Utajiri wa Babu Loliondo kufilisiwa

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975

MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.

Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.
 
Mwacheni babu wa watu kwani alilazimisha watu waende? Kwanza alisema ni matibabu ya kiimani
 
Wanamwonea wivu babu wa watu bure, kama mumeshindwa kuwaburuza mahakamani na kuwafilisi mafisadi waliokula mabilioni ya wapiga kura kwanini mmufilisi babu ambaye yeye kachukuwa 500/= tu?
 
Kama watamfilisi waanze kwanza na wachungaji wanaotembelea magari ya kifahari kwa hela za wenye imani wao kama Rwakatare,Kakobe,Lusekelo,Mwingira.Hakuna aliyelazimishwa kwenda na inawezekana ambao hawakupona imani yao ilikuwa haba
 
Mwacheni babu wa watu, kwanza alisema hiyo tiba ni IMANI, halafu mlitumwa kwenda huku kunywa dawa? Babu aliwaita? Mkome viherehere vyenu. Wafilisini waliochukua majasho ya wananchi (EPA) sio babu wa watu.
 
Hata na mimi nashindwa kujua madai yako ya msingi ni nini? lakini pia ni hospitali ngapi walishakwenda wakatibiowa bila kupona na je walienda kuwadai madaktari gharama za matibabau?
Walalamikaji wanadai nini? TShs 500 au gharaza za nauli?
 
kwani mlilazimishwa kwenda kwa babu?wajinga ndio waliwao'mbona wengine hatukwenda kwake?majungu hayo
Yep, wakiambiwa hawakusikia...walijipeleka wao wenyewe. Wakaifilisi serikali yao tukufu waliyoisikiliza!
 
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi' (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.

Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.
go babu go..........kiendacho kwa mganga...
 
Mganga wa kienyeji kama Babu wa Loliondo harudishi kitu.Sisi waona mbali tulisema humu jamvini.Tukapuuzwa sana na kusemwa sana.Babu ni mganga wa kienyeji tu.Hana lolote.Imekula kwao hao wadai.
 
tULIWAAMBIA TOKA MWANZO KUWA HUYO NDAGA FIJO NI TAPELI WATU WALIBISHA TENA KWA DHIHAKA KUBWA HUMU HUMU JF ,BABU ALIKUWA MJANJA ALITUMIA NJIA YA DINI KUWAINGIZA WATU MKENGE.

HUMU NDANI JF WATU WANA KASUMBA YA DINI HATA KAMA WAKIONYWA VIPI HAWASIKII KWA KUWA KWA NJIA MOJA AU NYINGINE DINI ZAO ZINAGUSWA.

PIA HAITOSHI KUMBURUZA BABU PEKE YAKE BALI HATA KANISA LA KILUTHERI NA ASKOFU LAIZER NAO WABURUZWE MAHAKAMANI KWANI NAO WALINUFAIKA NA MGAWO NA MWISHO SERIKALI KUPITIA KWA WAZIRI LUKUVI NAYO IBURUZWE VILEVILE.

KIKO WAPI BANDUGU NATARAJIA NIONE TENA HUMU JF WATU WALE WALIOKUWA WANASHUPALIA KUWA DAWA YA HUYO BABU NI MUUJIZA NA INAFANYA KAZI, WAJITOKEZEE
 
gKZ+f6mFh6mMjqCHi4Zwc3heZ2pMVnRJWpJbcrNticJsj8JiiNRwlM5kitFjiuBrleNqld1bidpVhOVZit5QgttLfthIe9tLft9ThDVxjZt2nGfVAAAAAElFTkSuQmCC
mjengo anaoumiliki kwa sasa babu wa loliondo
 
Hahahaha! Si waliambiwa unapona kwa Imani yako! sasa wanataka kushtaki nini tena? hawana imani hao,imani yao ndiyo ingewaponya!
 
Kama watamfilisi waanze kwanza na wachungaji wanaotembelea magari ya kifahari kwa hela za wenye imani wao kama Rwakatare,Kakobe,Lusekelo,Mwingira.Hakuna aliyelazimishwa kwenda na inawezekana ambao hawakupona imani yao ilikuwa haba
umewahi kuiona gari ya kakobe?au umewahi kumuona akizurura nayo?usiongee usichokijua kakobe alikuwa na gari kabla hajawa mchungaji.au unafikiri ni std 7.hatakama asingekuwa askofu leo maisha yake yangekuwa juu.usimfananishe na babu wa loliondo.
 
Hayo ni majungu tu na fitina mmeshidwa mafisadi kuwafilisi mnatafuta babu mmeona ndiye size yenu.Acha ni Imani tu kama hukupona Imani huna full stop.
 
Back
Top Bottom