Utafiti: Wanaume Hutumia Mwaka Mzima wa Maisha Yao Wakikodolea Macho Wanawake

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
Nimesoma juu ya utafiti huu ukanichekesha. Watafiti sasa wanasema kwamba kwa wastani mwanamme hutumia dakika 43 kila siku akibung'alia wanawake tofauti tofauti wanaokaribia 10. Hii ni sawa na kutumia mwaka mzima wa maisha yake (tukihesabu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 50) akitazama wanawake. Sehemu kubwa ambazo watu hupenda kufanyia shughuli hii ni katika maduka makubwa, katika baa, nightclubs na pengine tunaweza kuongeza barabarani (inasemekana baadhi ya ajali hutokea kwa sababu madereva wa kiume hawaangalii wanakokwenda bali wamekaza macho kwingineko kuangalia wanawake wanaotembea barabarani).

Wanawake nao pia wamo. Kwa wastani wao hutumia dakika 20 kuwacheki wanaume tofauti wanaofikia 6 kila siku. Hii ni sawa na miezi sita ya maisha yao ya kati ya miaka 18 na 50.

Umbo la mwanamke ndiyo sababu kubwa inayowafanya wanaume kumkodolea macho mwanamke wakati macho ya mwanamme ndiyo huwavutia zaidi wanawake. Tukumbuke hata hivyo utafiti huu ulifanywa kwa wazungu na ukifanywa kwetu pengine utaibua sababu na takwimu tofauti. Kwa habari zaidi soma hapa.

Kuna anayebisha kuhusu jambo hili la kutazamana?

 
e bwana huu utafiti nakubaliana nao....maana mie shingo huniuma kutazama vimwana...hasa nikiwa Kigali na nikija Dar..macho kwa warembo tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom