Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Yote ni feki kuanzia unywele hadi unyayo. Nyumba hadi mwanamke aliyekuwa naye vyote feki tu.

avatar2872_4.gif


Aisee wewe ni mzuri, naomba nisifie uumbaji wa Muumbaji
 
Suala la msingi hapa ni kufuatilia kujua kwa nini gari alilokuwa nalo namba zake ni batili, kwa maana kuwa namba hiyo hiyo inatumiwa na gari la mtu mwingine. Hali hii imeshamiri sana hasa katika mkoa wa Mbeya.

Sioni tatizo kwa yeye kuwa na nyumba za gorofa. Hivi ni kweli kuwa na gari tatu, nne tano au kumi ni utajiri? Hii ndiyo tafsiri ya utajiri kwa Tanzania? hizo nyumba hata tathmini hazifanyiwa kuweza kuestablish value zake lakini tunarukia tu huyu ni tajiri. Gari kuu kuu zinauzwa kwa fedha kidogo sana.

Umeeleza vizuri kuwa ana malozi ya mizigo yanayofanya biashara na bado unauliza hizo fedha amepata wapi? Tusitishe watu kuwa waoga wa kujiletea maendeleao kwa kigezo kuwa mishahara yao haiendani na mali walizo nazo. Si wote wameanza kazi wakiwa hawana kitu. Usimjaji mtu kwa kujiangalia wewe unapoanzia, kila moja ameanzia katika ngazi tofauti. Wapo walioanza kazi zao wakiwa na biashara tayari.

umesema kweli kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali au kuajiria kusiwe kigezo cha mtu kuchindwa kujitafutia maendeleo yake nakubaliana nawe kabisa sio kila mtu kwa sababu yuko serikalini basi umjudge kutokana na kipato chake wapo waliopata pesa au kufanya biashara kabla ya kupata kazi na walipo pata kazi hawakuacha kufanya biashara tusikimbilie kumtupia mtu lawama ati jambazi or kala rushwa hii sio sawa
 
Pengine ni mazoea na sitaki kushangaa maana kuna gari liliibwa pale mbagala likakamatwa baada ya mwaka muhusika akalifwatilia na kukuta aliekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha dar afande a.tibaigana ndie analimiki lilele gari..mhusika alipeleka vielelezo vyote mnavyovijua mwisho akaona aibu wakaomba wamalizane nje ya mahakama maana alienda mpaaka mahakamani

sasa swala la kuuwawa mh tujiulize mara mbili mbili kwa nini amekutwa na gari ya bima feki na namba feki usiku wa manane alikuwa analifanyia nini??usiku ule wa manane...na magari mengi ya wizi yalio na namba feki kazi yao mnaijua usiku huyu alikuwa anafanya nalao nini??


Wenu wasomaji
 
Aliikamata pale La Kairo hotel. Alitaka kuipeleka kituon ndo yakamsibu matatizo ya kukutana na polisi jamii.
 
Nchi hii bwana, ukifa tu, ndio kila kitu kinawekwa hadharani. inamaana hayo yote ya afande barlow hakuna aliyeweza kuongea before? tutaogopana hadi lini? kulindana eh?
 
Haya mambo ni ya kawaida sana kwa polisi. Kuna mjomba wangu mmoja aliwahi kuuziwa gari na watu fulani kule Moshi na alipouliza wapi kadi ya gari aliambiwa tunakutuma Dar ukamuone IGP fulani enzi hizo(jina nalihifadhi)atakupatia hiyo kadi basi huyo mjoma akaja akafikia kwangu.

Asubuhi akaniomba nimpeleke kwa huyo IGP, baada ya kuingia ofisini kwake alijitambulisha na akapokelewa kwa furaha sana na chai juu,akaandikiwa kiji-note aende kwa mkuu wa trafiki na vehicle inspector ambapo alipewa kibali cha usajili.

Tukaondoka hapo ofisini na baada ya siku chache mjomba wangu akapata kadi akasafiri zake kwenda Moshi. Hadi hivi leo ile gari ambayo ilikuwa mpya anayo na huwa anakuja nayo hapa Dar bila tatizo.

Hiyo ndiyo Tanzania jamani, mjenga nchi ndio mbomoa nchi.[/jadchiko
 
haya mambo ni ya kawaida sana kwa polisi. Kuna mjomba wangu mmoja aliwahi kuuziwa gari na watu fulani kule moshi na alipouliza wapi kadi ya gari aliambiwa tunakutuma dar ukamuone igp fulani enzi hizo(jina nalihifadhi)atakupatia hiyo kadi basi huyo mjoma akaja akafikia kwangu.

Asubuhi akaniomba nimpeleke kwa huyo igp, baada ya kuingia ofisini kwake alijitambulisha na akapokelewa kwa furaha sana na chai juu,akaandikiwa kiji-note aende kwa mkuu wa trafiki na vehicle inspector ambapo alipewa kibali cha usajili.

Tukaondoka hapo ofisini na baada ya siku chache mjomba wangu akapata kadi akasafiri zake kwenda moshi. Hadi hivi leo ile gari ambayo ilikuwa mpya anayo na huwa anakuja nayo hapa dar bila tatizo.

Hiyo ndiyo tanzania jamani, mjenga nchi ndio mbomoa nchi.

chiko huyo!alikuwa anapenda kuwalawiti wanawake..mzee mchafu sana yule..
 
Dah! hapa ndipo napokubali malipo ni hapa hapa duniani...they say dont speak evil of the dead, but with this we should aisee...mnyang'anyi huyu!
 
ndugu zangu ,hali kama hii watu wa hali ya chini ni vigumu kupata halki yao pale wanapo pata matatizo ,kwani watakimbilia kwa nani? utaenda kumlalamikia mtu mwenye fedha kumbe ni wakala wa bosi mwenyewe? au unatoa taarifa ya tukio flani kumbe unaye mwambia anajua kila kitu hadi anatafta namna ya kuficha ukweli. suala kama hili la kamanda kupatwa na mataizo kama hayo mda ule lina maswali mengi, kwa hiyo hata hilo la utata wa mali na anazo miliki inaonesha ni kiasi gani nchi yetu ilivyo na neemaq kwa walio juu na kuonesha ni kiasi gani ilivyo mbaya na hapafai kuishi kwa watu wa chini wasio kuwa kwenye sisitim.
 
umesema kweli kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali au kuajiria kusiwe kigezo cha mtu kuchindwa kujitafutia maendeleo yake nakubaliana nawe kabisa sio kila mtu kwa sababu yuko serikalini basi umjudge kutokana na kipato chake wapo waliopata pesa au kufanya biashara kabla ya kupata kazi na walipo pata kazi hawakuacha kufanya biashara tusikimbilie kumtupia mtu lawama ati jambazi or kala rushwa hii sio sawa
Yah,huyu Mzee alipambana sana, he deserved hivo vitu, familia yake haijaviendeleza kuna mashamba yake Geita na kiwanja Mwanza hakijajengwa mpaka leo
 
Mali kama ulipata kihalali itadumu
Kama ulipata kidhuluma zitapotea

Ova
 
Back
Top Bottom