Utapeli huu utaisha lini?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Utakuwa unasikiliza kipindi kwenye radio (kama clouds fm, bbc n.k) na mtangazaji anakuomba uchangie maoni kwa kutuma sms, unafanya hivo mapema na mtandao unakutaarifu kuwa ujumbe wako umepokelewa. Ajabu mpaka kipindi hicho kinaisha mtangazaji ana soma kidogo sana ujumbe, si wako au hasomi kabisa ujumbe wa msikilizaji.
Sasa najiuliza hii si kama utapeli wa kujipatia mapato kupitia sms ni nini?
 
Sasa unadhani wewe mwenyewe ndie unaetuma?
Mnatuma wengi na muda hauruhusu kusoma kila text.
 
Sawa kabisa Lizzy, kinachonikera ni hiyo pesa wanayopokea kwa kila mtuma ujumbe ambapo wanajua hakika hawawezi kusoma ujumbe wote toka kwa wasikilizaji wao. Kwa nini wasiwatake wasikilizaji wapige simu kama ambavyo baadhi ya radio na television wanafanya?
Lizzy, hapa nionavo mimi ni uvunaji wa pesa kirahisi hivo!!!!!!!!
 
MJ nawaonea huruma wasikilizaji ambao wanaombwa kutoa dukuduku lao kwa sms kumbe wanaliwa kijanja na makampuni ya simu!
 
Sawa kabisa Lizzy, kinachonikera ni hiyo pesa wanayopokea kwa kila mtuma ujumbe ambapo wanajua hakika hawawezi kusoma ujumbe wote toka kwa wasikilizaji wao. Kwa nini wasiwatake wasikilizaji wapige simu kama ambavyo baadhi ya radio na television wanafanya?
Lizzy, hapa nionavo mimi ni uvunaji wa pesa kirahisi hivo!!!!!!!!

Hiyo ni biashara, na kwa nnavyojua mimi (nilivyozoea) hua inajulikana kabisa kwamba ukipiga simu hata isipopokelewa wanakata pesa , ukituma sms hata wasiposoma pesa inakatwa pia. Kwahiyo mtu anapoamua kupiga simu kwenye hivyo vipindi au kutuma text anatakiwa ajue kabisa kwamba hamna guarantee kua simu yake itaingia ama text yake itasoma, na pesa yake itakatwa hata kama alichotaka kisipotimia.
 
Back
Top Bottom