Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania

Ndo inabidi waanze sasa kuandika taifa bila kujua history ya kiongozi wako ni kazi bure

Haiwabidi waanze kuandika. Ukisema inawabidi unaweka shuruti ambayo haipo.

Swala unaloongelea ni pana.

Kabla ya kuanza kutaka viongozi na wanasiasa waandike vitabu, inabidi jamii nzima ithamini kusoma. Andy Chande kaandika kitabu cha maisha yake, tena kakiweka mtandaoni kila mtu mwenye PDF akisome buree, sijui wanachama wetu wangapi wa hapa JF wamekisoma, au hata wanamjua Andy Chande ni nani katika historia nzima ya Tanzania.

Kitabu kipo hapa
http://andychande.com/A_KNIGHT_IN_AFRICA_by_SIR_JKC.pdf

Mtu mwenye njaa ambaye siyo tu hana muda wa kusoma, bali hana hela ya ziada kununua kitabu, hawezi kuthamini kusoma. Hivyo tuna kwenda kwenye suala la uchumi.

Kama huna sheria kama "Freedom of Information Act" inayoshurutisha watawala kutoa habari kwa waandishi wa habari kwa mfano, watakaoanika maovu ya wanasiasa, huwezi kuwapa sababu wanasiasa kuandika vitabu vitakavyoelezea matukio kutoka upande wao.

Na hata kama una hizi sheria, kama unaandika maovu kila siku na watu hawafuatilii (apathy) ndio unaona watu kama rais Kikwete wanasema "Ni upepo tu huu, utapita" hata hawajitetei kwa kutoa tamko la kuachiwa Salva, seuze kitabu.

Utamaduni wa kurekodi mambo kwa maandishi hatuna tangu zamani. Tungekuwa nao tungekuwa na maandishi yetu.

Hatuwezi kuwa na utamaduni huu kwa kuwataka wakuu watufanyie hisani ya kutueleza siri zao. Frederick Douglas alisema "Power concedes nothing without a demand. It never did and it never will".

Sasa, huwezi kuwaomba wakubwa waandike siri zao vitabuni. Unatakiwa kuwataka, kivitendo.

Na umma usio elimu utafanyaje hivyo? Kwa kuanza na kujielimisha.
 
Bookshop sio hoja vitabu vimejaa kwenye mitandao lakini jee wewe mleta uzi unasoma au ni ubingwa tu wa kushauri? watz wameandika vitabu vya maana mpaka mmoja kagundua equations of life zinazofumbua mafumbo yote katika maisha habari hiyo unayo? mtandao unaoitwa Home unaujua? na ukiutembelea utasoma kweli au kazi yako kuhimiza wengine? hebu na tuwe mfano wa yale tunyohimiza kwa wengine.......

Mkuu ninasoma vitabu na mwaka huu naweza kumaliza uandishi wa kitabu changu ndugu.huwa navipata ebay.vingine naletewa na marafiki.
 
Haiwabidi waanze kuandika. Ukisema inawabidi unaweka shuruti ambayo haipo.

Swala unaloongelea ni pana.

Kabla ya kuanza kutaka viongozi na wanasiasa waandike vitabu, inabidi jamii nzima ithamini kusoma. Andy Chande kaandika kitabu cha maisha yake, tena kakiweka mtandaoni kila mtu mwenye PDF akisome buree, sijui wanachama wetu wangapi wa hapa JF wamekisoma, au hata wanamjua Andy Chande ni nani katika historia nzima ya Tanzania.

Kitabu kipo hapa
http://andychande.com/A_KNIGHT_IN_AFRICA_by_SIR_JKC.pdf

Mtu mwenye njaa ambaye siyo tu hana muda wa kusoma, bali hana hela ya ziada kununua kitabu, hawezi kuthamini kusoma. Hivyo tuna kwenda kwenye suala la uchumi.

Kama huna sheria kama "Freedom of Information Act" inayoshurutisha watawala kutoa habari kwa waandishi wa habari kwa mfano, watakaoanika maovu ya wanasiasa, huwezi kuwapa sababu wanasiasa kuandika vitabu vitakavyoelezea matukio kutoka upande wao.

Na hata kama una hizi sheria, kama unaandika maovu kila siku na watu hawafuatilii (apathy) ndio unaona watu kama rais Kikwete wanasema "Ni upepo tu huu, utapita" hata hawajitetei kwa kutoa tamko la kuachiwa Salva, seuze kitabu.

Utamaduni wa kurekodi mambo kwa maandishi hatuna tangu zamani. Tungekuwa nao tungekuwa na maandishi yetu.

Hatuwezi kuwa na utamaduni huu kwa kuwataka wakuu watufanyie hisani ya kutueleza siri zao. Frederick Douglas alisema "Power concedes nothing without a demand. It never did and it never will".

Sasa, huwezi kuwaomba wakubwa waandike siri zao vitabuni. Unatakiwa kuwataka, kivitendo.

Na umma usio elimu utafanyaje hivyo? Kwa kuanza na kujielimisha.

Mkuu umeongea ya msingi ngoja tuwaamize watu ndo jambo la msingi sana.

Na pia wana jf wajipakulie hiko kitabu wasome.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kizazi cha akina Musiba, Shaban Robert, Ganzel nk sijui kimepotelea wapi?

Tutafute njia mbadala yakuhimiza vijana kusoma nakuandika vitabu,

Leo tunaanza kuhamaki wanapoibuka wapotoshaji wa historia ya nchi hii, badala ya kusahihisha makosa wao wanapotosha na kufarakanisha kabisa!

Nawengine wanakuja na takwimu za kitoto eti mie tayari nishasoma vitabu 33!

Ni vizuri kama umesoma kweli lakini je umeandika kitabu chochote? Na je taifa limenufaika vipi nakusoma kwako vitabu?

Baraza la kiswahili lichukue jukumu la kuhuisha juhudi za uandikaji wa vitabu na usomaji wake, hili litasaidia kukuza lugha yetu na utamaduni wetu.
 
Makala na vitabu vya watanzania mbona ni vingi sana. kwenye maktaba zetu za mashuleni, vyuoni na maktaba za mikoa zimejaa..Zipo pia makala nyingi za wasomi, wanasiasa na wanataaluma zinazotolewa sana kwenye magazeti/magazine/mitandaoni etc Sijui huo utafiti wako uliufanyaje.Mimi naona tatizo liko kwa wasomaji

Technolojia imerahisisha access ya wasomaji wengi kutumia mda mwingi mtandaoni kupata kila knowledge waitakayo pande zote dunia kwa online kuliko kutumia muda mwingi na gharama kutafuta vitabu physically etc .kama demand zake zimepungua Motivation za waandishi pia hupungua pia....
 
Umetoa ushauri mzuri sana mkuu.kweli watanzania tunatakiwa tubadilike maana asilimia kubwa wanasoma vitabu pale tu anapotaka kufanya mtihani fulani,mbali na hapo hawezi kujisomea kitabu kingine chochote kwa manufaa binafsi.Pia nimegundua maarifa unayopata kwa kusoma unaweza kukumbuka kwa muda mrefu kuliko ya kusimuliwa.
 
Makala na vitabu vya watanzania mbona ni vingi sana. kwenye maktaba zetu za mashuleni, vyuoni na maktaba za mikoa zimejaa..Zipo pia makala nyingi za wasomi, wanasiasa na wanataaluma zinazotolewa sana kwenye magazeti/magazine/mitandaoni etc Sijui huo utafiti wako uliufanyaje.Mimi naona tatizo liko kwa wasomaji

Technolojia imerahisisha access ya wasomaji wengi kutumia mda mwingi mtandaoni kupata kila knowledge waitakayo pande zote dunia kwa online kuliko kutumia muda mwingi na gharama kutafuta vitabu physically etc .kama demand zake zimepungua Motivation za waandishi pia hupungua pia....

Je vinawafikia watu na kuweza kuvipata mimi nimezunguka mahali kibao kutafuta vitabu nakosa.
 
Mwanangu FredKavishe ushauri wako mzuri sana ingawa mazingira tuliyo nayo hayaruhusu haya unayoshauri kufanikiwa. Mimi baba yako nilishaandika kitabu na kilichapishwa lakini kikakosa wasomaji. Pia wachapishaji wetu Tanzania wengi ni wababaishaji au wanaiogopa serikali hasa ukiandika mambo ambayo serikali haipendi. Mpaka ninavyoandika nina miswaada nane ambayo ilishakubaliwa na wachapishaji lakini baadaye wakasema hawatachapisha kwa vile serikali haitapenda. Kitabu changu kilikuwa kifundishwe mashuleni. Lakini baada ya muda nikaambiwa mara ukapa mara ukata mara hivi kiasi cha kunikatisha tamaa. Unatumia pesa yako kuhakikisha kitabu kinatoka. Ukiangalia mauzo unapata kichefuchefu.
 
Mkuu unaweza nisaidia nakala ya kitabu chako nitakipata wapi?
 
Usomaji wa vitabu unaongeza maarifa kwa hali kubwa sana. Ukisoma vitabu unaongeza maarifa sana, ni jambo zuri kujenga utamaduni wa kujisomea! Lakini ili kuongeza hamasa zaidi, inabidi kwanza jamii kubwa iweze kupata elimu japo ya msingi, kwani ni vigumu, mathalani mzazi aliye kijijini hana elimu aanze kuhamasisha familia yake au watoto wake waanze kujisomea vitabu!
 
Je vinawafikia watu na kuweza kuvipata mimi nimezunguka mahali kibao kutafuta vitabu nakosa.

Labda uwe specific,vya taaluma/field ya aina gani?

Usisahau pia kuna database za kutosha zenye Articles na vitabu mbalimbali electronically (vingine utalipia na vingine ni free).Taasisi nyingi duniani zinanunuahizo access kwaajili ya citation ya machapisho yao au data kwaajili ya analysis na decision making kwa mahitaji yao.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kizazi cha akina Musiba, Shaban Robert, Ganzel nk sijui kimepotelea wapi?

Tutafute njia mbadala yakuhimiza vijana kusoma nakuandika vitabu,

Leo tunaanza kuhamaki wanapoibuka wapotoshaji wa historia ya nchi hii, badala ya kusahihisha makosa wao wanapotosha na kufarakanisha kabisa!

Nawengine wanakuja na takwimu za kitoto eti mie tayari nishasoma vitabu 33!

Ni vizuri kama umesoma kweli lakini je umeandika kitabu chochote? Na je taifa limenufaika vipi nakusoma kwako vitabu?

Baraza la kiswahili lichukue jukumu la kuhuisha juhudi za uandikaji wa vitabu na usomaji wake, hili litasaidia kukuza lugha yetu na utamaduni wetu.

Kwa kweli ili kubusti waandishi wetu bakita linatakiwa kuhusika na mchakato mzima.
 
kiukweli nitakua wa mwisho kununua kitabu cha mwanasiasa..wengi kama si wote wanadhani wanajua kila kitu...yanini uuandikie kitabu umma ilhali pragmatism inaonesha umefeli na hakuna uhaueni wowote?
 
Labda uwe specific,vya taaluma/field ya aina gani?

Usisahau pia kuna database za kutosha zenye Articles na vitabu mbalimbali electronically (vingine utalipia na vingine ni free).Taasisi nyingi duniani zinanunuahizo access kwaajili ya citation ya machapisho yao au data kwaajili ya analysis na decision making kwa mahitaji yao.

Naongelea vitabu quality sio vitabu tu.
 
Utawezaje kupata wasoma vitabu wakati library zimekufa kifo cha mende, shule zetu zimekuwa za kata ubora wa elimu yetu ni reflection ya wanaoongoza. Failures wakipata madaraka madhara yake ndio hayo. Jiulize leo hii kwa nini TES ilikufa? Kwa nini kazi serikalini (Sio wakuu wachache) na mashirika ya umma hailipi?

Ukitaka kutengeneza pesa Tanzania lazima uwe mgeni au ushirikiane na wageni kuwakamua wazawa, ukiwa mzawa watakupiga vita ni wachache sana wanaofanikiwa. Viongozi ndio wako mstari wa mbele kujikomba kwa wageni na kuwadhalilisha wazawa wa nchi hii kuanzia JK mwenyewe.
 
Ndugu zangu kusoma vitabu na msongo wa mawazo haiwezekani.kusoma inabidi utulie kiakili nadhani hali mbaya za kiuchumi pia ni chagizo pia katika usomaji wa vitabu.
 
Utawezaje kupata wasoma vitabu wakati library zimekufa kifo cha mende, shule zetu zimekuwa za kata ubora wa elimu yetu ni reflection ya wanaoongoza. Failures wakipata madaraka madhara yake ndio hayo. Jiulize leo hii kwa nini TES ilikufa? Kwa nini kazi serikalini (Sio wakuu wachache) na mashirika ya umma hailipi?

Ukitaka kutengeneza pesa Tanzania lazima uwe mgeni au ushirikiane na wageni kuwakamua wazawa, ukiwa mzawa watakupiga vita ni wachache sana wanaofanikiwa. Viongozi ndio wako mstari wa mbele kujikomba kwa wageni na kuwadhalilisha wazawa wa nchi hii kuanzia JK mwenyewe.

Mkuu umeongea mengi mazuri inabidi tuzifufue library zetu.
 
Back
Top Bottom