Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Hili ni tone tu katika bahari. Wengi tu viongozi wetu wana hata ziaidi mara ishirini ya huyo.

Na bado baadhi ya vizito wanasema hawajui kwa nini watanzania kwa ujumla wao ni maskini.
 
Hilo la bima ya sh 60,000 (3rd party) tu nalo lilimshinda? Au ni huo mkanganyiko wa umiliki ndio ulifanya ashindwe kukata bima ya halali? Shame!
 
Hii ni kashfa kubwa sana. Nadhani badala ya kuchunguza kuuawa kwake kibao kingegeuzwa.

Hebu tazama mtumishi wa serikali tena wa ngazi ya juu vile anafanya uhalifu ambao ni jambazi tu ndio wenye kuufanya. Halafu bahati mbaya hawa eti ndio walinzi wa wetu na mali zetu!
Poor we!
 
Inakatisha tamaa
sana. Kama mlinzi wa kwanza wa sheria na amani katika mkoa anakuwa ndie
kinara mvunjaji sheria namba moja, who remains safe hapa??? Tukimbilie
wapi???

mnashangaa kwa Barlow RIP almost ma RPC wote wa mikoa kongwe na wakuu wa vikosi maalum kama reli traffic wana utajiri wa kutisha.
 
Jeshi, polisi vyote vinanuka rushwa, dhuluma na ujambazi uliokithiri. Taasisi zetu zote zimeoza.

mkuu hapa siyo rushwa tena ni ujambazi..Barlow inaonekana alikuwa anashirikiana na majambazi...
 
TAKUKURU nao hawakosekani humo pia
Mimi nafikiri siyo tatizo la uongozi, bali ni ile laana ambayo mtu mweusi anayo. Ebu fikiria mtu kama Barlow na umri wote huo anajenga Golofa? I think Black people are all Satan, Roho chafu kila mtu anataka ubinafisi, watoto wa wanakosa elimu, dawa hakuna wakati wengine wakijenga maorofa, it dosen't bring sense. Let us allow the white people to come back once again.
 
Mbona tumali twenyewe tudogo? Kaulizie mali za kamanda mstaafu SHIMBONI au wasiliana na Invisible akupe diteili uzimie!
 
mkisikia benki imeibiwa, majambazi wametoroka na mpesa gari limepotea ndio pesa zenu hizo hapo
 
No wonder few felt sorry about his sudden death. He reaped by the sword, and he died by it!

He might have gotten that cake in his lifetime through coercion, corruption and most dubious means imaginable given his pitiful wages as civil servant. But thank God, he didn't get to live long enough to eat and savor that rotten cake.

well said!
 
Utajiri
wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi
kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus
Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa
kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo,
Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo
malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya
Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza,
yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari
mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba
nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani
Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa
nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo
zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha
Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni
jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja
Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building
Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu
kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow
kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na
kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la
ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa
tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa
na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza
kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya
vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi
kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na
kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga
jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza
ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi
na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu
atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na
kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo
kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi
kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi
wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka
mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku
ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa
nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa
nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua
kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne.
Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea
na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya
kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na
magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota
Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika
umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake
kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na
wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya
mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo,
alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata
wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya
gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar,
ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini
Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa
umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima Sasa huu ndo utajiri wa kutisha? Mkuu vipi mawaziri wenye mabilioni uswis?
 
Mnakumbuka gari ya ex mwanasheria mkuu chenge ilikua haina bima?nchi hii walalahoi tunanyonywa sana
 
Hawa wakuu hivyo ndivyo wanavyo-survive. Kuna mmoja alichukua kiwanja sehemu moja yenye utata, alichokifanya ni kuwaonyesha waendesha magendo wakuu wa ule mji ambapo yeye alikuwa kaimu RPC. Hao waendesha magendo wakagawana majukumu, mmoja kaleta cement ya kutosheleza ujenzi, mwingine kaleta mbao, mwingine kaleta nondo, mwingine, mwingine vitu vya finnishing. Fedha ambayo ilimgharimu mkuu ilikuwa ni ya kuwalipa mafundi tu.
Halafu hao jamaa wa magendo hawakamatwi katika shughuli zao, na ikitokea polisi mgeni amewakamata huyo polisi anapewa onyo kali na wakuu wake.
 
Utajiri
wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi
kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus
Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa
kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo,
Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo
malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya
Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza,
yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari
mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba
nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani
Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa
nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo
zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha
Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni
jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja
Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building
Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu
kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow
kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na
kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

"Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la
ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa
tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa
na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia," alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza
kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya
vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi
kumkatalia.

"Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na
kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga
jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza
ghorofa nyingine mbili juu," alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi
na kuongeza:

"Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu
atasimamia yeye huko kwenye sheria."

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na
kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo
kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi
kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi
wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka
mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku
ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa
nondo zilizopotea.

"Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa
nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua
kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne.
Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea
na kazi pamoja nasi, " alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya
kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na
magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota
Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika
umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake
kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na
wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya
mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo,
alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata
wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya
gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar,
ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini
Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa
umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima Sasa huu ndo utajiri wa kutisha? Mkuu vipi mawaziri wenye mabilioni uswis?

UMAFIA HUU WA POLISI NA SERIKALI; NDIO UNAOPELEKEA UAMSHO KUAMBIWA NI MAGAIDI NA MA-ALQAIDA, WANAHOFU YA UMMA KUAMSHWA KUMBE KUNA UGAIDI WA STAILI NYENGINE PIA ; DUNIA NDOGO TU
 
Hilo la bima ya sh 60,000 (3rd party) tu nalo lilimshinda? Au ni huo mkanganyiko wa umiliki ndio ulifanya ashindwe kukata bima ya halali? Shame!

Hakuona umuhimu wa hiyo bima. Na ukizingatia yeye ni mtemi, hakuna polisi ambaye angehoji bima ya gari la bosi wao, na polisi wanayafahamu magari ya mabosi wao. Lakini mimi na wewe tukiweka bima fake watatusababishia usumbufu mkumbwa. Hii ndio TZ.
 
Sasa hapa ndo mpate kujuwa kuwa viongozi wa polisi wanashirikiana na majambazi. Hawa kina Kova wote ni wezi tu, wao badala ya kuleta amani wanaleta hofu. Binafsi siamini polisi hata mmoja nawafananisha na Kikwete na mawaziri wake. Jamani tuamke!
 
Back
Top Bottom