Utajili zaidi wa haraka

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Habari wanajamii!

Nawatafuta watu wenye mitaji ya kuanzia kama milioni 3 hivi tufanye nao biashara.

Biashara yenyewe iko namna hii ni kuzalisha umeme kwa kutumia machine ya kusaga itakayobadilishwa na kuwa ya kufua umeme kwa kufungiwa moter, nipo eneo moja Mkoani mwanza pembezoni mwa mji ni sehemu iliyo na watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa wamekuja kutafuta eneo hili, kwa bahati mbaya eneo hili hakuna umeme usambazwao na shirika letu la umeme la Tanesco bado haujafika, ingawa kuna mtu mmoja yupo sehemu hii ikijaribu kutoa huduma hii maeneo haya kwa kutumia machine ya kusaga yenye piston moja ambayo imeelemewa mzigo kwa mahitaji ya wateja kuwa makubwa hivyo kufanya watu kuendelea kukaa gizani


hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku

2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku

3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku

3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu

4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo

kwa kifupi mahitaji bado ni mengi mno na hudumu iliyopo sasa inalegalega sana kama utalizika na maono yangu ya kufanya nawe mfanyabiasha biashara hii katika eneo ili tafadhari tuwasiliane kwa kuniPM
 
kwa kuangalia nature ya hiyo biashara, utajua kuwa hailipi hiyo milioni 3 ni bora ua kaifanyie biashara ya kununua mpunga na kuuleta pale mabatini mwanza. nenda kabuni biashara nyingine
 
hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku
(kwa wakazi wa pembezoni na mji wa mwanza hawawezi kumudu bei hii, isitoshe wanaohitaji ni wachache kama wapo hawazidi 50, 50x500= 25000)

2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku
(wenye saloon hawana pato la kutosha kumudu hii gharama kama wapo hazidi 1, 1x3000=3000)
3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku
(hakuna ukumbi wa video unaoweza kumudu gharama hii labda useme @Tsh. 2000/day, kama yupo ni mmoja, 1x2000=2000)
3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu
(hakuna mwenye duka wa kumudu hii gharama isitoshe kwa vijini huwa wana wahi kufunga)
4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo
(kwa wenye baa labda kidogo nao hawawezi kuzidi 3, 3x4000=12000)

jumla ya mapato kwa siku itakuwa 25000+3000+2000+12000=42000 x30days =1,260,000 hapo bado hujatoa gharama za uendeshaji na matumizi ya ya kifamilia ambayo unaweza kuyakadiria kufikia 30,000/day, kwa mwezi kuwa 900,000, na kubakiwa na faidi ya 360,000 kwa mwezi,
hapa ni bora ukauze ng'ombe ufungue kwa mtaji wako binafsi na wala si wa kushirikisha mtu mtatafutana ubaya
 
Back
Top Bottom