faida ilkuwa kubwa. Dawa zenyewe tuliambiwa zinapatika kwa supplier pale Mwenge na kila chupa $6,000 na zinatakiwa chupa 2. Kwa nini wasinunue direct toka Mwenge? Tukaambiwa supplier wa Mwenge hatoi commission.

Kwa bahati nzuri meneja wa kitengo cha fumigation anafahamiana na watu wa UNHCR hapa Dar ES salaam, kwa hiyo kitu cha kwanza aliwapigia simu kuhakikisha kwamba dawa kama zile ni za kuhifadhi chakula wakamwambia sio. Tena wakamwambia pia kituo cha UNCHR kule Ngara kilishafungwa hivyo tukajua huyo "Mzungu" hayuko Ngara kama alivyodai.

Hata hivyo tukaamua kufuatilia tuone mwisho wake.Tukachukua blank cheque kuelekea Mwenge. Tulipofika Petrol Station ya Bamaga tukaambiwa tusimame pale mtu atakuja na dawa tumpe $12,000 atukabithi dawa. Alipokuja tukaingia kwenye gari yake akatuonyesha "dawa". Tukamwambia tunalipa kwa cheque akarusha. To cut the long story short baada ya hapo simu zilizopigwa na yule "mzungu" akilalamika kwamba yuko tayari airport na nasubiri dawa zilikuwa nyingi mno.

Ni kweli ni mtandao wa hali ya juu wa kitapeli na wazungu wamo!! BEWARE.
 
Sawa watu wananibiwa poleni lakini iweje mtu aanze kukuambia mambo ya ndani kwako na sijui uliko soma n.k. alafu uingie line?? mimi nimekumbana na hawa watu enzi za mwaka 1993 hapo kisutu, lakini hawakuwa wanatumia simu walikuwa ni wale wanakwambia sijui kuna benki imeporwa na ulikuwaukiwasikiliza tu umekwisha tena wale walikuwa wanakukaba.

Nacho washauri watanzania ni kujifunza utamaduni wa kuto mwamini mtu hivi hivi bila kujiridhisha na anacho kisema kwa kuona. Tena mtu kama anaongea kwenye simu na anaanza kujitambulisha wewe kata simu tu.

Hakuna mjinga wa kukuletea wewe project bila kuifanyia kazi. Tumezoea sana dezo.
 
maisha magumu mkuu ndio maana watu wanabuni mbinu za kujiongezea kipato, na kama utagundua hawawaibii walala hoi, so sio mbaya wanagawana uamskini, ilaa tuwe makini na hizo njia mpya za utapeli
kweli maisha ni magumu mkuu, lakini katika pilikapilka za kutoka ndio hivyo tena, watu hawaishihii kuwatapeli watu tu bali mambo ya kuuwa maalbino, ushirika, ulokole usio na kichwa wala miguu na mengineyo mengi ili mradi kama wewe ni mtafutaji lazima uibiwe, ukipona kwa hao matapeli bac utakamatwa kwa mganga au kwa Mtume
 
Hawa watu wanatumia nchi tatu Kenya/Uganda/Tanzania, kwani wakikupigia unaona kabisa code ni ya uganda au Kenya ukiwa Tz, na communication nao ni Wazungu/Wakenya wenye rafudhi ya kikenya.

Na kwakuwa member mmoja ameelezea kuwa yeye game lilichezwa Mlimani basi na sisi pale mlimani ndo tulicash pesa baada ya kutoa pesa benki, tukapewa mzigo kukimbiza airport kuwahi ndege iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Sudan kabla ya saa 7.30 mchana.

Baada ya kucash pesa mawasiliano yakakatika kote tukabaki na Mzungu wa Uganda, ndo tukagundua tiyari tumetapeliwa!! Yaani huwezi kuamini kwani tulibaki na machupa hayo maji (sample) mwishowe nikaona hapa polisi anaweza kuja home akanibamba nayo nikaonekana mimi ndo tapeli basi ilibidi nimwage yale maji na kuchoma chupa.
 
Bongo kila kitu kinawezekana......muhimu tusipende kuwa matawi ya juu without pain /struggle.....! Best harvest comes with hard work always sio tu njia za mkato.....ukilazimisha matokeo yake ndo hayo!
 
Ama kweli bure ghali!

Hivi hivi watu wali[peleka pesa yao DECI eti izae na wakapoteza viakiba vyao. Sijui tutajifunza lini kwamba unavuna ulichopanda?
 
Ama kweli bure ghali!

Hivi hivi watu wali[peleka pesa yao DECI eti izae na wakapoteza viakiba vyao. Sijui tutajifunza lini kwamba unavuna ulichopanda?

Watanzania hatupendi kujifunza kutokana na makosa yetu ya awali au ya wenzetu. Watu hawajapona maumivu ya DECI wengine wanawaza kuwa mamilionea ndani ya dakika tano. Tatizo letu tunapenda sana kujikweza kwa kutaka kupanda chati kwa vodafasta! Mafanikio endelevu hayaji namna hiyo. Watu wengi waliofanikiwa wamefanya kazi kwa bidii na maarifa tena kwa muda mrefu kabla ya kuvuna hayo matunda tunayoyaona sasa. Tukiendekeza ndoto za kuukata mara moja basi tusilalamike kwani hata hao wezi wanatimiza ndoto zao. Na ukiingia kwenye laini zao basi na wewe ni mwenzao!
 
Hao watu washawaliza wengi na hata majuzi tulitaka kuwakamata mitaa ya Sinza wakakimbia!

Mimi nimerecord hadi sauti yao! But if it is a police case ni rahisi kuwakamata through serial number za simu-handset. (baada ya registration ya simcard itakuwa rahisi through mobile number). Chukua simu yako, piga *#06# utaona serial number ya handset yako, hii ndo police wanatumia kuwapata wahalifu wasio wajanja, mhalifu mjanja atatumia call box ama simu yake then anaitupa, ama atatuma msg (ukituma msg kwenye mtambo wa simu serial number hai-display, ndo maana ilikuwa vigumu ku-trace wabaya wa Mwandishi Kubenea!).

Waalifu wengi wanajisahau wanapiga simu then wanabadilisha simcard wakifikiri huwezi kuwapata! Atabadili line ya Tigo, Zain, Voda ama Zantel, lakini simu ni ile ile. Kama unakumbuka wezi wa CRDB Azikiwe, na NBC moshi walikamatwa kwa staili hii, baada ya waalifu kutupa simcard na polisi kuikota.

Kawaida polisi wanatumia serial number na kuangalia watu unaowapigia mara kwa mara, say mkeo/mmeo ama mtu yeyote wa karibu, then from there upelelezi unaanza!

Wanawatapeli wengi hawa watu hasa wakitegemea kwamba December ni mwisho wao baada ya simcard registration!

POLICE WAKIWA SERIOUS WANAWAKAMATA!





Nakubaliana nawe kabisa utapeli umezidi. Wiki mbili zilizopita nilipokea sms ikiniambia kuwa nimeshinda milioni kumi kwenye mtandao wangu wa vodacom. Nikapewa na namba ambayo niwasiliane na hao wahusika ili tuitwe kwenye ITV then tupewe pesa zetu kwani tuko kama watu 5. Lakini cha kushangaza nikaambiwa ninunue dola 20 (vocha) then niweke kwenye simu yangu. Mimi sikuelewa nikaweka dola 20 kweli kwenye simu yangu na nilipoulizwa nika waambia nimekwisha weka, kumbe nilitakiwa niweke zile tarakimu ili wao waweke kwao na inakuwa kama ni fee. Kuona hivyo nikashutuka na kuwaambia nafikiri mpaka hapo na hiyo zawadi siitaki tena. Wakaniuliza niko wapi wanifuate nikawaambia niko mbeya na stori ikaishia hapo. Baada ya muda mfanyakazi mwenzangu mmoja akapokea simu na kuanza kururkaruka kuwa ni mshindi kapigiwa simu, kwa vile nilikuwepo pale nikamwambia ajaribu kupiga simu aliyopewa na ikawa haipatikani, nikamwambia achana nao wezi hao, habari ndiyo hiyo. Maisha yamekuwa magumu sana kiasi kwamba kila kukicha watu wanapiga bongo jinsi ya kuwaibia wenzao. Tuamuke tu sasa na mungu atubariki na TZ yetu!
 
Story hii ni kweli kabisa. Katika ofisi niliyomo tuna biashara mbali mbali ikiwemo ya fumigation. Mnamo February 09 meneja wa kitengo cha fumigation alipigiwa simu akaambiwa kwamba kuna dawa zinatakiwa kwenda Sudan ya Kusini kwa ajili ya kuifadhi chakula cha UNHCR. Kwamba mtu anayezichukua dawa hizo atatokea UNHCR Ngara mara tu itakapodhibitika kwamba dawa zipo atapanda charter toka Ngara hadi Dar Es Salaam nawakutane airport.

Mimi binafis nilihusika kuzungumza kiingereza na mzungu (mwenzangu hajui kimombo vizuiri) aliyejifanya yuko Ngara na aliniambia tukipeleka madawa hayo airport atatulipa cash hapo hapo na faida ilkuwa kubwa. Dawa zenyewe tuliambiwa zinapatika kwa supplier pale Mwenge na kila chupa $6,000 na zinatakiwa chupa 2. Kwa nini wasinunue direct toka Mwenge? Tukaambiwa supplier wa Mwenge hatoi commision.

Kwa bahati nzuri meneja wa kitengo cha fumation anafahamiana na watu wa UNHCR hapa Dar ES salaam, kwa hiyo kitu cha kwanza aliwapigia simu kuhakikisha kwamba dawa kama zile ni za kuhifadhi chakula wakamwambia sio. Tena wakamwambia pia kituo cha UNCHR kule Ngara kilishafungwa hivyo tukajua huyo "Mzungu" hayuko Ngara kama alivyodai.

Hata hivyo tukaamua kufuatilia tuone mwisho wake.Tukachukua blank cheque kuelekea Mwenge. Tulipofika Petrol Station ya Bamaga tukaambiwa tusimame pale mtu atakuja na dawa tumpe $12,000 atukabithi dawa. Alipokuja tukaingia kwenye gari yake akatuonyesha "dawa". Tukamwambia tunalipa kwa cheque akarusha. To cut the long story short baada ya hapo simu zilizopigwa na yule "mzungu" akilalamika kwamba yuko tayari airport na nasubiri dawa zilikuwa nyingi mno. Ni kweli ni mtandao wa hali ya juu wa kitapeli na wazungu wamo!! BEWARE.

Kwanza kabisa if you are smart and informed, mi naona ni ngumu kutapeliwa na hawa mabwana! Eti dawa inahitajiwa na UNHCR kwa ajili ya kuhifadhi chakula! Shirika linalohusika na Chakula Duniani si UNHCR, ni UN-WFP, hata kambini wanaotunza chakula ni wao wala si UNHCR. UNHCR wanahusika kugawa non-food commodities, mahema/turubai, mashuka, nguo n.k


Kitu kingine, si kwamba wana-Wazungu et wanaongea Kiingereza fasaha!, Jamani mmemsahau Steeve Nyerere anayeigiza sauti ya Bush, Obama, Marehemu Sadam Hussein na Sarkozy! So suala la kuiga lugha na kujifanya Mzungu, Mkenya ama Mganda, sio issue ni kuiga tu!

Kuna suala la line ya simu eti inadisplay code za Uganda ama Kenya. Hata wewe ukienda na Voda ama Zain ya Tanzania ukiwa Kenya ama Uganda itaonesha uko Tanzania. So hawa watu wanatumia line za nchi hizo tu na si kwamba wako huko, wako Sinza tu hapa Dar.

BEWARE AGAIN AND AGAIN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Just be careful. Usipende maisha mteremko. There is no such a thing called..Free Lunch.. sasa wewe ukisikia unatoa kiduchu halafu ukakuwa billionea unakimbilia. Hizo ni jinsi ya kuwapata watu wenye tamaa mbaya. You can't be a the top of Kilimanjaro without starting the journey at the bottom available entry point and climb slowly through the hillys and gullies route to the top. Tuacha kuota maisha bora overnight. It will never be there. It is a process and has steps. Asante sana Mjasiriamali kwa ku-share.
 
kwanza kabisa if you are smart and informed, mi naona ni ngumu kutapeliwa na hawa mabwana! Eti dawa inahitajiwa na unhcr kwa ajili ya kuhifadhi chakula! Shirika linalohusika na chakula duniani si unhcr, ni un-wfp, hata kambini wanaotunza chakula ni wao wala si unhcr. Unhcr wanahusika kugawa non-food commodities, mahema/turubai, mashuka, nguo n.k


kitu kingine, si kwamba wana-wazungu et wanaongea kiingereza fasaha!, jamani mmemsahau steeve nyerere anayeigiza sauti ya bush, obama, marehemu sadam hussein na sarkozy! So suala la kuiga lugha na kujifanya mzungu, mkenya ama mganda, sio issue ni kuiga tu!

Kuna suala la line ya simu eti inadisplay code za uganda ama kenya. Hata wewe ukienda na voda ama zain ya tanzania ukiwa kenya ama uganda itaonesha uko tanzania. So hawa watu wanatumia line za nchi hizo tu na si kwamba wako huko, wako sinza tu hapa dar.

Beware again and again!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


mkuu umetufungua masikio...
Asante,tunayajua lakini hatuyafikirii kwa haraka.
 
Tukishirikiana tutaweza tokomeza huu utapeli. Na hili litawezekana iwapo kila mpata habari/taarifa hii atamhabarisha jirani/rafiki/jamaa yake wa karibu!
 
hizo zote ni aina tu za deci watu wanafikiri there is free lunch in this world.........
achana na mambo ya madili jamani fanyeni kazi...............
 
Tatizo maisha yanapokuwa magumu hata challeng zinakuwa kubwa those who come with that idea are pple who failed to be enterprenuer any way this sholud be challenger to police,army and citizen
 
Back
Top Bottom