Utamaduni wa wahaya na kifo cha kanumba

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
WANAJF;
Kwanza naomba nitangulize pole kwa wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla kutokana na kifo cha mpendwa wetu Steven Kanumba. Sasa hoja yangu hapa ni moja tu kuhusiana na utamaduni wa Wahaya na kifo cha Kanumba. Hivyo, ninaomba hasa wale wenye uelewa (hasa watani zangu Wahaya) waweze kutupa maelezo hapa.

Hoja yangu ni kwamba je marehemu Kanumba ni Msukuma au Muhaya? Nauliza hili swali kwasababu kwenye gazet la mwananchi inasema hivi " Dada wa marehemu, Abela Kajumolo alisema kuwa mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican.

Alisema familia imepanga mazishi ya Kanumba yatafanyika Jumanne wiki ijayo na kwamba bado hawajaamua kama atazikwa Dar es Salaam au Bukoba," alisema.

Tayari kamati ya mazishi imeundwa na ikiwajumuisha Gabriel Mtitu, Stephen Jacob (JB) William Mtitu na Issa Mussa (Cloud) ambao wote ni wasanii wa filamu nchini.

Kamati ya usafiri itakuwa na Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Vincent Kigosi (Ray)".

Sasa swali langu ni kwamba kama Kanumba ni Msukuma na babake mzazi yuko Shinyanga ni kwanini option za mazishi ziwe ni Dsm na Bukoba na siyo Shinyanga kwao? nadiriki kusema kwao, kwani hata yeye marehemu alitambua hilo ndiyo maana anatumia jina la babake (Kanumba-hili si jina la kihaya bali ni jina la kisukuma), na pia alishatangaza kwamba atakwenda kugombea Ubunge kwao (Shinyanga na si Bukoba). hivyo alitambua fika kwamba yeye ni Msukuma na si Muhaya. Huko Bukoba ni kwao Mama yake, sasa kwanini marehemu akazikwe kwa bibi yake wakati ana kwao (Shinyanga)?

Nalazimika kuuliza hili swala kuhusu mila za watani zangu Wahaya kwasababu hata familia yangu haya yalitukuta mwaka jana tupofiwa na mke wa kaka yetu hapa Dsm. Kaka yetu alimwoa shemeji ambaye alikuwa ni muhaya na waliishi kama mwaka 1 kabla msiba haujamkuta shemeji. Sasa msiba ulipotokea ndipo Wahaya wakasema wanataka msiba ukafanyikie kwao mwanamke kwasababu mila zao zinawataka kufanya hivyo. Hili lilikuwa jambo gumu sana kwetu sisi ambao si Wahaya kwasababu binti yao alishaolewa na kaka yetu, hivyo kwa kuangalia mila zetu ni kwamba akiwa kwetu hawezi kuhamisha mila zao na kuzifanya ziwe za kwanza. Mke alipokubali kuolewa naye sasa anakuwa kwenye familia nyingine na taratibu za mila za kabila zake si rahisi zi operate kwenye culture nyingine. Tulivutana sana na kuwaeleza uhalisia wa tamaduni zetu na hata jinsi ukweli ulivyo na kuwaambia kwamba huyu ni mke wa kaka yetu na ni mwanafamilia yetu na hiyo msiba uko kwetu na atazikwa kwetu. Na ndivyo ilivyofanyika, japo na wao baada ya mazishi waliondoka na kuhaidi kwenda kuweka msiba kwao (sijui kama ilifanyika ama la, sina hakika kwasababu sikufuatilia zaidi baada ya kusafiri).

Hivyo, naomba ufafanuzi hasa toka kwa watani zangu Wahaya katika hili hasa inapotokea misiba ni kwanini Marehemu akazikwe kwa bibi yake wakati ana kwao?

NB: Nawaombeni radhi wale wote nitakaokuwa nimewakwaza kwa namna moja au nyingine, lkn nimelazimika kuandika kwasababu yaliwahi kunikuta na hata sasa yanatokea kwenye msiba wa marehemu Steven Kanumba.
 
Mila za wahaya zinakubali mtu azikwe kwa baba yake kama ni me...kama ni ke na kaolewa basi azikwe kwa mpenzi mumewe..Mila za kiislam zinatutaka mtu akifa azikwe pale alipofia na azikwe haraka asisafirishwe kwa kua ardhi ni ile ile tu, hii inasaidia kuepuka gharama zisizo na ulazima afu vilevile kuepuka kumsubua maiti mara huku mara kule na adha nyingine kama maiti ikianza kuharibika
 
mimi navyojua kwa mila za kihaya kwasababu mimi mhaya pia, mwanamke akiolewa anakuwa part and parcel ya familia ya mwanaume hata akifa atazikwa kwa mwanaume si kwao.
Mtoto akifariki anazikwa kwenye upande wa mwananume si mwanamke.
Kuonesha msisitizo kipindi cha nyuma ilikuwa mwanaume hawezi kulala kwao mwanamke mila zilikuwa haziruhusu kabisa utaenda utembee hata kama ni saa 5 usiku itakubdi uondoke ukalale pengine.
Nakuongeza kuwa kutokana na mgogoro wa familia ulikuwepo baina ya kanumba na baba yake labda kwa kutotumia busara wameshindwa kumshirikisha baba yake kanumba kwenye huu msiba wa mwanae.
Hata mimi nilishangaa kumwona babake kanumba anahojiwa tbc anaongea mambo ambayo ni tofauti na tuliyo ambiwa na akina ray na pia hata kamati ya mazishi inasema aliyekuwa anasubiliwa ni mama hata baba hajamtaja.
sitaki judge lakini ukweli hii si mila ya wahaya huu ni mgogoro wao binafsi ambao nahisi utakuja waletea matatizo.
 
baba mzani alonga
[video=youtube_share;UwXpjzN65jE]http://youtu.be/UwXpjzN65jE[/video]

Ahsante sana kwa hii Video kwani japo limeweza kunipa ufafanuzi wa tatizo langu.
Sasa kwanini yule dada kaweka option ya Bukoba?
 
mimi navyojua kwa mila za kihaya kwasababu mimi mhaya pia, mwanamke akiolewa anakuwa part and parcel ya familia ya mwanaume hata akifa atazikwa kwa mwanaume si kwao.
Mtoto akifariki anazikwa kwenye upande wa mwananume si mwanamke.
Kuonesha msisitizo kipindi cha nyuma ilikuwa mwanaume hawezi kulala kwao mwanamke mila zilikuwa haziruhusu kabisa utaenda utembee hata kama ni saa 5 usiku itakubdi uondoke ukalale pengine.
Nakuongeza kuwa kutokana na mgogoro wa familia ulikuwepo baina ya kanumba na baba yake labda kwa kutotumia busara wameshindwa kumshirikisha baba yake kanumba kwenye huu msiba wa mwanae.
Hata mimi nilishangaa kumwona babake kanumba anahojiwa tbc anaongea mambo ambayo ni tofauti na tuliyo ambiwa na akina ray na pia hata kamati ya mazishi inasema aliyekuwa anasubiliwa ni mama hata baba hajamtaja.
sitaki judge lakini ukweli hii si mila ya wahaya huu ni mgogoro wao binafsi ambao nahisi utakuja waletea matatizo.

Ahsante sana kwa ufafanuzi mzuri sana.
 
Mila za wahaya zinakubali mtu azikwe kwa baba yake kama ni me...kama ni ke na kaolewa basi azikwe kwa mpenzi mumewe..Mila za kiislam zinatutaka mtu akifa azikwe pale alipofia na azikwe haraka asisafirishwe kwa kua ardhi ni ile ile tu, hii inasaidia kuepuka gharama zisizo na ulazima afu vilevile kuepuka kumsubua maiti mara huku mara kule na adha nyingine kama maiti ikianza kuharibika

Prof., ahsante kwa ufafanuzi japo mimi concern yangu siyo kusafirisha maiti bali ni kwanini kuwe na option ya Bukoba badala ya Shinyanga/Mwanza? Hilo ndilo lilikuwa concern yangu.
 
Ngoja aje Ta Muganyizi na Bishanga watoe ufafanuzi kuhusu hili.

Kwetu uhayani mke anaitwa 'mukyala' (meaning mgeni/aliyekuja kutembea), kwetu mwanamke akiolewa ndo imetoka hiyo kwao atakuja 'kutembea' tu. Hata iweje akifariki atazikwa kwa mmewe hata kama walishaachana.Actually zamani kwetu mke angeweza kuachika na bado mtoto atakayezaa na mwanaume mwingine atakuwa ni wa former husband (anaitwa 'omwana webisisi). The same applies kwa watoto,watoto wako kwenye himaya ya baba hata kama walizaliwa na kukulia ujombani(bunyinarumi). Ndio maana kama ingetokea Mungu hajamchukua Kanumba kikwetu kama angeamua kuoa baba yake ndiye angemuolea (okumushwelelela) nandiye angemkabidhi mkuki (sio wajomba).
Nawapa pole sana wafiwa wote,Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
RIP Steve,tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.
 
Umefafanua(wabitoitora) vema!
 
halafu nahisi wanawake wa kihaya ni Tatizo.nimejionea wengi wanaachana na waume zao na kubaki na watoto.

mkuu sio unaisi awo watu ni tatizo,wanajiona kama walizali tanzania kwa baati mbaya ovyo sana hawa watu.
 
Back
Top Bottom