Utani na Msichana ninaye fanya naye kazi unataka kunivunjia ndoa yangu

Mangi Moshi

Member
Jun 21, 2011
22
11
Kuna msichana nafanya naye kazi katika kampuni moja. Sasa tumezoea kweli kutaniana na kuitana majina ya Kimahaba huku kukiwa hakuna uhusiano wowote wa Kimapenzi. Jana saa nne usiku nikiwa nafanya kazi zangu kwenye kompyuta sebuleni na simu ikiwa chumbani akanitumia ujumbe unaosomeka "Honey, its too cold today, I wish you could be beside me now, I cant Imagine how the situation could be". Aisee, mama watoto alikuwa kajipumzikia kitandani huyoo akaamka na kwenda mezani, akachukua simu na kusoma meseji. Kilichojiri hapo nilisikia mlango wa chumbani umefunguliwa, baadaye nikasikia paa, nimepigwa kofi zito la shavuni. Nilipozinduka nikamkuta analia, akaniambia haya twende chumbani ukavae uende ukampe joto huyo malaya wako. Nikasita, nikapigwa tena kofi la begani na kuambiwa nyanyukaaaa, malaya mkubwa wewe. Unataka kuniuwa niache watoto wanakula shida na malaya zako. Kwa kweli ilikuwa ni zengwe sana. na leo nimemkia hotel, baada ya kuona vurugu inataka kuanza kushirikisha majirani. Wife amekataa kabisa kunielewa, leo nimempigia simu hapokei, meseji hajibu binti nimemueleza yaliyonikuta kwa sababu ya ushenzi wake anachekacheka tu, natamani nimmeze kwa kweli. Natafakari nielekee wapi nkitoka hapa kazini.Nawasilisha kwa ushauri.
 
Kati yako wewe na huyo msichana kuna mmoja anamtaka mwenzake kweli wakati mwenzake yupo katika hali ya kawaida ya utani tuu,wa mtu na mfanyakazi mwenzake!!!Hilo ni tatizo kubwa,na kama huyo msichana anania ya mapenzi na wewe,basi alifanya hivyo makusudi kukugombanisha na mkeo ili ufanye kweli,kuwa muangalifu juu ya hili!!!
 
Pole sana mkuu,utani kama huu haufai hata kidogo.Kwa nini umemzoeza mke wako kusoma MESSAGE zako?
 
thatha aisee, kama umeamua kukimbia mji, inatia mashaka make umeongezea petrol kwenye moto!
tutaamini vp kuwa ulikuwa Hotelini pekee yako bl "Malaya" huyo (according to your WIFE)!
na kama uko INNOCENT kwann unashindwa kumface my wife wako?
Hacha hzo bana enheeeeeeeeeee!
ila nakupa pole, ila angalia utani.... ungekuwa wewe ndo umemtania alaf BF wake akanyaka ungefanyaje??
 
Kuna msichana nafanya naye kazi katika kampuni moja. Sasa tumezoea kweli kutaniana na kuitana majina ya Kimahaba huku kukiwa hakuna uhusiano wowote wa Kimapenzi. Jana saa nne usiku nikiwa nafanya kazi zangu kwenye kompyuta sebuleni na simu ikiwa chumbani akanitumia ujumbe unaosomeka "Honey, its too cold today, I wish you could be beside me now, I cant Imagine how the situation could be". Aisee, mama watoto alikuwa kajipumzikia kitandani huyoo akaamka na kwenda mezani, akachukua simu na kusoma meseji. Kilichojiri hapo nilisikia mlango wa chumbani umefunguliwa, baadaye nikasikia paa, nimepigwa kofi zito la shavuni. Nilipozinduka nikamkuta analia, akaniambia haya twende chumbani ukavae uende ukampe joto huyo malaya wako. Nikasita, nikapigwa tena kofi la begani na kuambiwa nyanyukaaaa, malaya mkubwa wewe. Unataka kuniuwa niache watoto wanakula shida na malaya zako. Kwa kweli ilikuwa ni zengwe sana. na leo nimemkia hotel, baada ya kuona vurugu inataka kuanza kushirikisha majirani. Wife amekataa kabisa kunielewa, leo nimempigia simu hapokei, meseji hajibu binti nimemueleza yaliyonikuta kwa sababu ya ushenzi wake anachekacheka tu, natamani nimmeze kwa kweli. Natafakari nielekee wapi nkitoka hapa kazini.Nawasilisha kwa ushauri.

Umeyataka mwenyewe, unavuna ulichopanda.
 
Sijui unataka tukushaurije....wajua my wife wako angekuwa ndo kaandikiwa hivyo na wewe ukasoma ungeshamrudisha kwao na mahari ukadai.
Mpe nafasi.
 
huyo binti anakutaka ila wewe unaona ni kama mzaha, fanya uamuzi haraka wa kutojibu au kupokea simu zake na pia mwambie masihara yenu yafike kikomo au yaishie huko huko ofisini, itafika wakati mke wako anaweza choka na hayo anayoyaona na akaamua nae kufanya yale anayodhani wewe unayafanya. KUWA MAKINI ...UIKIMWI UNAUA!
 
Huko ulikoenda kulala ndio umeharibu kabisa,mkeo atajua ulienda kwa huyo mchafuzi.Hatukatazwi utani lakini kwanini hukuweka mipaka,we unaona hiyo text imekaa vizuri?nahisi huyo binti ana plani ambayo hujaigundua!Ukiendelea kucheza ipo siku utajutia!

We mwanaume bwana,kufa kiume!Rudi home leo,tena mapema.Muombe mamsapu ka outing kidogo,ukamuweke wazi mambo yalivyo na umuombe msamaha.Mpige stop huyo binti,tena uwe serious haswaa.Akiendelea,mpe mamsapu simu awe anajibu yeye meseji za huyo binti,kama akipiga simu pia apokee yeye (mkeo)ila asimtukane.
 
pole mkaka ila ww umeyataka mwenyewe na matan ya kijinga jinga na huyo bint, sasa kama kwel hana hisia zozote juu yako kwa nn
acheke cheke pia kama ni rafik yako tu mwambie aje kukusaidia kumbembeleza huyo mkeo.
 
ingekuwa ni mm, kwanza kama kweli huyo rafiki wa ofisi hatuna mahusiano na ni rafiki kweli nitamuomba tuongozane nyumbani, aongee na mamsap wangu ili ukweli ujulikane....
si ana simu alyotumia kunitext? tutaona sent items au namba zake zitaprove. ila kama atakataa kwenda, nitajua hakuwa rafiki ila alkuwa na nia nyingine kwangu.
 
Kuna msichana nafanya naye kazi katika kampuni moja. Sasa tumezoea kweli kutaniana na kuitana majina ya Kimahaba huku kukiwa hakuna uhusiano wowote wa Kimapenzi. Jana saa nne usiku nikiwa nafanya kazi zangu kwenye kompyuta sebuleni na simu ikiwa chumbani akanitumia ujumbe unaosomeka "Honey, its too cold today, I wish you could be beside me now, I cant Imagine how the situation could be". Aisee, mama watoto alikuwa kajipumzikia kitandani huyoo akaamka na kwenda mezani, akachukua simu na kusoma meseji. Kilichojiri hapo nilisikia mlango wa chumbani umefunguliwa, baadaye nikasikia paa, nimepigwa kofi zito la shavuni. Nilipozinduka nikamkuta analia, akaniambia haya twende chumbani ukavae uende ukampe joto huyo malaya wako. Nikasita, nikapigwa tena kofi la begani na kuambiwa nyanyukaaaa, malaya mkubwa wewe. Unataka kuniuwa niache watoto wanakula shida na malaya zako. Kwa kweli ilikuwa ni zengwe sana. na leo nimemkia hotel, baada ya kuona vurugu inataka kuanza kushirikisha majirani. Wife amekataa kabisa kunielewa, leo nimempigia simu hapokei, meseji hajibu binti nimemueleza yaliyonikuta kwa sababu ya ushenzi wake anachekacheka tu, natamani nimmeze kwa kweli. Natafakari nielekee wapi nkitoka hapa kazini.Nawasilisha kwa ushauri.
dah inabidi ummege tu huyo binti manake inaonekana kadhamiria
 
Pole mbe masawee! Mnaleta utani kwenye ndoa aisee. Yaani usikimbie nyumbani hata kama ni makofi yavumilie, pia tafuta watu wazima wenye busara zao wajaribu kusema na wife wako na kumuelezea hali halisi though mmevuka mipaka ya utani babangu!
 
Mke wako hapo kashapoteza trust kwako, inabidi tu ufanye kweli! Lamba huyo workmate!
 
Pole sana. Nadhani cha kufanya kwanza ni kumwambia huyo dada ofisini kua hutaki tena mautani yake ya kijinga na asikuandikie until further notice. cha pili, mwambie mke wako kua umemkomesha huyo binti, it won't happen again. alafu tatu ndio uanze kumuelewesha huo uhusiano wenu (ambao sio halali, tuseme ukweli). Usipo fata hizo hatua utakua unaongea na mama hapo hapo dada wa ofisini anatuma tena msg ingine.
Hivi na huko kulikua na baridi jana? maana huku ni balaa
 
Back
Top Bottom