mimi navyojua kwa mila za kihaya kwasababu mimi mhaya pia, mwanamke akiolewa anakuwa part and parcel ya familia ya mwanaume hata akifa atazikwa kwa mwanaume si kwao.
Mtoto akifariki anazikwa kwenye upande wa mwananume si mwanamke.
Kuonesha msisitizo kipindi cha nyuma ilikuwa mwanaume hawezi kulala kwao mwanamke mila zilikuwa haziruhusu kabisa utaenda utembee hata kama ni saa 5 usiku itakubdi uondoke ukalale pengine.
Nakuongeza kuwa kutokana na mgogoro wa familia ulikuwepo baina ya kanumba na baba yake labda kwa kutotumia busara wameshindwa kumshirikisha baba yake kanumba kwenye huu msiba wa mwanae.
Hata mimi nilishangaa kumwona babake kanumba anahojiwa tbc anaongea mambo ambayo ni tofauti na tuliyo ambiwa na akina ray na pia hata kamati ya mazishi inasema aliyekuwa anasubiliwa ni mama hata baba hajamtaja.
sitaki judge lakini ukweli hii si mila ya wahaya huu ni mgogoro wao binafsi ambao nahisi utakuja waletea matatizo.
nimejifunza kiasi kuhusu mila za kihaya.sielewi kwa nini watu wanapenda kuwasema vibaya wahaya.kwani nina rafiki yangu ameolewa na muhaya,alivyoulizwa mume wako ni kabila gani,alivyotaja muhaya,watu waliguna.yeye ni mtu wa morogoro
We mama mbona una frustrations sana leo? Mbona mama alipigiwa simu fasta? Kwa mtu mwenye akili baada ya msiba kutokea baba ndio anakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa kwa kuwa ndio Decision maker. Huenda amewaachia wahaya wajifagilie kwanza yeye atatinga siku ya kumpumzisha. Hata namna ya kifo inareflect kuwa jamaa hakupitia malezi mazuri.
RIP The Great Kanumba, the Shinyanga boy
Kumbe frustration zinapimwa kwenye sred?
Basi hiyo ndo my very romatic language niliyoiibua uvunguni mwa moyo.
back to the topic.
Hata kama mama alikuwa wa kwanza kujulishwa, bado baba kama kapewa taarifa alitakiwa kuhudhuria tu.
Kama mzazi anaweza kuzira msiba wa mwanae inakupa idea ya aina ya mtu mwenyewe 'kisasi'
kama ana kisasi hadi cha msiba, kisasi cha kumlea kitakuwa kilikuwaje?
Kiafrika, msiba huondoa tofauti zetu hata kama ni kinafiki.
Kwetu uhayani mke anaitwa 'mukyala' (meaning mgeni/aliyekuja kutembea), kwetu mwanamke akiolewa ndo imetoka hiyo kwao atakuja 'kutembea' tu. Hata iweje akifariki atazikwa kwa mmewe hata kama walishaachana.Actually zamani kwetu mke angeweza kuachika na bado mtoto atakayezaa na mwanaume mwingine atakuwa ni wa former husband (anaitwa 'omwana webisisi). The same applies kwa watoto,watoto wako kwenye himaya ya baba hata kama walizaliwa na kukulia ujombani(bunyinarumi). Ndio maana kama ingetokea Mungu hajamchukua Kanumba kikwetu kama angeamua kuoa baba yake ndiye angemuolea (okumushwelelela) nandiye angemkabidhi mkuki (sio wajomba).
Nawapa pole sana wafiwa wote,Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
RIP Steve,tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.
halafu nahisi wanawake wa kihaya ni Tatizo.nimejionea wengi wanaachana na waume zao na kubaki na watoto.
Aisee mimi nilikuwa najiuliza inakuwaje hawa wasanii wanaongelea mipango ya harusi kwa kumshirikisha mama wakati yeye amesema baba yake yupo na hawana ugomvi? Pacho mwamba alipoulizwa na ile TV ya mchangani tv mawingu kuhusu haki za Kanumba akasema mama yake ndio atachukua. Sidhani kama baba ya Kanumba ametendewa haki, hii ni kwa kuwa wanawake wakiachwa huwa wanawajaza uongo watoto kuwa baba ndiye mbaya kuficha upuuzi walioufanya ukasababisha ndoa kuvunjika. Mtoto asipochanganya na zake anaishia kumchukia au kumdharau baba yake
Kwetu uhayani mke anaitwa 'mukyala' (meaning mgeni/aliyekuja kutembea), kwetu mwanamke akiolewa ndo imetoka hiyo kwao atakuja 'kutembea' tu. Hata iweje akifariki atazikwa kwa mmewe hata kama walishaachana.Actually zamani kwetu mke angeweza kuachika na bado mtoto atakayezaa na mwanaume mwingine atakuwa ni wa former husband (anaitwa 'omwana webisisi). The same applies kwa watoto,watoto wako kwenye himaya ya baba hata kama walizaliwa na kukulia ujombani(bunyinarumi). Ndio maana kama ingetokea Mungu hajamchukua Kanumba kikwetu kama angeamua kuoa baba yake ndiye angemuolea (okumushwelelela) nandiye angemkabidhi mkuki (sio wajomba).
Nawapa pole sana wafiwa wote,Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
RIP Steve,tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.
Umefafanua(wabitoitora) vema!