Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Ndugu zangu wanajf,

Habari zenu za asubuhi ni matumaini yangu mu wazima wa afya na mpo kwenye mapambano ya kulisukuma gurudumu la maisha ya kila siku kwenye barabara yenye vikwazo ni vigingi heavy. Wale ambao Mungu hajawajaalia uzima kwa siku ya leo nawapeni pole na InshaAllah Mungu atawapa afya na kuweza kufanya shughuli zenu za kila siku kama awali.

Kuna jambo linanikera sana na nimeona nina wajibu wa kulitoa dukuduku hili. Inaaminika kuwa JF ni myumba ya "great thinkers" kwangu mimi neno "home of great thinker" lina maana kubwa sana! Ni kweli kunapokuwa na watu wenye kufikiri nje ya box ni sehemu ya kujipatia elimu mbadala ambayo huwezi kuipata darasani. Napenda kusema kuwa JF ni zaidi ya darasa! Ila kuna kitu kinaharibu na kitu hiki si kingine bali utamaduni wa kuelewa kile kinachopostiwa humu JF.

Kuna makala kadha wa kadha utakuta mtu amesoma kichwa cha habari na kuanza kujibu vitu ambavyo havimo kwenye mada husika! Nashindwa kuelewa vitu viwili je anaetoa comment ameelewa kilichoandikwa? au hajasoma habari yenyewe zaidi ya kile kichwa cha habari?

Lakini pia watu wanashindwa kuelewa kwamba kadri mtu anavyojisomea mambo mbalimbali, ndivyo anavyopanua wigo wa uelewa wa mambo yakiwamo mabadiliko ya dunia. Kwa hiyo, tabia ya kujisomea ina umuhimu mkubwa katika jamii kama wahusika wataweza kuzitumia ipasavyo. Tabia ya kujisomea inasaidia kwa kiasi kikubwa kupanua uelewa wa mtu katika maisha yake na kufahamu mambo mengi. Tena tabia hii inaweza hata kupunguza idadi ya vijana wanaoishi vijiweni na wanaotumia dawa za kulevya.

Wazazi tuna nafasi kubwa ya kujenga utamaduni wa kujisomea kwa watoto wetu, lakini mara nyingi utakuta wazazi hawana muda wa kukaa na watoto wao na kuwafundisha kujisomea vitabu. Matokeo yake wanafunzi wanapokuwa watu wazima (kama sisi hapa jf) wanakosa hamasa ya kupenda kujisomea na matokeo yake tunayajua. Ni kweli kuwa utamaduni huu wa kujisomea unajengeka vizuri zaidi iwapo utaanzia utotoni, lakini pia wanaoanza kupenda vitabu ukubwani si wachache.

J. K. Nyerere ana haya ya kusema (1967) alisema
… Books are a very important way to knowledge and to self-improvement; from them we can learn new ideas; new techniques of working and new methods. We can learn about the development of men in all its different aspects; we can broaden our understanding of other peoples and even of ourselves. All the experiences of mankind, all his discoveries and his inventions can be learned about through reading.

Sote ni mashahidi jinsi watu walivyoipokea taarifa ya Mhe Zitto Kabwe kila mtu aliandika analolijua yeye. Wengi wetu tumemhukumu kuwa katangaza kugombea Urais 2015, wapo walioenda mbali wakasema "Nikajiuliza hivi ni kweli Zitto alitangaza nia ya kupambana na Slaa kuwania Urais kwenye kura za maoni?" mwingine amesema

Sijui ikifika siku yenyewe na Zito aisipojitokeza kwenye kinyang'anyiro watu watasema nini!!

Zitto ni kibaraka wa CCM !
Lengo lake sio Urais bali kuivuruga Chadema.

Kuutaka uraisi si uhaini

Ooh boy!!

Ukiangalia mfano hiyo hapo juu utagundua tofauti ya uelewa wa kila aliesoma "Ndio nautaka Urais - Zitto" . Je Zitto alisemaje?

Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.

Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili.

Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo.

Nina amini kama mtu atasoma kilicho andikwa content basi hawezi ku comment maneno tofauti au nje ya kile kilichoandikwa na si kichwa cha mada maana wakati mwingine kichwa cha habari kinakuvutia uisome habari lakini hakina uwiano na habari yenyewe ila kuna connection tu na habari husika.


Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba mwamko wa Watanzania kujisomea vitabu au hata magazeti yanyohusu mambo ya jamii, siasa, uchumi na utamaduni ni mdogo.

Hata unapoingia kwa mfano kwenye forum za nchi jirani utaona nakuamini watu wengi wanapenda kusoma na kuandika tofauti ya nyumbani kwetu.

Naona zifanyike jitihada za dhati kabisa kuamsha utamaduni wa kusoma kwa watanzania wote hii ni pamoja na wadau wa kuandika na utunzi kama kina MM na wale wa sekta ya propaganda kama kina Ritz watusaidie kukaapamoja kufanya utafiti na kujua kitu hichi kifanywaje ili hali iwe nzuri.

Kwa upande wa teknolojia kukua nchini nikiri imesaidia kupatikana mawasaliano ya kompyuta. Tunashukuru kwani imekuwa ni njia mojawapo ya kurahisha upatikanaji wa habari na hata majibu ya maswali kutokana na kuwekwa tafiti mbalimbali kwenye tovuti tofauti.

Kupitia kompyuta hizo, wanafunzi wanaweza kupata majibu ya maswali yao wanayoulizwa wakiwa darasani.

Kompyuta pia ni njia mojawapo ya kujisomea, hasa baada ya kuperuzi na utafutaji wa habari zote zinazohusu masomo, machapisho au siasa, hii ni moja ya faida za ujio wa teknolojia hiyo. Teknolojia hii imetuweka karibu kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na hata JF ila tofauti na hapa kwenye hasa kwenye hizi forums kwa wenzetu wa nchi za jirani utaona na kuamini watu wengi wanapenda kusoma, kuelewa na kuandika kile wanachokielewa. Samahani sana kama nitwakwaza ila ukweli sisi hapa JF kila mtu anajua hakuna anaetaka kujifunza kwa mwenzie hasa kwenye maswala ya siasa.

Hivyo ni vema Watanzania tuwe makini na matumizi haya ya teknolojia hizi mpya ili kizazi chetu cha leo kisiwe cha kumeza kila kitu bila hata kuumiza kichwa, nikiwa na maana ya kufikiri, kwa kuwa huo ndio msingi na malengo makuu ya usomi na ufahamu.

Nimeupenda sana ushauri huu kwa wana habari kama kina MM ulipata kutolewa na Bwana Walter Bgoya Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji Vitabu nchini na Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publishers na ninaona ni busara kama nikiwakumbusha tena kina MM ili na yeye awakumbushe wengine.

"Kama wasanii na waandishi wa habari hawajengi utamaduni wa kujisomea kamwe hawawezi kuwa wasanii au waandishi wa habari wazuri. Hii ni sawa na ziro kabisa. Hakuna njia ya mkato katika kuwa msanii au mwandishi mzuri ni lazima kusoma na kujua mambo mengi.

Wewe utawezaje kumuelimisha mtu kama hujajua masuala mbalimbali yanayomuhusu? Lazima tufanye utafiti na kujisomea mambo mengi ili tujue nini tunawahabarisha na kuwaelimisha wasomaji na wasikilizaji wetu. Ndiyo maana tunasema kama hujafanya utafiti huna haki ya kuongea"

Nikiwa nahitimisha makala hii, naomba nirudi katika maisha ya kawaida ya kila siku. Hii leo wapo watu wanashindwa kabisa hata kuchangia mawazo yao linapokuja suala la mijadala, mfano mjadala wa katiba uliopo sasa, matatizo ya umeme na miundo mbinu mibovu inayosababisha foleni zilizogeuka kuwa kero, mgombea binafsi na hata uanzishwaji mfumo wa vyama vingi wakati ule wa miaka ya 1990.

Na hii inatokana na watu hao kutokuwa na uelewa wa kutosha unaotokana na kujisomea au maarifa yanayopatikana kutoka katika vitabu, magazeti na maandiko mbalimbali.

Ni vema serikali na wadau wote nchini, waone umuhimu kutilia mkazo suala la kujisomea na kuandika maandishi (vitabu), kwa sababu kuwa na uhuru wa mawazo bila kuwa na mwamko wa kujisomea au kuandika ni kudumaa kwa maendeleo.

Na ni jukumu letu sisi kuweza kujiwekea utamaduni wa kujisomea na kukifahamu kile tunachokisoma.

IF TOU WANT TO HIDE ANYTHING FROM AFRICAN, PUT IT IN THE BOOK,
habari ndo hiyo, we have to change

Wasalam.

====

RECOMMENDED on JamiiForums:

Hivi Ndivyo Tabia Ya Kupenda Kujisomea Ilivyoboresha Maisha Yangu. Inawezekana Hata Kwako Pia

USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo
 
Ahsante Mkuu kwa bandiko hili maridhawa,

naona na wewe umeamua kufanya kautafiti kwa kushusha nondo ndeefu ili kujua kama kweli kuna wasomaji.

Wasomaji wapo ila wakati mwingine msomaji anapata shida kutokana mwandishi au waandishi, pale mwandishi anapoandika (haijalishi anaandika nini) bila kuzingatia misingi ya fasihi andishi, hii inaweza kupelekea andiko husika kuchosha, kukera na kutovutia kusoma....

Sio kila mtu anaweza kuwa mwandishi ila inatakiwa jamii yote iwe ya wasomaji.

Kweli sakata la ile Makala ya "NINAUTAKA URAIS" limeleta mushkheri sana hadi wengine limetuchosha, ila kwa upande wangu nadhani ningewalaumu sana watu wangu kama kauli hyo ingetoka kwa mtu mwingine (au kama ye ndio ingekuwa mara ya kwanza kueleza alicho ulizwa) na sio huyo aliyetoa labda mjadala ungekuwa tofauti.

Kilichoathiri maandishi yake ni historia yake (rejea kampeni zake za ubunge 2010 kule kwao alieleza kuwa ndio mara yake mwisho kwenda kuomba kura za ubunge na 2015 ataenda kuomba kura za .......)

Hivyo kauli yake ya sasa ikarudi kama mwangwi hvyo sio mpya sana japo tu saiv alikuwa ameihariri, hivyo Mkuu Shossi hilo nalo lilichangia kuathiri mjadala hapa jamvini japo sitaki kutetea wakurupukaji ambao pia walikuwa wengi.

Kwa ujumla tatizo la usomaji miongoni mwa sisi watz sio tena kitu cha kuulizana bali kitu kinachohitaji mikakati husika toka kwa wadau mahsusi. Sio tena kuwalaumu au kuwasema.

Hilo ni tatizo na linataka mikakati ya kulitatua, hvyo labda tusaidie nini kifanyike kuwaokoa watz toka kwenye ugonjwa huo.
 
Kilichoathiri maandishi yake ni historia yake (rejea kampeni zake za ubunge 2010 kule kwao alieleza kuwa ndio mara yake mwisho kwenda kuomba kura za ubunge na 2015 ataenda kuomba kura za .......)
Hapo kwenye RED utamu wake unatakiwa mleta hoja analeta kitu analitical watu wanakisoma na kukikubali sio kusema historia yake na kuishia hapo.

Tatizo hili halipo kwetu sisi tu wasomaji wa kawaida lipo hata kwa wana siasa tunao humu ndani wakiulizwa wanakuja na majibu mafupi kama mkia wa mbuzi na yasiojitosheleza. Na mara nyingine atakuwambia "mimi ndio naujua ukweli ila namshitakia Mungu" kwanini usiueleze huo ukweli ili uongo ujitenge?

Swala la mada ya Zitto nimelitolea kama mfano tu lakini ukiangalia mada nyingine utaona jinsi gani watu michango yao inavyokuwa sio constractive! Kuna watu unasoma comments zao mpaka unafeel kweli huyu mtu ameandika kitu sawia mfano mtu anapotoa comment yake kuhusu utamaduni wa kusoma vitabu akasema.
IF TOU WANT TO HIDE ANYTHING FROM AFRICAN, PUT IT IN THE BOOK,
habari ndo hiyo, we have to change

Mtu huyo ametoa maneno machache sana ambayo mwandishi mahiri anaeijua fasihi anaweza kuandika kitabu chenye pages 1000!
 
..nadhani kuna tatizo la uandishi pia.

..je, tatizo hili linasababishwa na tatizo la kutokujisomea??

NB:

..kuhusu Zitto, nadhani unapaswa kuzingatia matamshi na mwenendo wake kabla ya kuandika makala ile.

..Wakati wa kampeni za 2010, akiwa jimboni kwake, alitamka kwamba hatagombea tena ubunge, kwamba come 2015 atakuwa Presidential candidate.

..nadhani "wingu" la tamko la Zitto la 2010 ndilo lililopelekea makala yake isisomeke unavyoona wewe ilipaswa kusomeka.
 
..nadhani kuna tatizo la uandishi pia.

..je, tatizo hili linasababishwa na tatizo la kutokujisomea??

NB:

..kuhusu Zitto, nadhani unapaswa kuzingatia matamshi na mwenendo wake kabla ya kuandika makala ile.

..Wakati wa kampeni za 2010, akiwa jimboni kwake, alitamka kwamba hatagombea tena ubunge, kwamba come 2015 atakuwa Presidential candidate.

..nadhani "wingu" la tamko la Zitto la 2010 ndilo lililopelekea makala yake isisomeke unavyoona wewe ilipaswa kusomeka.

Mkuu JokaKuu,

Heshima yako.

Napenda ujue kila mwanasiasa ana malengo yake binafsi na hakuna anaetaka sifa ya kutumikia wananchi halafu yeye afe masikini especial kwenye nchi zetu hizi za kiafrika. Wanasiasa wanakuwa na malengo yao ya kuutumikia umma na wengine kujiimarisha kiuchumi!

Zitto ni mwanasiasa ameshakuwa mbunge wa jimbo lake kwa muhula ziadi ya mmoja na pengine malengo yake ilikuwa awe mbunge mpaka 2015 baada ya hapo aombe ridhaa kwenye chama asimame kwenye Urais. Kila mmoja ana ndoto yake na pengine hiyo ni ya Zitto na anataka ai attain mimi sioni tatizo kabisa kwa mtu kusema nia yake ninamchukia yule anaefanya mipango ya chini chini akiulizwa anaruka futi 1000.

Kuhusu waandishi kuchosha ni kweli kuwa hata waandishi wanatakiwa wawe na utamaduni wa kusoma angalia makala za MM halafu linganisha na makala za Johnson Mbwambo mwandishi wa Raia Mwema halafu utaona makala ipi imeshiba nondo na mifano kadha wa kadha kutoka maadiko kadha wa kadha.

"Kama wasanii na waandishi wa habari hawajengi utamaduni wa kujisomea kamwe hawawezi kuwa wasanii au waandishi wa habari wazuri. Hii ni sawa na ziro kabisa. Hakuna njia ya mkato katika kuwa msanii au mwandishi mzuri ni lazima kusoma na kujua mambo mengi.
Wewe utawezaje kumuelimisha mtu kama hujajua masuala mbalimbali yanayomuhusu? Lazima tufanye utafiti na kujisomea mambo mengi ili tujue nini tunawahabarisha na kuwaelimisha wasomaji na wasikilizaji wetu. Ndiyo maana tunasema kama hujafanya utafiti huna haki ya kuongea"
 
Umenena mkuu, ila Kabla sijachangia chochote ngoja kwanza nifanye kau-tafiti Kama ni kweli anapo shambuliwa Mtu wa Imani fulani lazima ukomae kutetea hata kama kulikuwa hakuna haja ya kumtetea
 
Mkuu JokaKuu,

Heshima yako.

Napenda ujue kila mwanasiasa ana malengo yake binafsi na hakuna anaetaka sifa ya kutumikia wananchi halafu yeye afe masikini especial kwenye nchi zetu hizi za kiafrika. Wanasiasa wanakuwa na malengo yao ya kuutumikia umma na wengine kujiimarisha kiuchumi!

Zitto ni mwanasiasa ameshakuwa mbunge wa jimbo lake kwa muhula ziadi ya mmoja na pengine malengo yake ilikuwa awe mbunge mpaka 2015 baada ya hapo aombe ridhaa kwenye chama asimame kwenye Urais. Kila mmoja ana ndoto yake na pengine hiyo ni ya Zitto na anataka ai attain mimi sioni tatizo kabisa kwa mtu kusema nia yake ninamchukia yule anaefanya mipango ya chini chini akiulizwa anaruka futi 1000.

Kuhusu waandishi kuchosha ni kweli kuwa hata waandishi wanatakiwa wawe na utamaduni wa kusoma angalia makala za MM halafu linganisha na makala za Johnson Mbwambo mwandishi wa Raia Mwema halafu utaona makala ipi imeshiba nondo na mifano kadha wa kadha kutoka maadiko kadha wa kadha.

"Kama wasanii na waandishi wa habari hawajengi utamaduni wa kujisomea kamwe hawawezi kuwa wasanii au waandishi wa habari wazuri. Hii ni sawa na ziro kabisa. Hakuna njia ya mkato katika kuwa msanii au mwandishi mzuri ni lazima kusoma na kujua mambo mengi.
Wewe utawezaje kumuelimisha mtu kama hujajua masuala mbalimbali yanayomuhusu? Lazima tufanye utafiti na kujisomea mambo mengi ili tujue nini tunawahabarisha na kuwaelimisha wasomaji na wasikilizaji wetu. Ndiyo maana tunasema kama hujafanya utafiti huna haki ya kuongea"

Mohamed Shossi,

..sasa kumbe hata wewe mwenyewe unakubali kwamba Zitto katangaza nia!!

..au na mimi nasumbuliwa na tatizo la kujamii la "utamaduni wa kutojisomea"??

..hata mimi sina tatizo na Zitto kugombea Uraisi. tatizo langu ni TIMING ya matamko yake.

..hivi kweli was it "Presidential" kutoa tamko kwamba atagombea 2015, wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010, huku chama chake kikiwa na mgombea ktk uchaguzi[wa 2010] huo??
 
Mohamed Shossi,

..sasa kumbe hata wewe mwenyewe unakubali kwamba Zitto katangaza nia!!

..au na mimi nasumbuliwa na tatizo la kujamii la "utamaduni wa kutojisomea"??

..hata mimi sina tatizo na Zitto kugombea Uraisi. tatizo langu ni TIMING ya matamko yake.

..hivi kweli was it "Presidential" kutoa tamko kwamba atagombea 2015, wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010, huku chama chake kikiwa na mgombea ktk uchaguzi[wa 2010] huo??

Ni kweli Zitto ametangaza nia hata kama sio direct lakini timing za nini mkuu? kwani umeambiwa siasa ni kilimo kwamba unatakiwa kupanda masika au vuli ikianza?

Kweli nadhani hata wewe unasumbuliwa na huo ugonjwa wa kijamii wa kutojisomea je Zitto ndio kiongozi pekee duniani kutangaza anautaka ukuu wa nchi kabla ya muda?

Unajua kuwa Gerhard Fritz Kurt Schröder historia inasema kabla ya kuwa chancellor wa Ujerumani kuna siku alienda mpaka kwenye ukuta wa Ikulu ya Ujerumani na akasema kuwa siku moja na yeye atakuwa Chancellor na kuingia katika ule mjengo! Hiyo ilikuwa ni ndoto yake haina tofauti na ya Zitto kwani baadae Gerhard Fritz Kurt Schröder alikuja kuwa kiongozi wa Ujerumani kati ya mwaka 1998 mpaka 2005 pengine Zitto pia dream zake zikawa kweli who knows?

Halafu hivi Chama cha Zitto si kina neno Demokrasia au ile D kwenye CDM ina stand for what? JokaKuu mimi najua Demokrasia ina maana pana sana inampa mtu uhuru wa kusema anachokiona kinafaa bila kuadhiri katiba ya nchi au chama husika!

Mimi nadhani tutumie hii mitandao ya intanet kuweza kulifahamu vizuri neno demokrasia unless hii ya kwenye CDM iwe ina tafsiri nyingine pia tuijue.
 
Umenena mkuu, ila Kabla sijachangia chochote ngoja kwanza nifanye kau-tafiti Kama ni kweli anapo shambuliwa Mtu wa Imani fulani lazima ukomae kutetea hata kama kulikuwa hakuna haja ya kumtetea

Mkuu imani ya mtu haina nafasi kwenye kujenga nchi ambayo ina imani tofauti na itikadi tofauti. Nchi itajengwa na sisi wenye dini tofauti mbona hizi fikra za dini/koo na kikanda zinaturudisha nyuma sana. Hebu tafakari kabla ya kunena/kuandika kuwa na utamaduni wa kusoma kitu ukielewe kisha uchangie mchango ambao ni constructive unifundishe kile nisichokijua tuache tabia zetu za kiasili za kupuuza mambo ya msingi kukaliana kwa chuki, choyo na majungu yanayosukumwa na dini au itikadi za vyama!
 
Ni kweli Zitto ametangaza nia hata kama sio direct lakini timing za nini mkuu? kwani umeambiwa siasa ni kilimo kwamba unatakiwa kupanda masika au vuli ikianza? kweli nadhani hata wewe unasumbuliwa na huo ugonjwa wa kijamii wa kutojisomea je Zitto ndio kiongozi pekee duniani kutangaza anautaka ukuu wa nchi kabla ya muda? unajua kuwa Gerhard Fritz Kurt Schröder historia inasema kabla ya kuwa chancellor wa Ujerumani kuna siku alienda mpaka kwenye ukuta wa Ikulu ya Ujerumani na akasema kuwa siku moja na yeye atakuwa Chancellor na kuingia katika ule mjengo! Hiyo ilikuwa ni ndoto yake haina tofauti na ya Zitto kwani baadae Gerhard Fritz Kurt Schröder alikuja kuwa kiongozi wa Ujerumani kati ya mwaka 1998 mpaka 2005 pengine Zitto pia dream zake zikawa kweli who knows?

Halafu hivi Chama cha Zitto si kina neno Demokrasia au ile D kwenye CDM ina stand for what? JokaKuu mimi najua Demokrasia ina maana pana sana inampa mtu uhuru wa kusema anachokiona kinafaa bila kuadhiri katiba ya nchi au chama husika! mimi nadhani tutumie hii mitandao ya intanet kuweza kulifahamu vizuri neno demokrasia unless hii ya kwenye CDM iwe ina tafsiri nyingine pia tuijue.

Mohamed Shossi,

..NDIYO, kuhusu suala la TIMING, siasa inaweza kufananishwa na kilimo, kwamba kuna wakati wa kupanda, kupalilia, kuvuna, etc etc.

..kwa mfano: wakati wa kampeni ni kipindi cha kuomba ridhaa ya wananchi kwa uchaguzi husika. Kipindi hicho siyo cha kutangaza ndoto na nia za chaguzi zinazofuatia, ukizingatia kwamba mhusika ni mwanachama wa chama cha siasa.

..Zitto alikosea alipotangaza nia ya kugombea Uraisi 2015 wakati akipiga kampeni za ubunge wa 2010. Kitendo hicho kilizua maswali mengi[distraction] ndani ya CDM, ukizingatia kwamba chama kilikuwa kinampigia kampeni Dr.Slaa kwa nafasi ya Uraisi 2010--2015.

..wengine tulianza kujiuliza ikiwa Dr.Slaa, na Zitto, wana siri nzito kwamba Slaa ata-serve term moja tu. Au, labda Zitto tayari alikuwa anajua CDM na Dr.Slaa watashindwa ktk harakati zao za kusaka Uraisi 2010. Zaidi, je Zitto alikuwa amepanga kum-challenge a sitting president of his own party come 2015??

..kuhusu masuala ya Gerard Schroeder, tujiulize wakati anafanya yote hayo alikuwa na nafasi gani ktk chama chake au serikali. Kwa mtizamo wangu masuala haya yanategemea pia na nafasi ya mhusika ktk chama chake, serikali,na hata jamii. Labda tunaweza kujifunza kutokana na tukio la Ted Kennedy kum-challenge Jimmy Carter mwaka 1980.

..Ted Kennedy alikuwa ana-exercise haki zake za kidemokarasi, lakini wapo Democrats ambao hawajaweza kumsamehe Kennedy mpaka leo hii kwa kitendo kile. Kwa mtizamo wangu unapokuwa mwanachama wa chama cha siasa kama alivyo Zitto, basi unapaswa kuwa na balance kati ya ku-exercise ur democratic rights na maslahi ya chama chako.

..It is OK Zitto kuutamani Uraisi. Lakini nadhani kipindi cha kampeni za uchaguzi 2010 was not the right time kutangaza nia yake for 2015. Pia wakati huu wa kampeni za Arumeru siyo muafaka kutoa matamshi yale. Zitto angesubiri wakati chama chake kitakapoanza mchakato wa kumtafuta mgombea wa Uraisi, ndipo na yeye atangaze nia.
 
Utamaduni wa kutosoma TZ hauna madhara kwenye maswala ya siasa tu bali madhara yake yanaonekana kwenye sekta zote za kijamii....

Tatizo la kutokujisomea TZ linaanzia katika familia na linakwenda mpaka katika vyombo vyetu vya kielimu...e.g universities.....hili linatokana na utamaduni wa watanzania kupenda short cuts....watu hawapendi kujishughulisha/kutumia jasho lao ili kupata kile watakacho....matokeo yake ni wizi wa mitihani kuanzia ngazi za chini sana..eg primary schools....mpaka universities kuna wanaonunua mitihani.....au kusoma wakati wa mitihani tu......

Matokeo yake tunapata watu na viongozi wa hovyo hovyo kwenye utumishi wa umma....watu wenye kupenda shortcuts kwenye maisha.....watu wasiojishughulisha...watu rahisi..watu wasiotumia akili zao.....watu wapenda rushwa na vitu rahisi rahisi......athari yoote hii ktk jamii ya mtanzania inapelekea nchi hii kuwa pale ilipo leo....ndio sababu hata utaona viongozi wanakuwa wazito kujiingiza kwenye mashirikisho kama EAC.....maana wanawajua watu wao...hawako serious bado....

Tunajiuliza inakuwaje nchi imakuwa na mikataba ya hovyo hovyo na wawekezaji??majibu tunayo wenyewe....kwa nchi yenye watu/viongozi wasiopenda kusoma/kushughulisha akili zao unategemea iweje!!!!!
 
Kwa muda mrefu, kwa mujibu wa Jenerali Ulimwengu,sisi watanzania, tukiongozwa na wanasiasa walaghai,ambao bila sababu za msingi tunawahusudu, tumewekeza katika upuuzi na kujenga utamaduni wa kufuatilia habari nyepesi,zisizo na uhusiano wowote na mustakabali wetu.

Sasa ni sharti,iwapo tuna nia ya kusonga mbele, katika eneo lolote lile, tubadilike na tuanze kusoma majarida, magazeti na vitabu.

Madhara ya kutofanya hivyo yapo wazi:tunakosa uwezo wa kuchambua masuala kiuyakinifu,tunakosa stadi mbalimbali za maisha.Katika vijiwe wa kahawa, ndani ya daladala, vipindi vya redio na runinga, mitandao ya kijamii, katika maeneo yetu ya kazi,na hata bungeni kunakojadiliwa masuala mazito ya kitaifa,tunaendesha mijadala isiyo na kina,hili linaweka wazi ombwe la maarifa miongoni mwetu.

Aidha,tutajikuta,mara kwa mara,tunakuwa subjects wa wanasiasa wakati haikupaswa iwe hivyo..Sababu kadhaa zinatolewa kuwa vyanzo hivyo vya maarifa ni ghali na watanzania ni maskini.

Ingawa hii yaweza kuwa na ukweli ndani yake,inakuwaje ,kwa mfano ,mtu mwenye kipato cha kukidhi mahitaji muhimu ashindwe kununua japo gazeti?
 
FortJeasus

Vyanzo vya habari TZ si shida kabisa.....tena siku hizi kuna internet sehemu nyingi.....na magazti ya maana yapo mengi tu...lakini watanzania mambo utakayokuta wanajadili(tena wengine wasomi tu)ni mambo ya starehe na udaku tu....watanzania wanajulikana kwa kupenda anasa...

Nguvu inayotumiwa na watanzania kwenye mambo ya anasa ingekuwa inatumika kuijenga nchi...tusingekuwa hapa tulipo leo.....watu wanakaa kwenye mitandao e.g fb..kinachoendelea humo ni starehe tu...nani kamchapa mke wa mtu au nani anatoka na star gani?..nani kapiga deal ya kuibia serikali wapi...au mpira...man u kamfunga arsenal etc etc etc..story ndio hizo hata vijiweni...tena haijalishi..

Wasomi na wasio wasomi story ndio hizo...ukiangalia aina ya magazeti yanayosomwa...ni udaku...nani kabakwa wapi etc etc...kama ni magazeti ya siasa....ndio unasikia maji taka....kuna magazeti makini yenye issues...e.g raia mwema, the guardian, citizen,or the east african....lakini wanaosoma wachache....

Tatizo kubwa la kusoma mambo liko vijijini ambako ungetegemea watu wangekuwa up to date na issues lakini huko ni msiba mkubwa kwani watu hawawezi kusoma/kuandika na hata kama wangeweza....muda wao mwingi wanautumia au shambani au kutafuta kuni na maji......ndio sababu inakuwa rahisi kwa watawala dhalimu kuwadanganya raia na kupata kura zao kwa urahisi.......
 
naomba kujua faida ya kusoma vitabu kwa wingi,Rais wetu ni msomaji wa vitabu na tumeshuhudia hata kwenye mikutano mbalimbali jinsi anavyotulia na mavitabu yake kusubiri kukaribiswa kwa hotuba,vile vile tuliona kule marekani muda aliokaa kule week tatu muda mwingi alikuwa library akisoma na kubukua mavitabu mbalimbali,naomba kujua faida kwa mtu kama huyu ambaye nchi inamshinda kuendesha huku akijikita kwenye usomaji vitabu kwa wingi ina maana anachosoma hakimsaidii kufanya kazi zake??,kwa mimi ambaye sio msomaji wa vitabu kuna tofauti gani na msomaji vitabu??
 
Usishangae muda mwingi JK anasoma vitabu vya katuni hasa Tom & Jerry pamoja na Power Puff Girl ndio maana kila akikutana na Wadanganyika wakati akiwahutubia anakuwa anacheka cheka maana anawaona kama vikatuni!

Usitegemee anagain chochote kwa kusoma vitabu ni mikatuni tu imemjaa kichwani!
 
Ifike mahali Watanzania tuache kusoma mambo yasiyo na faida katika maendeleo yetu. Leo ukipanda gari, utaona watu wengi wameshika magazeti ya udaku. Ni ni mara chache kuona mtu ameshika kitabu akijisomea au magazeti yanayoelimisha.
 
Inawezekana anafikiri anasoma vitabu kumbe anaangalia picha! Pengine anasoma hadithi za bulicheka.
 
No! Usomaji gani usio na tija? Flamboyant anaweza kuwa mkweli, maana tija ya usomaji huo ipo sirini.
 
Siamini kama JK ni msomaji mzuri wa vitabu ila pia naomba mnisaidie kama tozi huyu amewahi kuandika kitabu na kipo tusaidiwe kinaitwaje?
 
Back
Top Bottom