Utajiri wa Daniel Yona unatisha!

Nini Pendekezo lako Mwitongo.

Napendekeza uchunguzi huru kujua uhalali wa mali za viongozi wengi katika nchi hii. Suala la uwanja hata mimi babangu ana mashamba (mapori) makubwa tangu mwaka 1950, lakini hajawa tajiri kiasi hiki. nadhani mwanya wa utajiri wa hawa watu ni siasa na utumishi wa umma, kwa kifupi ni wizi. Huhitaji daktari kukueleza fulani kafa, wakati unaona hana shingo!
 
Natoa ushauri kama mods atakubali tufungue thred maalumu ya kuorodhesha mali zoote za hawa wezi ambazo tunaamini hawakuzipata kihalali ili ikifika 2015 tusimike hapo bedera ya Tanzania .
naomba kuwasilisha
 
Unachezea mafuta na madini weye? Na nishati ikiwa kwa pembeni? Utashangaa ukisikia majina ya wenye hela huko majuu....
 
Kuna moja kajengea wanawe kule kunduchi ununio baharini kabisa ukuta wake unoga na maji ya bahari, watu wanakula bata lol
 
kweli inauma ila hakuna jinsi maana ndio tanzania yetu kila kukicha utajiri unazidi zaidi na gap kati ya maskini na matajiri linaongezeka
 
sina maneno mengi...



432250_282832125112235_708150493_n.jpg

 
kuna jamaa yangu aliwahi kunambia kipindi kile cha mkapa walikua wanaviuza viwanda jamaa walikuwa wanapelekewa hard cash kwa mabox na wahindi home
 
mungu ibariki afrika..................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:biggrin::biggrin:ngoja niiimbe wimbo huu kidogo nipunguze machungu...
 
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha

Ulionyeshwa kijiji cha Mukandala?
 
....... Mbona hakuna jipya ............. ni vitu vya kawaida...... yale mabangaloo ya kina Mama Lwakatare unaweza kufananisha na hiiiiiiiiiiiiiii?
 
Alikuwa akishirikiana na fisadi Mkapa katika wizi wao na inasemekana ana mali nyingine nchi za nje zikiwemo majumba, lakini usishangae katika kesi yake akiibuka kidedea kwa ukosefu wa ushahidi wa kumtia hatiani.

Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha
 
Ile kampuni yake na BWM inaitwaje?
Si nasikia walijiuzia ule mgodi kwa bei ya kutupwa???
Ufisadi mkubwa wa BWM aliufanya kwa kushirikiana na huyu bwana na Kigoda,na walikuwa maswaiba katika madili,ndiyo chanzo cha utajiri wao wa kutisha
 
hapa dar LUKU agents zote za mtoto wake!kwani zilianzishwa wakati baba alipokua waziri wa nishati
 
Kwa Tanzania hii ni vigumu kujua mali halali ni ipi hasa. Mali zote zilizopatikana baada ya Azimio la Zanzibar kwa viongozi wetu ni mikono iliyojaa damu.
 
Ninashangazwa sana huu usanii wa hizo kesi zao, mtuhumiwa mkuu kwenye kesi yao ni Mkapa, Na wanajua kabisa Mkapa mwenyewe hawezi kufungwa ni kesi ya viini macho tuu na kuwapotezea watanzania muda na rasilimali zao.
 
Back
Top Bottom