Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania

Nadhani huwa anasoma prospectus za vyuo vya Marekani, nasikia ana mpango wa kwenda kuongeza shule baada 2015 hili swala la u DR wake kutokushemika linamkera sana.
 
..Naona unataka kutushawishi kwamba rais wetu anapend akusoma vitabu! Try again!
 
naomba kujua faida ya kusoma vitabu kwa wingi,Rais wetu ni msomaji wa vitabu na tumeshuhudia hata kwenye mikutano mbalimbali jinsi anavyotulia na mavitabu yake kusubiri kukaribiswa kwa hotuba,vile vile tuliona kule marekani muda aliokaa kule week tatu muda mwingi alikuwa library akisoma na kubukua mavitabu mbalimbali,naomba kujua faida kwa mtu kama huyu ambaye nchi inamshinda kuendesha huku akijikita kwenye usomaji vitabu kwa wingi ina maana anachosoma hakimsaidii kufanya kazi zake??,kwa mimi ambaye sio msomaji wa vitabu kuna tofauti gani na msomaji vitabu??


Hili ni suala mtambuka, kikawaida data ndizo huzaa information flani, information ambayo inatakiwa isomwe na kuzaa knowledge flani, ukishapata hiyo knowledge, understanding ya mambo hutokea/huongozeka na mwisho wa yote commulative understanding of issues hupelekea someone to have wisdom. Hivyo ili Rais au kiongozi afanye informed decisions na right judgement ya issues, sharti awe na clean and reliable data/statistics as well as up to date information ambazo hata akizisoma 24/7 hours apate right information.

Hapa kwetu mambo hayapo hivyo. Data/Statistics zilizopo kwenye vitabu vya Serikali yetu ni za uongo na zimejikita kwenye unafki na zimelenga kumwonyesha Rais kuwa uongozi wake upo kwenye right direction na kwamba huku chini kuna mambo mazuri yanafanyika, zinamweleza mambo yapo sawa kumbe in reality mambo hayapo hivyo. Sikiliza hotuba mbali mbali zinazotolewaga na viongozi wetu wakitembelewa na uongozi wa kitaifa. Mfano mwingine ni statistics za BOT kuwa uchumi unapaa!!!huu uchumi wetu jamani unapaa kwa kuascend au kudescend???kadharika takwimu za watumishi wa umma, hadi leo hazieleweki, sasa hapo kweli unategemea hata Rais akisoma vitabu vya wizara ya utumishi akavielewa vilivyo vitamsaidia nini ilhali vitabu hivyo vimecontain wrong information???

Sasa hivi ukimuuliza Rais, Tanzania ina watu wangapi, huwezi pata jibu la maana, sasa kama hujui nchi ina watu wangapi??hata ukikesha kusoma vitabu vitakusaidia nini???Mipango yote inaanzia kwenye namba ya watu unaowaongoza. Ukiangalia takwimu za rasilimali zetu e.g wanyamapori, Madini etc, Takwimu za mapato na matumizi, takwimu za kudhibiti uhalifu kama ujangili na kadharika ni hivyo hivyo. Lakini je!!ni kweli kuwa mambo yapo kama watendaji wanavyoeleza??Inawezekana vipi mambo kwenda sawa ilhali miaka yote kuna upungufu wa fedha katika kutekeleza miradi iliyopo kwenye budget???Au inamaana kuwa budget yetu sio realistic na inakuwa inflated makusudi???

Kwa hiyo TOP THINKER hata kama Rais atakesha akifungua vitabu na majarida, as long as information in those articles ni wrong, unreliable and outdated na ni za kinafki. haziwezi kumfanya rais awe na knowledge, understanding wala wisdom ya kusolve matatizo yetu. No wonder JK alipokuwa akihojiwa na BBC/CNN alisema wazi kuwa, haelewi kwanini Tanzania ni masikini.Kweli, hawezi kuelewa reality ilhali watendaji wanakufeed wrong information. So JK anakesha kusoma wrong information inayotokana na unrealistic/unreliable data/statistics. Aidha, inamfanya ashindwe kupata uhalisia wa mambo na hivyo kutopata real understanding of issues na hivyo katu hawezi fanya maamuzi sahihi na yenye busara.
Wenzetu walioendelea wamejikita kwenye takwimu ambazo ni reliable na ndio maana kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.
 
naomba kujua faida ya kusoma vitabu kwa wingi,Rais wetu ni msomaji wa vitabu na tumeshuhudia hata kwenye mikutano mbalimbali jinsi anavyotulia na mavitabu yake kusubiri kukaribiswa kwa hotuba,vile vile tuliona kule marekani muda aliokaa kule week tatu muda mwingi alikuwa library akisoma na kubukua mavitabu mbalimbali,naomba kujua faida kwa mtu kama huyu ambaye nchi inamshinda kuendesha huku akijikita kwenye usomaji vitabu kwa wingi ina maana anachosoma hakimsaidii kufanya kazi zake??,kwa mimi ambaye sio msomaji wa vitabu kuna tofauti gani na msomaji vitabu??

naona umeamua kumtusi JK indirectly!!!!
 
Yeye aendelee kujisomea tuu, nadhani mavitabu yake ni yale yenye Ramani za sehemu za utalii duniani so hutumia kujua locations za kwendaa!
 
Mtoa mada umetumia muda mrefu kuongelea swala la watu1) kutojisomea 2)Na hata wanaojisomea eti hawaelewi.Nasikitika kusema we ni mpotoshaji mkubwa tena mkubwa. Na kama ulidhani hutagunduliwa ndo umeshagunduliwa.Kilichokuharibia katika maelezo yako marefu ya kumtetea zito mfano ulioutoa.Kujisomea una maana gani, kama mtu hajasoma amewezaje kujibu, kwa akili yako unadhani jibu refu ndilo linalobeba uzito au ndio sahihi. Unaweza kujibu kwa kirefu bado ukajibu pumba tu.Na nani hakimu wa majibu makini na pumba, ni wewe au?acha arrogance szisizo na tija wewe! eti unasema wanajisomea hawaelewi:umejuaje?kwa vile swala lazito limeleta majibu tofauti, hivi inadhani watu wote mkiwa na uelewa uleule kuna sababu gani ya kujadili?Jitahidi umtetee zito lakini kumbuka for every action you do is an interpretable action(wapi na wapi tafsiri zikafafa?matofali sisi au ambayo nayo hata hayafanani), the same as the words you say.Najua ukisoma hii replay utasema sijaelewa kwa sababu iko tofauti na your line of thinking.Acha arrogance zako na ku-kid watu ili umtetee Zitto.
 
katika vitu vinavyonivutia sana ni kujifunza kusoma na kujisomea!!
Usomaji wa vitabu huleta elimu, lakini ukaririfu wa yaliyoandikwa kwenye vitabu huleta ufaulu wa Mithani. Ingawa wanaofaulu si wote wanafaulu kwa kukariri yaliyomo vitabuni. Kwa hiyo kama jamii inawapima watu kwa ufaulu wa mitihani badala ya ujuzi wa mambo, basi tabia ya kujisomea hufa yenyewe.

Kama mtu anajua kwamba kinachotakiwa ni cheti chenye ufaulu badala ya uelewa wa mambo, ni kwa nini watu wasinunue mitihani au vyeti? Ajira zinatolewa kwa kuzingatia vyeti na wala si ujuzi wa mambo, watanzania wajisomee ili iweje? Ukiangalia kwenye yale mashindano yanayoshirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Afrika Mashariki mbali ya wanafunzi wetu kutokuwa wajuvi wa Lugha ya Kiingereza lakini pia ni watupu kwenye uelewa wa vitu vingi sana.

Huwa najiuliza kama wale wanafunzi wanaopelekwa kwenye mijadala ile ndiyo wale walio bora kabisa kwenye vyuo vyao, basi hao wengine hali yao itakuwaje? Unaweza kukuta mtu ana shahada ya uzamili ya mambo ya lugha kutoka chuo kikuu lakini hana uwezo wa kuandika jambo kwa mririko mzuri akaeleweka.
 
Nimefanya uchunguzi wangu mdogo ya kugundua watanzania wengi hatupendi kuandika kuanzia makala wala vitabu pia kusoma vitabu navyo ni shida sana.

Jana nilimuuliza mwanasiasa, je ushawahi kuandika kitabu akajibu hapana! Hatuwezi kuendelea kama taifa letu watanzania hawatapenda kuandika vitabu. Wanasiasa na watu maarafu wenye mafanikio wengi hawana vitabu vya kuelezea history yao ya mafanikio toka wakiwa wadogo.

Pia watanzania ni wavivu wa kusoma vitabu ni wakati sasa wa kuamka na kuanza kujiwekea mfumo wa kusoma kitabu kimoja kwa miezi 3 kwa mwaka utamaliza vitabu zaidi ya 4 itakuwa sio mbaya kwako kuliko kukaa bila kusoma.

Wanasiasa wachache sana ndo waandika makala, kina Kitila, Zitto, Mnyika, Makamba January nk wengine sijawahi kuona wakiandika hata makala mpaka sasa wengine wamekaa zaidi ya miaka 15 bungeni mtu hana hata makala moja kwenye gazeti lolote, hata blog... hii inatia aibu.

Ni wakati sasa watanzania kuamka na kujenga mazoea ya kusoma na kuandika na kujibu hoja kwa kuziandika sio kukosa kama tunakumbuka CCM walipinga hoja ya CHADEMA kuhusu sera ya majimbo; je, ni wanasiasa wangapi walipinga kwa kuandika? Je, kuhusu elimu ya bure nao walipinga lakini hakuna aliyeandika kwanini haitawezekana ina maana wanasiasa wetu hawasomi ukijenga utamaduni wa kusoma unaweza ukakosa kitu kwa kuandika sio kusema haiwezekani leo lowasa anapita na kusema elimu bure inawezekana je ametuandikia wapi kutupa mchanganuo wake.

Ni wakati wanasiasa waanze kuandika,waanze kusoma vitabu kuweza kujenga hoja zenye mashiko vile vile kuelewa wanachoongea wanasiasa wa sasa wamekuwa hawahoji kama watanzania tumekuwa hatuhoji kitu kikija tunakikubali tu bila kuhoji na kukipinga kwa hoja na sio matusi na propaganda.

Hongera kwa mzee mwanakijiji na kampeni yake ya mpe kitabu mtoto asome mimi niliweza kupita nyumba 7 na kuwasomesha vitabu watoto siku hiyo tungekua na utamaduni huu kila nyakati hata mara 1 kwa mwezi ingesaidia sana.

Njia za kuweza kuhamsha hari ya kusoma kwa watoto wetu:
1. Wazazi wahakikishe wanatafute hata kitabu kimoja kwa mwezi awe anasoma na mwanae nyumbani hii itamjengea utamaduni wa mtoto kupenda kusoma na atakua nayo hadi akikua.

2. Kwenye safari ndefu tujitahidi kubeba hata kitabu kimoja cha kusoma ukiwa njiani

Changamoto zinazokabili soko la vitabu
1. Hakuna bookshop za ukweli hapa Tanzania. Wengi tunashindwa kupata vitabu tunavyotafuta maana wengi sio wasafiri wa kwenda nchi za nje wengi ni wakazi wa hapa

2. Vitabu vyetu bado ni low quality. Wengi wanakurupuka kuandika, tunahitaji vitabu ambavyo baada ya miaka 3 ukikisoma unaweza rudia tena kusoma na kusoma tena, sio kitabu tu.

Lazima tuanze sana kujenga huo utamaduni wa kuandika na kusoma lakini ni muhimu kuwa na Mfumo mzuri wa elimu kwa kila raia na kila mtoto aweze kupata hivyo vitabu ajenge nia ya kuvisoma hakika taifa litabadilika kutoka walalamikaji mpaka wajenga hoja.
 
Bora hao wanasiasa wengine wasiandike, maana watatutengenezea historia mpya ambazo haipo. Mfano kuelezea Tanzania ni muungano wa nchi mbili mwaka 11964, ikihusisha visiwa vya Pemba na Zimbabwe. Ila nakuunga mkono kwa kuhamasisha moyo wa kusoma vitabu kwa watoto, huu ni mtaji muhimu sana.
 
Bookshop sio hoja vitabu vimejaa kwenye mitandao lakini jee wewe mleta uzi unasoma au ni ubingwa tu wa kushauri? watz wameandika vitabu vya maana mpaka mmoja kagundua equations of life zinazofumbua mafumbo yote katika maisha habari hiyo unayo? mtandao unaoitwa Home unaujua? na ukiutembelea utasoma kweli au kazi yako kuhimiza wengine? hebu na tuwe mfano wa yale tunyohimiza kwa wengine.......
 
Back
Top Bottom