Utani kati ya makabila

MaMkubwa1

Member
Nov 2, 2011
17
1
Jamani hodi humu jamvini!
Huenda swala hili limeshaongelewa huko nyuma ... mimi sijui maana mie ni mgeni. Lakini ni katika kutafuta ufahamu. Je UTANI kati ya makabila ulitokana na nini? Japo dhana hii ina mwelekeo wa kizamani / wa kale ukizingatia juhudi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika kuelekea kwenye utaifa ikiwa ni pamoja na ndoa za watu wanaotoka makabila tofauti , lakini haimaanishi kutotafuta jinsi jamii tofauti zilivyoweza kupatana na kuishi katika msingi na mifumo fulani fulani. Hivyo kwa sasa tuongelee “utani” kati ya makabila. Je ulitokana na nini? Haya makundi yalichaguana vipi kuwa ‘watani”? Je hii ni dhana ya huku kwetu Tanzania tu au na kwingineko ipo?
 
Utani ulifuatia mnyukano, mapigano kati yao, heshima ikajengwa na wakaitana watani (MngoniVs Mnyamwezi/MngoniVs Mhehe ..... endeleza
 
Nadhani hata sasa hivi ili heshima iwepo lazima tuwanyuke kwanza CCM halafu baadaye atakuwa mtani wetu
 
Utani ulifuatia mnyukano, mapigano kati yao, heshima ikajengwa na wakaitana watani (MngoniVs Mnyamwezi/MngoniVs Mhehe ..... endeleza
Msukuma vas Mzaramo, Mngoni Vs Mbena, Mluguru, Mfipa, Mnyakyusa, Msukuma, Mnyamwezi, Mmakonde, Mndengeloko, ........
 
Samahani mmeenda nje ya mada. Mimi nitaenda moja kwa moja kwenye point.

1. Kumbuka Asilimia kubwa ya watanzania ni wabantu. Kwa hiyo tumetokea kwenye jamii ya aina moja. Nakatika makabila ya kibantu yana dhana zifuatazo:-
a. Mashemeji kutania.
b. Babu na wajukuu. Na mengine mengi.
Katika kugawanyika kwa makabila ya kibantu yaligawanyika na dhana hiyo hiyo. Na makabila yote haya unayo yaona yametokana na koo mbalimbali. Kwa hii mantiki matani haya yote ni ya kihistoria.

2. Kuhusu nchi nyingine. Kwa uelewa wangu, kwa nchi za kibantu zinadesturi ileile. Lakini nchi ambazo si za wabantu si dhani kama wanautani huu. Maana mambo ya utani ni utamaduni wa kibantu, Katika kuelimisha, kukosoa, vilivile kuburudisha.
 
Back
Top Bottom