Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Kazi ya mapacha watatu. Hata RZ1 mali wamempa wenyewe, na kwa kuwatumia watu wengine ili mkulu asiwaguse
 
KIKWETE KUBALI AU KATAA KUHUSU UTAJIRI WA HUYO BWANA MDOGO MTOTO WAKO,NCHI HII SIO KILA MTAWALA LAZIMA AWE BILLIONEA,UNARUDISHA NYUMA JUHUDI ZETU ZA KUREKEBISHA NCHI YETU,USIPOCHUKUA HATUA NILIZOKUSHAURI UTAONA MATOKEO YAKE:bored::bored::bored::bored:
 
Naaaaaaaam, anatakiwa ajibu tuhuma kuhusu mwanae. Au mwane ajitokeze aeleze baada ya kuhitimu degree yake ya sheria mwaka 2005 (kama sijakosea), amefanya miujiza gani yakuweza kuwa bilionea ili nasi tuige kwake tuwe mabilionea!!!!!!!!!!!! Vinginevyo, ni ufisadi ule ule wa akina rachel, na kwamba jk kaigeuza ikulu kuwa mtaji wa familia.
 
Hatimaye yale yaliyobashiriwa sasa yametimia. Ilizungumzwa huko nyuma kwamba hawa mapacha watatu wataanza kampeni ya nguvu ya kuchafua watu kwa stori za uongo ili hatimaye wote waonekane wamechafuka kama mkakati wao wa kubaki CCM kwa vile ni dhahir kwamba hawana pa kwenda kwa vile ni mzigo na hawana mvuto.

Kwa wenye akili na wanaoweza kufanya utafiti mdogo tu watagundua kwamba habari hizi hazina hata chembe ya ukweli kwa vile dhamira yake ilikuwa ni kutekeleza shabaha yao na kwa bahati nzuri kwao, haijakosa uungwaji mkono wa watu ambao ama hawajui mlolongo wa mbinu chafu za kujinasua.

Mtikila tunamfahamu, baada ya kupoteza relevance yake kwa jamii sasa amekuwa ni kama jeshi la kukodiwa ili aweze kuishi mjini.

Ndiye huyu huyu aliyekwenda kusaini petty cash voucher kwa Rostam kupata hela ya kuishi na akabana mpaka alipoumbuliwa. Leo anamuomba radhi Sumaye baada ya kutuhubiria watz juu ya uchafu wake huyu jamaa.


Tulishadokeza huko nyuma kwamba sasa hivi watatumika hata wale wenye mvuto na heshima mbele ya jamii ili kuwanasua mapacha hawa.

Tumeona Dr. akipaza sauti kwa vitu ambavyo tunajua havina ukweli. Haya ni matokeo ya hawa jamaa kujibanza kwa CDM ili wanusurike na panga hili la shaba linalowakabili.

Tanzania Daima sasa hivi ni sehemu ya Habari Corporation katika kuimba mapambio ya kuwasifu na kuwatakasa mafisadi hawa.

Tutayaona na kuyasikia mengi katika kipindi hiki cha kujaribu kurejesha gamba lakini ukweli ni kwamba jamaa ni LAZIMA WAONDOKE na hakuna msaada wa propaganda na upotoshaji wowote utakaosaidia kuwaondoa jamaa katika shida hii.

Ni mzigo wa sumu ambao ni lazima utokomezwe, naihurumia CDM inavyojaribu kujiua kwa kukumbatia wale wale iliyokuwa inawapigia kelele.
 
Naililia nchi yangu Tanganyika, kuishi kwa mjomba Tanzania nimechoka. Kwanza mjomba ana laana pamoja na utajiri alionao bado wanae ni masikini wa kutupwa yeye kila siku ni mlevi.

Wageni ndio wana faidi mali za mjomba mimi pamoja na kuwa mpwa wake simwelewi nikimwomba anirudishe kwa wazazi wangu ananizungusha. Sasa nimekuwa mtu mzima naondoka narudi kwa wazazi wangu Tanganyika kwani najua hata baraka zangu nilizipoteza nilipodanganywa nikaja kuishi kwa mjomba.

KATIBA MPYA ITAKAYOTURUDISHIA TANGANYIKA NI LAZIMA.
 
Tanzania Daima tunaomba mrudi kwenye kazi yenu, Kibanda na Ngurumo mnaelekea kuandika sana about names and not critics on issues, badala ya kuongelea ufisadi in general mnaongelea ufisadi na mapacha upande mmoja. kama mapacha upande wa pili.

Nauliza kwanini haya yasikae pamoja, upande wa pili hauna nafasi ni lazima uingizwe kwenye kapu moja kubwa la ufisadi.

CHONDECHONDE.
 
jibu hoja hiyo kikwete,halafu tunataka tujue kule ukweni kwako iringa kwa waarabu mbona ghafla amemiliki malori zaidi ya 100 kwa mara moja,kama mkeo mpya ndo plan zenu tunataka maelezo
 
Kazi ya mapacha watatu. Hata RZ1 mali wamempa wenyewe, na kwa kuwatumia watu wengine ili mkulu asiwaguse


Angekuwa safi si angekataa hizo mali, wewe mtu anayekula kwa ulafi akivimbia atamlaumu mpishi?

Ni ukweli usiofichika kuwa Kikwete na familia yake sasa wanakula bila hata ya kunawa, na karibu watavimbiwa na kutapikia viatu vyao na kuwachafua walio pembeni yao.

Kikwete amempa rafiki yake SUBASH PATEL mgodi wa chuma Liganga, huyu ndie ambaye anamjengea Kikwete majumba yake. Kupitia kampuni yao ingine ya ujenzi, kupitia biashara zao amejenga majumba yafuatayo ndani ya miaka 5 iliyopita.

1. Majumba ya rais Msoga Chalinze.


2. Jumba la rais Mikocheni


3. Nyumba ya rais Bagamoyo.


4. Magorofa ya rais yaliyopo mitaa ya Jamhuri Street, etc


Kikwete amempa mdogo wake tenda ya kujenga barabara ya Bagamoyo - Msoga ambayo alitumia kampuni ya Kikorea na kuwashirikisha SUMA. Ilikuja kuthibitika kuwa ile kampuni ya Kikorea haikuwa na uwezo, na pesa walishachukua na mdogo wake kukunja mgawo wake.

SUMA JKT na serikali ndio walioingia hasara kubwa. Kwa kuficha aibu jambo hili likafunikwa na tenda ya barabara hiyo akapewa mkandarasi mpya, ile kampuni yao rafikie, na kulipwa upya tena bila kufuata NCTS, au approval ya Bunge.


Mke wa rais ameendelea kufanya ufisadi nadhani anataka kumshinda Anna sasa. Anapita dunia nzima kuchangisha kupata pesa kwa jina la Tanzania. Lakini afadhali ya mwenzake alikuwa anakula na kupuliza, kwani misaada yake ya vitabu, vitanda, baiskeli za walemavu, compyuta etc, ilikuwa inasambazwa nchi nzima.

Yeye pesa zote anazopata kwa jina la Tanzania anazipeleka LINDI. Alipewa bilioni 10 na Bilionia wa Kijapani, akaenda kujenga shule, ambayo haifiki bilioni 3 na yingine akajenga hoteli ya kitalii LINDI.

Acha misaada mingi tu inayokuja, ambako sasa amejielekeza kuweka vitega uchumi. Yupo Marekani sasa ambako amepewa dola milioni 28, nadhani hizo pia nyingi zitaishia kujenga Magorofa kwa mgongo wa kuifanya taasisi iwe sustainable. Ni vema sasa makampuni yaka acha kuzipa taasisi, mfano wa WAMA pesa.


Huyo Ridhiwan ndio wala sina la kuongeza, yaliokuwa yameanzia huku sasa yanadhibitika na haya tunayoeleza sasa yatafuatia.

Afadhali ndugu yake Miraji, sio fisadi ukiachilia ulevi, at least anaweza kuongea watu wakamuamini.
Lakini hawa wengine wasubiri safari za mahakamani pale muda wa Rais utakapomalizika.
 
Hapo hatoki kwani aliyempa mwanae huo utajiri ni rostam na huyohuyo ndiye waliyepanga kutosa.
Hata al adawi alifuatwa kwake na huyo dogo.
 
Nape kama mjanja aongelee tena ishu ya ghorofa la UVCCM ambako kampuni yenye ubia na rais ndio imejenga pale. Kwanza lile jengo historia yake lilikuwa la taasisi moja ya dini likataifishwa wakapewa TANU YL.

Tunasubiri tu siku waliokuwa na ile plot wakianza kuidai, huwezi kutaifisha mali za watu kwa matumizi ya umma halafu baadaye unaibadili kwa matumizi ya binafsi sio ustaarabu.


Wazee wa zamani waatakuwa wanaelewa kuwa ile plot ilikuwa ya taasisi gani, watu wanasubiri tu kabla ya kuuwasha moto.


Huyo Nape ndio wa kumtetea Rizwan leo, mtu ambaye alikuwa ndio anamchafua kabla, unafiki tu.
 
Angekuwa safi si angekataa hizo mali...wewe mtu anayekula kwa ulafi akivimbia atamlaumu mpishi????

Ni ukweli usiofichika kuwa kikwete na familia yake sasa wanakula bila haata ya kunawa na karibu watavimbia na kutapikia viatu vyao na kuwachafua walio pembeni yao...

Kikwete amempa rafiki yake SUBASH PATEL mgodi wa chuma liganga....huyu ndie ambaye anamjengea Kikwete majumba yake ..kupitia kampuni yao ingine ya ujenzi.....kupitia biashara zao amejenga majumba yafuatayo ndani ya miaka 5 iliyopita......
1] Majumba ya rais Msoga Chalinze.
2]Jumba la rais mikocheni
3]Nyumba ya rais Bagamoyo..
4]Magorofa ya rais yaliyopo mitaa ya jamhuri street...etc

Kikwete amempa mdogo wake tenda ya kujenga barabara ..ya bagamoyo - msoga ..ambayo alitumia kampuni ya Kikorea na kuwashirikisha SUMA ...ilikuja kudhibitika kuwa ile kampuni ya kikorea haikuwa na uwezo ..na pesa walishachukua na mdogo wake kukunja mgawo wake...SUMA jkt na serikali ndio walioingia haasara kubwa....Kwa kuficha aibu jambo hili likafunikwa na tenda ya barabara hiyo akapewa mkandarasi mpya[ile kampuni yao rafikie] na kulipwa upya tena bila kufuata NCTS...au approval ya bunge.

Mke wa rais ameendelea kufanya ufisadi nadhani anataka kumshinda Anna sasa....anapita dunia nzima kuchangisha kupata pesa la jina la tanzania lakini afadhali ya mwenzake alikuwa anakula na kupuliza kwani misaada yake ya vitabu,vitanda,baiskeli za walemavu ..compyuta etc ilikuwa inasambazwa nchi nzima ...yeye pesa zote anazopata kwa jina la Tanzania anazipeleka LINDI.....alipewa bilioni 10 na bilionia wa kijapani ..akaenda kujenga shule ...ambayo haifiki bilioni 3......nyingine akajenga hoteli ya kitalii LINDI...,Acha misaada mingi tu inayokuja ...ambako sasa amejielekeza kuweka vitega uchumi....yupo marekani sasa ambako amepewa dola milioni 28...nadhani hizo pia nyingi zitaishia kujenga magorofa ..kwa mgongo wa kuifanya taasisi uwe sustainable...............ni vema sasa makampuni yakaacha kuzipa taasisi mfano wa WAMA pesa ....

Huyo rizwan ndio wala sina la kuongeza,.......yaliokuwa yameanzia huku sasa yanadhibitika ....na haya tunayoeleza sasa yatafuatia.........
Afadhali ndugu yake Miraj ...sio fisadi..ukiachilia ulevi...at least anaweza kuonge watu wakamuamini...lakini hawa wengine wasubiri safari za mahakamani pale muda wa Rais ukimalizika!!

Labda utukumbushe misaada ya mama Mkapa alikuwa anapeleka wapi..I mean kanda gani.??maana nchi hii inaelekea ya Nigeria na Ivory Coast hivi sasa kwa kasi ya ajabu..umoja na uzalendo aliotuachia Mwalimu unakanyagwa bila aibu mchana kweupe.
 
Sijui huyu Mtikila hizi nyeti huwaga anazitoa wapi tu.

EEh kaka..katika hizi inshu mtikila ni next level...na yeye anaamini kwamba akina Dk Slaa na wengineo wanamwiga yeye,yeye anaanzisha na wengine wanafata and not otherwise
 
Ukipata nafasi itumie vizuri! Ridhiwani inabidi apongezwe kwa kugrab opportuinity! Big up Ridhiwan, endeleza mapambano ya kutafuta hela!

Anatafuta au anachota? can he consider himself as a hustler? Nope. Huyu ni mwivi tu, tena hata soni hana.
 
Miafrika bana..yaani mtu anapewa dhamana ya uongozi na watu wake, kisha anashirikiana na maponjoro kuwaibia watu wake mafukara waliompa dhamana ya kuwaletea maendeleo.
 
Wandugu mimi bado nalilia KATIBA HURU NA MPYA kwa nchi yetu bila kujali chama gani cha siasa kitaendesha nchi miaka ya baadaye. Haya tunayosema malori 100 ni asilimia ndogo ya hela za viongozi wetu zilizo kwenye mabenki nje ya nchi acha miradi inayotumia majina fake ya viongozi wetu. Nani alikuwa anajua Ghadafi na watoto wake wana fedha nje kiasi hicho..as long pesa zinanufaisha mabenki ya nje hawajasema chochote ila siku ambayo hawakutaki madarakani watasema yote. Kuna umuhimu wa Ridhwan na baba yake kuona jinsi watanzania wanavyoteseka vijijini mahospitalini nk. leo wewe Rais unadiriki kuona mwanao anafuja pesa watu wanakufa kwa njaa... hakuna accountability, responsibility, humanity kwa mambo anayofanya Ridhwani..hajui kabisa kuna mwananchi anakosa sh. 500 yakununua dawa yeye anatumia roughly average ya Tsh. 50,000 kwa siku. Tukubali unapokuwa Rais automatically kuna benefits zitaenda kwa familia yako, atakuja mfanyabiashara au rafiki wa mwanao na kutaka kufanya biashara clean lakini kupata hiyo chance kupitia familia ya rais itakuwa rahisi...sawa lakini basi sikuchukua pesa za walipakodi .... sijui JK alifikiria nini kumruhusu mwanaye kuingia kwenye siasa ingawa ni uamuzi wa mtu lakini inaonyesha wazi kabisa wanataka kuleta uongozi wa kifalme na matokeo yake ni kama Libya, Egypt..tumeona jinsi urafiki wa mwana na Masha ulivyomtoa nje ya uongozi..... tusome nyakati ...viongozi wa kesho watakuwa kutokea miaka 35..hawajui uhuru sijui itikadi za chama bali watakuwa ni wachapa kazi na mlioondoka mzimu utawajia ikiwamo kupelekwa mahakamani kwa kutufanya vijana wa sasa kuishi maisha ya kubangaiza
 
Labda utukumbushe misaada ya mama Mkapa alikuwa anapeleka wapi..I mean kanda gani.??maana nchi hii inaelekea ya Nigeria na Ivory Coast hivi sasa kwa kasi ya ajabu..umoja na uzalendo aliotuachia Mwalimu unakanyagwa bila aibu mchana kweupe.

SIWEZI KUJIBU SWALI RAHISI KAMA HILO, JUST GOOGLE HIYO EOTF na WAMA watakuwa wameandika misaada yao ilienda wapi.

Afteral kama umenielewa hata hiyo EOTF siungi mkono ndio maana nikasema wafadhili waache kusaidia taasisi zote mfano wa WAMA, ikiwemo EOTF.

Kwani inaonekana pesa misaada haiwafikii wote. hata ninaposema afadhali EOTF, upande wa distribution mwisho wa siku wote hawafai.


TUACHE TABIA YA KU TAKE COVER YA UKANDA NA UDINI PALE TUNAPOAMBIWA UKWELI ....
 
Haya ndio maajabu ya karne wimbo wa tanzania daima kwa sasa ni kutetea mapacha watatu watanzania wenye nia njema tusilonunue hili gazeti kwani limekuwa kichaka cha kutetea mafisadi
 
Mtikila - ni mwendawazimu

Cleopa Msuya - Tunaomba maelezo ya nini kilichotokea 12/04/XX pale Morogoro (kweli wewe ni msafi)

Joseph Sinde Warioba - Sina comment - Uwaziri Mkuu wako uliishia kwa Mke! Strange!

Frederick Sumaye - What are you UP TO?

Tanzania Daima - Why are you becoming the Voice of "triplets"?

I feel Like Shooting someone - cold blood!

Just go and shoot, tunasubiria pa kuanzia tu kama Tunisia. Sorry that u have nothing to say about the main subject ,its likely that u r one of them
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom