Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba mwamko wa Watanzania kujisomea vitabu au hata magazeti yanyohusu mambo ya jamii, siasa, uchumi na utamaduni ni mdogo
Tafiti zipi, zilifanyika lini na wapi? Ukilinganisha na nchi jirani zipi?
JF ni jukwaa la wanajamii. Jamii inajumuisha watu wa aina zote: wasomi wa ngazi tofautitofauti hata wasiosoma. Watu wa vijiweni wengi wao wanaelimu ndogo sana hutegemei kuwakuta wanajishughulisha na kusomea
Ndugu zangu wanajf,

Habari zenu za asubuhi ni matumaini yangu mu wazima wa afya na mpo kwenye mapambano ya kulisukuma gurudumu la maisha ya kila siku kwenye barabara yenye vikwazo ni vigingi heavy. Wale ambao Mungu hajawajaalia uzima kwa siku ya leo nawapeni pole na InshaAllah Mungu atawapa afya na kuweza kufanya shughuli zenu za kila siku kama awali.

Kuna jambo linanikera sana na nimeona nina wajibu wa kulitoa dukuduku hili. Inaaminika kuwa JF ni myumba ya "great thinkers" kwangu mimi neno "home of great thinker" lina maana kubwa sana! Ni kweli kunapokuwa na watu wenye kufikiri nje ya box ni sehemu ya kujipatia elimu mbadala ambayo huwezi kuipata darasani. Napenda kusema kuwa JF ni zaidi ya darasa! Ila kuna kitu kinaharibu na kitu hiki si kingine bali utamaduni wa kuelewa kile kinachopostiwa humu JF.

Kuna makala kadha wa kadha utakuta mtu amesoma kichwa cha habari na kuanza kujibu vitu ambavyo havimo kwenye mada husika! Nashindwa kuelewa vitu viwili je anaetoa comment ameelewa kilichoandikwa? au hajasoma habari yenyewe zaidi ya kile kichwa cha habari?

Lakini pia watu wanashindwa kuelewa kwamba kadri mtu anavyojisomea mambo mbalimbali, ndivyo anavyopanua wigo wa uelewa wa mambo yakiwamo mabadiliko ya dunia. Kwa hiyo, tabia ya kujisomea ina umuhimu mkubwa katika jamii kama wahusika wataweza kuzitumia ipasavyo. Tabia ya kujisomea inasaidia kwa kiasi kikubwa kupanua uelewa wa mtu katika maisha yake na kufahamu mambo mengi. Tena tabia hii inaweza hata kupunguza idadi ya vijana wanaoishi vijiweni na wanaotumia dawa za kulevya.

Wazazi tuna nafasi kubwa ya kujenga utamaduni wa kujisomea kwa watoto wetu, lakini mara nyingi utakuta wazazi hawana muda wa kukaa na watoto wao na kuwafundisha kujisomea vitabu. Matokeo yake wanafunzi wanapokuwa watu wazima (kama sisi hapa jf) wanakosa hamasa ya kupenda kujisomea na matokeo yake tunayajua. Ni kweli kuwa utamaduni huu wa kujisomea unajengeka vizuri zaidi iwapo utaanzia utotoni, lakini pia wanaoanza kupenda vitabu ukubwani si wachache.

J. K. Nyerere ana haya ya kusema (1967) alisema

Sote ni mashahidi jinsi watu walivyoipokea taarifa ya Mhe Zitto Kabwe kila mtu aliandika analolijua yeye. Wengi wetu tumemhukumu kuwa katangaza kugombea Urais 2015, wapo walioenda mbali wakasema "Nikajiuliza hivi ni kweli Zitto alitangaza nia ya kupambana na Slaa kuwania Urais kwenye kura za maoni?" mwingine amesema









Ukiangalia mfano hiyo hapo juu utagundua tofauti ya uelewa wa kila aliesoma "Ndio nautaka Urais - Zitto" . Je Zitto alisemaje?



Nina amini kama mtu atasoma kilicho andikwa content basi hawezi ku comment maneno tofauti au nje ya kile kilichoandikwa na si kichwa cha mada maana wakati mwingine kichwa cha habari kinakuvutia uisome habari lakini hakina uwiano na habari yenyewe ila kuna connection tu na habari husika.


Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba mwamko wa Watanzania kujisomea vitabu au hata magazeti yanyohusu mambo ya jamii, siasa, uchumi na utamaduni ni mdogo.

Hata unapoingia kwa mfano kwenye forum za nchi jirani utaona nakuamini watu wengi wanapenda kusoma na kuandika tofauti ya nyumbani kwetu.

Naona zifanyike jitihada za dhati kabisa kuamsha utamaduni wa kusoma kwa watanzania wote hii ni pamoja na wadau wa kuandika na utunzi kama kina MM na wale wa sekta ya propaganda kama kina Ritz watusaidie kukaapamoja kufanya utafiti na kujua kitu hichi kifanywaje ili hali iwe nzuri.

Kwa upande wa teknolojia kukua nchini nikiri imesaidia kupatikana mawasaliano ya kompyuta. Tunashukuru kwani imekuwa ni njia mojawapo ya kurahisha upatikanaji wa habari na hata majibu ya maswali kutokana na kuwekwa tafiti mbalimbali kwenye tovuti tofauti.

Kupitia kompyuta hizo, wanafunzi wanaweza kupata majibu ya maswali yao wanayoulizwa wakiwa darasani.

Kompyuta pia ni njia mojawapo ya kujisomea, hasa baada ya kuperuzi na utafutaji wa habari zote zinazohusu masomo, machapisho au siasa, hii ni moja ya faida za ujio wa teknolojia hiyo. Teknolojia hii imetuweka karibu kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na hata JF ila tofauti na hapa kwenye hasa kwenye hizi forums kwa wenzetu wa nchi za jirani utaona na kuamini watu wengi wanapenda kusoma, kuelewa na kuandika kile wanachokielewa. Samahani sana kama nitwakwaza ila ukweli sisi hapa JF kila mtu anajua hakuna anaetaka kujifunza kwa mwenzie hasa kwenye maswala ya siasa.

Hivyo ni vema Watanzania tuwe makini na matumizi haya ya teknolojia hizi mpya ili kizazi chetu cha leo kisiwe cha kumeza kila kitu bila hata kuumiza kichwa, nikiwa na maana ya kufikiri, kwa kuwa huo ndio msingi na malengo makuu ya usomi na ufahamu.

Nimeupenda sana ushauri huu kwa wana habari kama kina MM ulipata kutolewa na Bwana Walter Bgoya Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji Vitabu nchini na Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publishers na ninaona ni busara kama nikiwakumbusha tena kina MM ili na yeye awakumbushe wengine.

"Kama wasanii na waandishi wa habari hawajengi utamaduni wa kujisomea kamwe hawawezi kuwa wasanii au waandishi wa habari wazuri. Hii ni sawa na ziro kabisa. Hakuna njia ya mkato katika kuwa msanii au mwandishi mzuri ni lazima kusoma na kujua mambo mengi.

Wewe utawezaje kumuelimisha mtu kama hujajua masuala mbalimbali yanayomuhusu? Lazima tufanye utafiti na kujisomea mambo mengi ili tujue nini tunawahabarisha na kuwaelimisha wasomaji na wasikilizaji wetu. Ndiyo maana tunasema kama hujafanya utafiti huna haki ya kuongea"

Nikiwa nahitimisha makala hii, naomba nirudi katika maisha ya kawaida ya kila siku. Hii leo wapo watu wanashindwa kabisa hata kuchangia mawazo yao linapokuja suala la mijadala, mfano mjadala wa katiba uliopo sasa, matatizo ya umeme na miundo mbinu mibovu inayosababisha foleni zilizogeuka kuwa kero, mgombea binafsi na hata uanzishwaji mfumo wa vyama vingi wakati ule wa miaka ya 1990.

Na hii inatokana na watu hao kutokuwa na uelewa wa kutosha unaotokana na kujisomea au maarifa yanayopatikana kutoka katika vitabu, magazeti na maandiko mbalimbali.

Ni vema serikali na wadau wote nchini, waone umuhimu kutilia mkazo suala la kujisomea na kuandika maandishi (vitabu), kwa sababu kuwa na uhuru wa mawazo bila kuwa na mwamko wa kujisomea au kuandika ni kudumaa kwa maendeleo.

Na ni jukumu letu sisi kuweza kujiwekea utamaduni wa kujisomea na kukifahamu kile tunachokisoma.



Wasalam.

====

RECOMMENDED on JamiiForums:

Hivi Ndivyo Tabia Ya Kupenda Kujisomea Ilivyoboresha Maisha Yangu. Inawezekana Hata Kwako Pia

USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo
 
Watanzania wachache sana wana tabia ya kupenda kujisomea vitabu na majarida. Bahati mbaya yetu hiyo. Hata book shops ziko chache sana
 
Back
Top Bottom