Utakiona cha mtema kuni!, Kama ni hadithi , ilikuwa kwenye kitabu gani? Mtunzi alikuwa nani...na mengineyo....

Habri za asubuhi wadau!?

Naomba kuelewa chanzo hasa cha hiyo kauli "... cha mtema kuni". Je hiyo ilikuwa ni hekaya au nini hasa?

Na kama ni hekaya kama zilivyo za Abu nuwasi, je Kitabu chake kinaetwaje ili nijue ni nini hasa kilimpata huyu mtema kuni hadi leo huwa tunatishwa kukiona alichokiona mtema kuni.


Mtema kuni maana yake ni mkata kuni!
Kuna vitabu vya ngano za kale vilikuwa na hadithi iitwayo kisa cha mtema kuni! Kipo kwenye archives za Google Books labda, niliwahi kukisoma zamani ila siikumbuki habari yake vyema, nitajaribu kusimulia kwa kadiri ninavyokumbuka.

Mtema kuni mmoja alikuwa akizoea kuenda mwituni kukata kuni kila leo, hakuyapenda maisha yake! Siku moja bibi kizee mmoja alimfiuata huko msituni na kumuambia mimi ni malaika, sema una shida ipi nikusaidie, jamaa akasema shida zake na yule kizee akampatia(sikumbuki kama ni mayai ama mashoka) matatu. Akamuambia atumie moja kila alipokuwa na shida na akahitaji suluhisho.

Kisa hiko kinaelezea matukio ya kusababishwa na ujinga mara tatu yaliyomfanya mtema kuni yule yale mayai/mashoka yote alopewa na kizee yule! Basi alirudi tena kwenye kazi yake ya kutema kuni, yule kizee alikuja tena wakati mwingine na kumuuliza vipi mbona bado ungali ukikata kuni? Akamjibu yaliyomsibuna ujingawe bbasi ama hapo yule bibi alimchapa viboko sana ama alimpa adhabu nyingine fulani hivi. Hiko ndio kisha cha mtema kuni!|

Matumizi sahihi ya kauli onyo hii ni pale mtu anapokuwa anafanya kosa ama mzaha fulani na kuurudia rudia ndio hukanywa kwa kuambiwa kwamba punde tu atakiona cha mtema kuni, yaani ataona kile kilichompata huyo kwenye ngano ya hapo juu!
 
Tokea zanani mtu akitaka kukutisha anakuambia utakiona cha Mtema kuni. Tishio hilo limekwenda hivyo miabka mingi tuu na watu tumeona ni maemo wa kawaida tuu.
Lakini juzi Rais wetu alipohutubia hadharani na kusema wapinzani waandamane na "Watakiona cha Mtema kuni"
Sasa hebu tuelimishane Hugo Mtema Kuni alikiona kitu gani?
 
Swala linanitatiza, kisa cha mtema kuni,
Ni lipi lilomkwaza, kwa kumtaja vinywani,
Akatufanya kuwaza, mtema kuni ni nani,
Kisa cha mtema kuni, alifanyani?

Kisa cha mtema kuni, ni kauli ya zamani,
Wahenga walibaini,kisa chake kwa undani,
Sisi akhiri zamani,hatukimanyi yakini,
Kisa cha mtema kuni, alifanyani?

Katika kutema kuni, kilichomsibu nini?
Alikutana na nini,alipofika porini?
Au watu wamebuni, kufurahisha uneni?
Kisa cha mtema kuni, alifanyani?

Nilidhani akilini, alipotea mwituni,
Baada kutema kuni, katumbukia shimoni,
Hakutokea nyumbani, mwisho wa mtema kuni,
Kisa cha mtema kuni, alifanyani?

Nilibuni fikirani,alikutana na jini,
Kapelekwa baharini,akazamishwa majini,
Baada ya siku tisini,akarudishwa nchini,
Kisa cha mtema kuni alifanyani?

Mambo mengi nilidhani, juu ya mtema kuni,
Kakata mzeituni, ukanena ewe nani?
Ukamkwida shingoni,mbio akazisaini,
Kisa cha mtema kuni,alifanyani?

Swala hili si utani, limenikwaza amini,
Nalianika ugani, msawiri bloguni,
mtafakari makini, wa Mrima na wa Pwani,
Kisa cha mtema kuni, alifanyani.

Nahitimisha uneni, wasomaji bloguni,
Naomba nipokeeni, jawabu lenye mizani,
Makene wa kasirini,na wengine duniani,
Kisa cha mtema kuni asili yake ni nini?

Shairi hili niliwahi kuliandika katika magazeti ya Mwananchi Juni 23 2001 na Nipashe Juni 19 2001 lakini hadi sasa sijapatiwa jibu nimeamua kulikariri katika blogu asaa huenda nitapatiwa jibu la kuniridhisha.

Wakatabahu.
 
nimekuwa nasikia utukiona cha mtema kuni au utapata cha mtema kuni. ninini hasa kilimpata huyu mwanamke?
 
9f8a9a57a9d96f92002b66d0c7f34287.jpg
 
Habari zenu wadau, tumezoea kusikia hili neno "UTAKIONA CHA MTEMA KUNI"! Ikimaanisha kuna jambo baya litampata/atafanyiwa mtu fulani kama lilivyompata/alivyofanyiwa MTEMA KUNI.

MTEMA KUNI ni mtu anayetafuta kuni/anayekata kuni porini kwaajili ya matumizi ya kawaida (kupikia au kuuza).
Naombeni kujuzwa huyu MTEMA KUNI alifapatwa na madhila gani mpaka anatumiwa kama mfano hadi leo?
 
Kwa kifupi mtema kuni aliona au kupatwa na jambo ambalo mpaka leo hamna aliyewahi kulifahamu, alidhurika na akakutwa hivyo, lililompata ni kubwa, la ajabu, hamna ajuaye.

Ndo maana unapoonywa kwamba utakiona cha mtema kuni hata wewe hujui kama ni jambo au adhabu, ni ipi, ni siri , hujui lifuatalo kama vile ilivoshindikana kujua hasa alichokiona huyu mtema kuni. hii hutumika katika kuonya watu, maana kwa hulka ya binadamu, hata kama utamtenda jambo baya sana ila usimtajie, ukimtajia anajiandaa kisaikolojia, ndo maana unasikia mtaani mtu anakwambia "we, nichezee, nakuua na naenda kufia jela", kajiandaa na kifungo cha maisha au kunyongwa, yaani kuijua ile adhabu kunampunguzia makali fulani siku anapoamua kufanya kosa listaihilo hiyo adhabu.

Ndo maana , kwa mfano wanachuo wamefanya mgomo, afu serikali inatoa onyo kali, inasema wanafunzi wote warejee darasani, atakayekaIdi kukiona, sijui ushawahi kujiuliza kukiona nini? ukisema atakayekaidi atafukuzwa, ni rahisi wengine kupiga hesabu na kuzikubali gharama za kufukuzwa ili imradi wafanyiwe wakitakAcho hata kama kitafaidisha wengine.

Au askari wazuiapo maandamano hawasemi, atakayeandamana, tutampiga mabomu ya machozi, fimbo kwa wingi, risasi na mabuti, hapana, "ATAKAYEANDAMANA KUKIONA" eehe, kukiona nini? Hizi lugha si za bahati mbaya, zina maana na kazi yake. Ndo cha mtema kuni.
 
Aman iwe nanyi wapendwa
Ni siku nyingi sana huwa nasikia kisa cha mtema kuni

Je mtema kuni ni nani?
Je aliwahi kuwepo au tu ni story za kutunga?
Kitu gan kilimpata huyu mtema kuni?
Kwa kifupi naomba kujua kisa na mkasa mzima wa mtema

Maana huwa naona mtu ukifanya kosa unaambiwa utakiona cha mtema kuni hivyo bas naomba kujua mkasa huu

Nawasilisha

London boy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom