Utajisikiaje wakati mke wako anapokwenda kuchekiwa afya ya uzazi na Gynacologist wa kiume

Dr-of-three-Phd

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
202
30
Utajisikiaje wakati mke wako anapokwenda kuchekiwa afya ya uzazi na Gynacologist wa kiume? Wewe unakuwa umeongozana naye kisha dr anakuomba uwapishe? Mkeo huku nyuma anabaki akimfunulia utupu wake mwanaume baki!

Je hakuna njia mbadala ya kuingiza vidole/mkono?
 
Hii ni noma sana. Madaktari wengi siku hizi hawana maadili. Dr anatakiwa amcheki endapo kuna nurse around - hapohapo. Ndiyo taratibu. Mke wako anaweza kuomba nurse awepo akichekiwa. Mbadala wa vidole ni ultrasound.
 
Kwanza elewa Dr hana haki ya kumcheki mke wako bila ruhusa yake. Most of the time kuna namna nyingi zingine za kupima bila kumuingiza vidole (as you say) ila either inachukua muda, au ina bei au mbaya zaidi haina uhakika.
Pili fahamu ya kwamba Dr hana ruhusa ya kukuomba umpishe abaki na mke wako kama mke wako anataka wewe ubaki.
Next time uliza kuhusu exam zingine na kama hakuna kabisa basi omba ubaki na mkeo.
 
Hii ni noma sana. Madaktari wengi siku hizi hawana maadili. Dr anatakiwa amcheki endapo kuna nurse around - hapohapo. Ndiyo taratibu. Mke wako anaweza kuomba nurse awepo akichekiwa. Mbadala wa vidole ni ultrasound.

Hapo kwenye nyekundu umepotoka Chupaku....unaposema madaktari wengi hawana maadili kwa kigezo gani? Una statistics zozote? Au kwa sababu hospitalini kukitendeka mazuri 1000 hayataandikwa ila likitokea baya 1 inakuwa breaking news basi nawe unahukumu wahudumu wa afya kwa kufuata mkumbo tuu! Sio vizuri bana..

Ultrasound haiwezi kuwa mbadala wa physical examination...gynaecologist anapompima mwanamke si vidole tuu, vidole ni final..na sometimes kuotkana na tatizo lenyewe vidole vinaweza visitumike kabisaa. Lakini hata hivyo...hata huko ambako ultrasound machines zipo mpaka corridoni bado PV examination ni essential pale inapokuwa indicated.

Mwanamke anapofanyiwa PV examination kwanza anaombwa na anaridhia, kama hataki hakuna atakayemlazimisha. Pili kama amefuatana na mwenza wake (mumewe, mchumba), huyo mwenza ana haki ya kuwepo wakati mwanamke huyo anachunguzwa, na kama hayuko na mwenza wake..basi mwanamke huyo ana haki ya kuomba nesi awepo wakati anachunguzwa. Madaktari makini wengi huwa wanaita nurse aje awepo wakati wa kuwafanyia wanawake uchunguzi. Tatizo unakuta hospitali manesi habaa, utampata wapi huyo wa kuja kusimamia zoezi hilo wakati huyo huyo anahitajika wodini, clinic, etc?!

Usiwe na haraka ya kujudge kabla hujaangalia mfumo wenyewe ukoje...critically!
 
Niliwahi kuona katika kipindi kimoja cha Oprah jinsi Wanawake walivyokuwa wanalalamika kwa kuona kama wanadhalilishwa na maGynecologist. Wengi walidai kwamba saa nyingine Dr anakuwa amewaacha mwaaaa kisha hutoka kule chumbani kwa dakika kadhaa na kuwaacha hivyo hivyo bila hata kuwaambia wajifunike. Wengine walihisi walipokuwa wanaguswa guswa kwamba Dr alikuwa anapitiliza maadili na hivyo kufanya vitu ambavyo wanawake wale waliona havikustahili.

Oprah naye mwenyewe alidai kwenda kumuona Dr wake ilikuwa anafikiria mara mbili mbili mpaka kaamua kutafuta Gynecologist mwanamke na huo ndio ushauri aliowapa wanawake wengi waliolalamika kwamba hawako comfortable kila inapobidi kuwaona maGynecologist wao (wanaume)
 
Tatizo dr anapoingiza vidole we unaichukulia kwa maana zingine.. ichukulie kama kipimo tu mkuu after all dr akishamaliza examination yake husahau hapo hapo

BTW ; its has been done that way since time immemorial
 
Option ya kwanza ni kuomba kukutana na daktari wa kike, kama hakuna daktari wa kike, basi unachotakiwa ni kuulizia kwa watu wa karibu kama wanajua daktari ambaye ni mwadilifu.

Daktari anaruhusiwa kukagua sehemu yenye tatizo tu na si sehemu zingine zisizo uhusiana na tatizo lililo kupeleka kwake.

Mwenza wako anaruhusiwa kuwepo wakati wa kupimwa, ila mara nyingi uombwa kutoka nje ili kuepusha rabsha au kutokuwa comfortable na hali utakayoiona pale.
 
Utajisikiaje wakati mke wako anapokwenda kuchekiwa afya ya uzazi na Gynacologist wa kiume? Wewe unakuwa umeongozana naye kisha dr anakuomba uwapishe? Mkeo huku nyuma anabaki akimfunulia utupu wake mwanaume baki!

Je hakuna njia mbadala ya kuingiza vidole/mkono?
si anaumwa? lazima atibiwe ndo maana hata wewe ukipata tatizo kwenye njia ya haja kubwa mkeo ataombwa akupishe ubaki na dokta ili akuingizie kidole kwenje njia yako ya haja kubwa ili aweze kujua tatizo. nadhani na wewe utakua tayari tu tena bila mashaka kwakua unahitaji kupona.
 
ethically speaking Dactari yeyote anapokuwa anataka kumchunguza mgonjwa wa jinsia tofauti lazima pawe na NESI pembeni .. sijui kama tanzania hiyo inakuwa applied lakini hapa hospitali nilipo ni lazima... huwezi ukabaki na mgonjwa wa jinsia tofauti ukitaka kumfanyia uchunguzi sehemu zake za siri..

Pia ninyi mama zetu, dada zetu kama mtakuwa mnaona aibu request Nurse aje mule chumbani IF dactari wako wants to see your pelvis for food poison !?! una uhuru wa kohoji why ?! madactari ni watu wakuelewa na wakarimu sana.. ofcoz sometomes tunakuwa tunachoka baada ya kufanya kazi overnight but ukimuuliza polepole atakujibu tu. Na sidhani kama ni rahisi kwa dactari yeyote kupata ashki ya kimapenzi atapoona sehemu za siri za mmke.. hakuna cha ajabu we have seen them all on different colors/size on different diseases toka tunaanza med. school 1st year on the 1st semister on cadavers

TRUST US WE ARE DOCTORS
 
Hapo kwenye nyekundu umepotoka Chupaku....unaposema madaktari wengi hawana maadili kwa kigezo gani? Una statistics zozote? Au kwa sababu hospitalini kukitendeka mazuri 1000 hayataandikwa ila likitokea baya 1 inakuwa breaking news basi nawe unahukumu wahudumu wa afya kwa kufuata mkumbo tuu! Sio vizuri bana..

Ultrasound haiwezi kuwa mbadala wa physical examination...gynaecologist anapompima mwanamke si vidole tuu, vidole ni final..na sometimes kuotkana na tatizo lenyewe vidole vinaweza visitumike kabisaa. Lakini hata hivyo...hata huko ambako ultrasound machines zipo mpaka corridoni bado PV examination ni essential pale inapokuwa indicated.

Mwanamke anapofanyiwa PV examination kwanza anaombwa na anaridhia, kama hataki hakuna atakayemlazimisha. Pili kama amefuatana na mwenza wake (mumewe, mchumba), huyo mwenza ana haki ya kuwepo wakati mwanamke huyo anachunguzwa, na kama hayuko na mwenza wake..basi mwanamke huyo ana haki ya kuomba nesi awepo wakati anachunguzwa. Madaktari makini wengi huwa wanaita nurse aje awepo wakati wa kuwafanyia wanawake uchunguzi. Tatizo unakuta hospitali manesi habaa, utampata wapi huyo wa kuja kusimamia zoezi hilo wakati huyo huyo anahitajika wodini, clinic, etc?!

Usiwe na haraka ya kujudge kabla hujaangalia mfumo wenyewe ukoje...critically!

mkuu watu kama hawa huwa wanasikiliza story za magazetini ... mimi binafsi nilishawahi kushitakiwa na mgonjwa kwa attending wangu kwamba sikumchukulia seriously ... alikuwa na upper respiratory infection (common cold) ilikuwa nikipindi cha baridi huku, nikamwambia just go back home stay warm and drink more water. Jamaa alienda kunishtaki sikumchukulia serious, ilikumridhisha nikapewa penalty ya to stay over night for 2 days ilikuwa nikipindi nipo intern kabla sijaanza residency ..

my point nadhani kuna watu ni natural born hawa appreciate doctors & hawawamini
 
Kwa experience yangu nilivyokuwa shule madada wengi walikuwa hawapendi kabisa mambo ya per vaginal examination,yaani mkiingia wodini wanaona kinyaa ndo maana ukiangalia utakuta madaktari wa wanawake wenye jinsia ya kike ni wachache sana.ultrasound haiwezi ikawa mbadala wa physical examination hata siku mmoja.ethically kumlinda mgonjwa na kunilinda miye inabidi nurse awepo wakati wa examination ila kuna baadhi ya wakinamama wanaomba asiwepo mtu,ninachofanya nazungusha screen kwa mgonjwa ila nurse bado anabaki chumbani just in case.watu wengi wanafikiri tunapenda kuwaingiza wake zao vidole for no reason ila inabidi kutokana na ugonjwa wanaoumwa.kama haupo comfortable tafuta gynaecologist wa kike
 
Miaka ya nyuma Dr. lazima awe na Nurse hata wakati wa kupimwa Nurse anakuwa chumba cha jirani sana na pale Dr. anapopimia, sasa sijui kwanini Dr. awe pekee yake au ndo sayansi na teknolojia.
 
Miaka ya nyuma Dr. lazima awe na Nurse hata wakati wa kupimwa Nurse anakuwa chumba cha jirani sana na pale Dr. anapopimia, sasa sijui kwanini Dr. awe pekee yake au ndo sayansi na teknolojia.

Mamndenyi..huna haja ya kujiuliza kwa nini Dr awe peke yake, unaruhusiwa kuomba uwepo wa nurse au mwenza wako, una haki hiyo! Sa kama hukuomba na clinic ina upungufu wa staff nurses wako busy na mambo mengine (kwa kawaida clinic nyingi hata za private huwa hivi) kuna uwezekano mkubwa wa Daktari kutokumbuka kuomba uwepo wa nurse..lakini unaruhusiwa kumkumbusha!

Ila kama tukiwa honest...jamani madaktari wanaodhalilisha wanawake wakati wa kuwaexamine sehemu zao za siri wapo wachache sana (kama wapo), na pengine ni madaktari wa kada za chini (ambao hujiita madaktari japo siomadaktari bali ni wasaidizi wa madaktari katika kukabili uhaba wa madaktari nchini) ambao bado credility yao ethically ni questionable. Mara nyingi unapoona kwenye magazeti ya Udaku heading za sijui 'Daktari kafanya nini..' huwa si madaktari, bali ni hizi kada nyingine zilizo hospitali, lakini kwa sababu gazeti litauza zaidi ikiandikwa daktari basi tunadhalilishwa tu kila siku! Inavunjisha moyo sana..
 
Utajisikiaje wakati mke wako anapokwenda kuchekiwa afya ya uzazi na Gynacologist wa kiume? Wewe unakuwa umeongozana naye kisha dr anakuomba uwapishe? Mkeo huku nyuma anabaki akimfunulia utupu wake mwanaume baki!

Je hakuna njia mbadala ya kuingiza vidole/mkono?

Kiongozi,

Unapokwenda kupata ushauri wa afya, au, tiba kwenye vituo vya afya jifanye kama mtoto mdogo - maana - mficha ficha maradhi kifo umuumbua!
 
Riwa! .. Mfano ni magonywa gan huwa yanahitaji hiyo huduma ya kuingiza vidole kwenye kupima?
 
Mkeo ni mgonjwa na ahitaji kutibiwa, mwache daktari afanye kazi yake. Wivu wa mapenzi hautakusaidia chochote, mwache mama atibiwe uendelee kufurahia penzi lake.
 
Back
Top Bottom