Utajiri wa Babu Loliondo kufilisiwa

watz mmemshindwa mzee wa vijisent,mnataka kuhangaika na babu wa watu!!mwacheni apumzike,sijawahi ona mtu akijipeleka kwa mwizi ili aibiwe
 
Huu ni umbea kwani kuna mtu alishiklwa aende kule alikua kwa maamuzi binafsi??
 
Bado hajaacha kutoa kikombe,hapa Arusha stand yapo magari yanaenda Sumunge kwa Babu.ila sasa ivi aitangazwi kama mwanzoni.
 
Duh!!! Kibabu kumbe kilikuwa kitapeli. Ama kweli wajinga ndio waliwao.
 
Watakuwa wanamuonea, alisema kila mara kuwa ni tiba ya imani, na sio yeye, kwamba yeye hajui chochote, ndio sababu aligoma kuitwa mganga wa kienyeji.
Walienda kufanya nini huko?
Labda ni wivu tu ndio unawasumbua.
Manake kama ni kufaidi waliofaidi ni wafanya biashara wa hoteli, chakula na usafiri, hao ndio wa kufilisiwa
au la sivyo wenye kulalamika kila mtu akachukue 500 yake, ila alipie maji yake bei ya maji ya kukata kiu.
Mbona wamepata nafuu wengi tu?
 

MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.


Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.

Kwani wagonjwa wote ambao huenda Muhimbili, Agha Kahn, KCMC n.k hupona? Lini umesikia mgonjwa ameishtaki hospitali? Acha majungu na wivu, na wewe ota dawa ili uukate.
 
kekundu kekunduu kekundu shetani kekundu....wajinga ndio waliwao.......kumcha bwana ni jambo la maarifa tena ni jambo lenye thamani bali wapumbavu huidharau hekima hii wataangamia....
 
Mlitaka babu akalime mbuga, mjini hapa watu tunaishi kimjini mjini.......mjini watu hawaji na majembe shauri yako utalima lami?? akili ndo huweka watu mjini!!!!si unaona akina papaaa musofe, ndama mtoto ya ng'ombe na wengineo kibaaaaaaaaooo
 
nakumbuka wakati inshu ya babu inaanza kukolea ulikua ukiongea kuhusu kumponda babu kwenye umati wa watu wanataka kukula nyama,leo tena....toka lini ukaenda kumshitaki mganga wakienyeji?kisa dawa aliyokupa haikufanya kazi?
 
babu hakujitangaza ila kuna watu walimpa promo ya nguvu hawa ndio wa kulaumiwa pamoja transporters walio take advantage ya IMANI hii
 
Wanamwonea wivu babu wa watu bure, kama mumeshindwa kuwaburuza mahakamani na kuwafilisi mafisadi waliokula mabilioni ya wapiga kura kwanini mmufilisi babu ambaye yeye kachukuwa 500/= tu?

kweli kabisa na alisema ukiwa na IMANI....mmeshaliwa jamani msio na imani jipangeni tena....sasa na katiba mpya
 
Hao wanaotaka kumburuza mahakamani hawana akili na lazima watashindwa. Dawa ya imani na mahakama wapi na wapi?
 
Hata na mimi nashindwa kujua madai yako ya msingi ni nini? lakini pia ni hospitali ngapi walishakwenda wakatibiowa bila kupona na je walienda kuwadai madaktari gharama za matibabau?

Swali la msingi sana hili
 
Tusimulaumu babu wa loliondo. Wajinga ndio waliwanyo kakobe alisema lakini hawakusikia na bado wengine wanaendelea kuliwa na huyu babu.
 
Huyu ni mganga wa kienyeji kawa waganga wengine kiingiacho kwa mganga hakirudi kwani hakumlazimisha tena alikuwa ancaji tshs. 500 tuu sasa watamdai kitu gani imekula kwao.
 
Amewadanganya wabunge na mawaziri huyu babu inaonyesha ni mjasiriamali mzuri hakuchukua kitu kitu kikubwa ili wasishituke.
 
Back
Top Bottom