Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Bongo wote ni walaji tu,msitake kujifanya nyie members wote ni malaika. Leo hii mkipewa cheo mtakula kuliko hawa jamaa.
 
SIWEZI KUJIBU SWALI RAHISI KAMA HILO..JUST GOOGLE HIYO EOTF na WAMA watakuwa wameandika misaada yao ilienda wapi afteral ...kama umenielewa hata hiyo EOTF siungi mkono..ndio maana nikasema wafadhili waache kusaidia taasisi zote mfano wa WAMA ..ikiwemo EOTF.....kwani inaonekana pesa misaada haiwafikii wote....hata ninaposema afadhali EOTF ...upande wa distribution mwisho wa siku wote hawafai....
TUACHE TABIA YA KU TAKE COVER YA UKANDA NA UDINI PALE TUNAPOAMBIWA UKWELI ....

Mie ningeulizwa kuchagua baina ya hao mashetani wawili ningemchagua Mama Salma, huko kusini pamoja na mikoa kama Kigoma kumekuwa marginalised kwa muda mrefu sana na sioni kwanini hio WAMA iwe big issue wakati ni pesa za charity, sio kodi.

Hata ukiangalia miradi ya maendeleo na miundombinu wako nyuma and no one says shit, kwa sababu hakuna mtu wa kullobby na kuwakingia kifua.

Huu ndio ujinga ninaoukataa hapa, nchi inaendeshwa kilevi na imekuwa mismanaged for a long time. Lets be fair kwamba kuna maeneo yako marginalized na wao pia wanahitaji barabara, mashule & walimu wazuri, mahospitali etc.

Siko hapa kutetea sehemu wala dini yeyote, kila mtz anahitaji kujaliwa.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Sumaye ni fisadi tunajua wala mtu asitake kumtetea sababu anautaka urais ndiyo maana akaenda marekani kutafuta digrii

Na wewe nenda marekani ukatafute degree uje ugombee urais 2015 sio mbali. Au kama unayo,inakuwa easy zaidi; gombea 2015 kwani ni haki ya kila m-tz.
 
@omr umeonaee ,yani wabongo tumejaa unafki wa kufa mtu.hebu mnaojua hii issue mtuekee ushahidi hapa.maana isijekua ni kampen za majitaka.unaposema 'nasikia hiyo ni hearsay.bila ushahidi inabaki kua tetesi NOT Confirmed
 
bongo wote ni walaji tu,msitake kujifanya nyie members wote ni malaika. Leo hii mkipewa cheo mtakula kuliko hawa jamaa.

achana uhuni ndugu yangu, ukweli na usemwe, hata kama unamuuma mkubwa wako. Kuishi kwa mazoea kuwa wabongo wako hivi ndo makosa makubwa yaliyotufikisha hapa.unaachia watu wanaiba rasilimali zote za nchi huku ukidhani ni heli yao waliojaliwa!!!!!!!! Amuka ndugu yangu.
 
@omr umeonaee ,yani wabongo tumejaa unafki wa kufa mtu.hebu mnaojua hii issue mtuekee ushahidi hapa.maana isijekua ni kampen za majitaka.unaposema 'nasikia hiyo ni hearsay.bila ushahidi inabaki kua tetesi not confirmed

kama mtu anatuhumiwa uongo si-- akanushe? Dr slaa kamtaja akiwa igunga, r1 hajakanusha!! Jk naye hajakanusha, kama hukanushi inakuwa ukweli. Sasa unataka watanzania tusemeje???
 
naomba nimnukuu askofu mmoja alikua anahubir kule mwanza 'je kila mtu ajichunguze nikweli tunauchukia ufisadi au tunawachukia mafisadi kwasababu sisi hatujapata nafasi za kuwa mafisadi' mwisho wa kunukuu. Jichunguze nafsi yako uone inavyokusuta kama na ww ukipata chansi hutapata nafasi ya kujineemesha ww na ukoo wako. Acheni chuki binafsi!

Naona unajitahidi kujitoa ufahamu!! Ila ngoja nikukumbushe, hao viongozi wamebeba dhamana ya kuongoza nchi (kwa niaba ya watz), wangejitoa kama hawawezi na bado wana nafasi ya kujitoa.

Hata iwe mimi,lazima nijitambue kuwa ninapowawakilisha wananchi vibaya basi ipo siku nitahukumiwa. Uwanja wa biashara ni mkubwa sana nje ya siasa yenyewe; ila kwa nyie mambumbu mnaona siasa ndio mtaji pekee. Subirini sasa hukumu yenu...
 
Mhh..kwani yeye slaa nani hadi kila anaporoka jambo watu wakimbie kujitetea?acha hizo slaa si mungu,watu hawamtii mungu iwe vipi slaa akiongea watu wajikanyage kumjibu.SI AENDE MAHAKAMANI KAMA ANA EVIDENCE NA HUYO RIZ ATAkanusha ama kukubali.ulitaka akanushie kwenye media?sheria gani inasema hivo?
 
Huyo ridhwan anafikili hii uingereza yan akitoka baba yake anakuwa rais yeye ivyo anatafuta mapemaaaa hela ya kampen hila ajue awez kabisa kuwa rais wa tz hata awe bilionea hao wakoloni weusi watatuua wanatudanganya tumepata uhuru kumbe wap tumepata utulivu tuu aman hakuna kwan kwenye aman hakuna malalamiko hivyo tz hatuna uhuru ni maneno tuuuuu uhuru wanao wakina rostam,kikwete,lowasa na familia zao ila siku moja tuta waswaga selo
 
Mhh..kwani yeye slaa nani hadi kila anaporoka jambo watu wakimbie kujitetea?acha hizo slaa si mungu,watu hawamtii mungu iwe vipi slaa akiongea watu wajikanyage kumjibu.SI AENDE MAHAKAMANI KAMA ANA EVIDENCE NA HUYO RIZ ATAkanusha ama kukubali.ulitaka akanushie kwenye media?sheria gani inasema hivo?
Acha kubwatuka! Ukweli lazima usemwe!
 
Naona unajitahidi kujitoa ufahamu!! Ila ngoja nikukumbushe, hao viongozi wamebeba dhamana ya kuongoza nchi (kwa niaba yawatz kama hawawezi na bado

Hata iwe mimi,lazima nijitambue kuwa ninapowawakilisha wananchi vibaya basi ipo siku nitahukumiwa. Uwanja wa biashara ni mkubwa sana nje ya siasa yenyewe; ila kwa nyie mambumbu mnaona siasa ndio mtaji pekee. Subirini sasa hukumu yenu...
Kwani mtoto yule kamaliza shule 2008 na utajiri wa mabilioni anautolea wapi?Watu wataluuma yake hiyohiyo wameajiriwa miaka mingi na hawajapata hayo mabilioni,umakin unahitajika
 
Mtikila - ni mwendawazimu

Cleopa Msuya - Tunaomba maelezo ya nini kilichotokea 12/04/XX pale Morogoro (kweli wewe ni msafi)

Joseph Sinde Warioba - Sina comment - Uwaziri Mkuu wako uliishia kwa Mke! Strange!

Frederick Sumaye - What are you UP TO?

Tanzania Daima - Why are you becoming the Voice of "triplets"?

I feel Like Shooting someone - cold blood!

una maana 12/04/1980 mauaji ya Edward moringe sokoine? tupe ukweli mwana wa nchi yetu
 
Mhh..kwani yeye slaa nani hadi kila anaporoka jambo watu wakimbie kujitetea?acha hizo slaa si mungu,watu hawamtii mungu iwe vipi slaa akiongea watu wajikanyage kumjibu.SI AENDE MAHAKAMANI KAMA ANA EVIDENCE NA HUYO RIZ ATAkanusha ama kukubali.ulitaka akanushie kwenye media?sheria gani inasema hivo?

Wewe naona umeanza kudata mambo ya mungu yamekujaje hapa, kwa hiyo kama wewe humtii mungu unadhani ni wote, yaani unaona fahari kusema watu hawamtii mungu, no wonder chama na serikali yenu haina utii kwa wananchi wake, maana kumbe hata hofu ya mungu hamnayo?

Unaweza ukawa unakwazwa sana na dr slaa hasa kutokana na jinsi anavyowaendesha, lakini utake usitake pamoja na kwamba yeye sio mungu, lakini tayari akiongea watu wanajikanyaga, mfano mzuri ni huo wa kujivua magamba, bila ujasiri kama wa dr na wote wanaomuunga mkono mengi tusingeyajua, tungeendelea kufa kimyakimya kama wafuasi wa kibwetere (unamkumbuka? au ulikuwa hujazaliwa)

Mtanzania jenga moyo wa uzalendo ipende nchi yako acha kutetea maovu, lazima ipo sababu ya wewe kutetea ufisadi, ni lazima unafaidika kwa namna moja ama nyingine. lakini kumbuka unakula urithi wa wanao.

Tafakali
 
Kwani mtoto yule kamaliza shule 2008 na utajiri wa mabilioni anautolea wapi?Watu wataluuma yake hiyohiyo wameajiriwa miaka mingi na hawajapata hayo mabilioni,umakin unahitajika

Mkuu, swala la waliomaliza nae kutopata mabillion ni topic nyingine kabisa! Kila mmoja ana bahati zake,uzembe wake na mihangaiko yake.

Hapa swala ni kwamba siasa imetumika kama mtaji wa yeye kuchipukia na utajiri katika miaka ya karibuni. Wanamagamba hawa
 
@UKWELI gani ambao hauko supported with evidence dont get me wrong kwamba napigia debe ufisadi .naulizia kuhusu USHAHIDI.tuhuma haiwezi kuwa na ukweli kama hamna evidence.
Hili suala la mtu kukurupuka na kuanza kutaja majina hata mimi mbona naiweza.,bora mtikila huwa anakwenda mahakamani sasa slaa naye atake initiative hiyo.mtuhumiwa aweza kukaa kimya asikanushe but that doesnt mean he/she is guilt it is up to the accuser to PROVE.PERIOD
 
Hiv wewe ridhiwan na baba yako mnatutaka nini wa tz hapa nilipo mzee wangu anafikilia ada ya semister ya pil lakn nyie mnanunua mi sem trairel yan nyie mtajuta siku moja mngekuwa china mngekuwa marehem mda sana
 
Binafsi sina wasiwasi naelewa hizo mali ni za watanzania wote ni suala la muda tu atazikana mwenyewe na ninauhakika wa 95% zitarudi hazina.
 
wewe unayetafuta ushahidi kwani kuna ushahidi gani dhidi ya RACHEL? HI KASHFA NI MBAYA KWA KIKWETE NA ITAMWANGUSHA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom