Utajiri wa viongozi si wafanyabiashara

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Baada ya kuona mali walizonazo Yona, Mramba, Chenge, Lowasa, Sumaye,NK
naona ni vyema tukajiuliza, je ni kweli inawezekana kazi ya umma tanzania inalipa kuliko biashara , na utaalamu wa aina yeyote.
Sasa kama hii ni kweli ni kwanini wanasiasa wasiuueleze umma wa tanzania ni vipi huu utajiri unapatikana wakiwa watumishi wa umma ili kizazi hiki na kijacho kifanye vivyo hivyo, na watumishi wengi wa serikali waondokane na umasikini walionao???????????

Ukijafanya uchunguzi wa kivivu utaona mawaziri sitini kwa miaka 30 wanashikilia bajeti ya tanzania kwa takribani miaka kumi. Utajiri wao wangelipa au kama wamelipa kodi ni pato kubwa sana kwa taifa.

Kwa sababu hii si kweli wamegeuka kuwa nchi ndani ya wananchi, hii inamaana kwamba, hawa viongozi baada ya kuwapa kazi na ofisi za serikali kufanya kazi ya umma wakafanya kazi yao. Hawafanyi mikataba na nchi bali na wao wenyewe, hawajengi nchi bali wanajijenga kwa mtaji wetu.
Viongozi wetu wamegeuza nchi na kuwa vitega uchumi vyao! sasa tunashangaa.!!!!!

Kwa sababu hakuna biashara waliyofanya ikawapa huo utajiri hivyo utajiri wao sio halali.Ama waliiba mitaji, ama waliiba fedha taslim, ama waliiba mikataba, ama waliiba kwenye bajeti zao, ama waliiba pamoja na wachuuzi.Ama walilazimisha tenda nk............

Ni lazima ukaguzi yakinifu ufanywe kwa viongozi wote walioshika madaraka tangia uhuru na pale itakapo gundulika kiongozi alipata mali kwa kutumia kodi za watanzania tumfilisi na interest rate inayokubalika itumike.
Wapelekwe mbele ya sheria na haki itendeke.

Bila kufanya hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

money loundering ni sheria ambayo ipo hivyo itumike kwa yeyote atakeyeshindwa kudhibitisha mali zake na mtitiriko wake.Baada ya hapo tuanze kujenga nchi.

BILA KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUWEKA PLASTA KWENYE JIPU BILA KULITUMBUA.

Gharama ya ukombuzi wa kiuchumi ni kubwa kuliko kisiasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom