matumbo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 7,225
- 3,944
Mimi ningaliiona sensa ya maana kama serikali inatumia raslimali zake kuinua uchumi na hali duni ya watanzania. Unaspend hela nyingi kuhesabu watu wakati shule hazina hata madawati? Unamhesabu mtu leo kesho anakufa kwa kukosa dawa ya kutuliza maumivu? Wamama wanaenda kujifungua wanalundikana kama ng'ombe kwenye chumba kimoja bila vitanda wala huduma muhimu? Kama huwezi kumhudumia hata mjamzito unamhesabu nani?
Kwenda kuwahesabu watanzania ni usanii mtupu. Kwanza serikali ishughulikie mahitaji muhimu kama elimu, mahospitali, barabara hadi vijijini then ituhesabu. Watanzania tumekata tamaa kwani viongozi wanajilundikia mali huku sisi tukifa duni. Unamhesabuje mwananchi ambae hutibiwi hospitali moja nae? Ni kwa nini wasiwahesabu wale wanaopokea matibabu India tukajua ni kiasi gani cha kodi kinahitajika kwa mwaka ili tujikunje kufanikisha matibabu hayo?
Sensa ya kitanzania ni kama mtu anasesabu tu mbuzi. Haina manufaa yeyote kwa raia wake. Kama mtu anagoma kuhesabiwa ni sawa kabisa na ni haki yake. Tuache unafiki na tuambiane ukweli. Wanaonufaika na uchumi wa Tanzania sii watanzania hata kidogo.
Kama serikali inafanya kazi ya serikali basi ikiita watu kuhesabiwa wataenda tena bila ubishi wowote, ila kama ni huu usanii na unafiki wa kujinufaisha binafsi na familia zenu wengi watawagomea. Tunahitaji serikali itakayoweka system in order ili mtoto akizaliwa ajulikane amezaliwa. Mtu akifa ajulikane amekufa na sii ujinga wa kusukumana na watu eti unawahesabu huku huwahudumii hata katika mahitaji ya msingi.
Jengeni shule bora, hospitali za maana na njia bora za usafiri kwanza. Wapeni wanetu elimu bora. Jengeni vyuo bora na sii kuwakimbiza watoto wenu kusoma nje kwa garama ya mashule yetu. Rudisheni kwanza usafiri wa reli ili wananchi wasafirishe mazao na bidhaa zao bila usumbufu wa kulipia malori ya ridhimoja na vituo vyake vya mafuta.
Acheni unafiki. Hii serikali haina lolote la maana hata kama tungalihesabiwa wote kabisa. Sensa itajikamilisha yenyewe kama serikali inaihudumia jamii iliyoiweka madarakani. Bila hivyo hata tungalijipanga wote kwenye mstari na kuhesabiwa kwaq pamoja ni bure.
ndio maana tunasema mliotishia kugomea sensa hamjielewi mnagomea kwa sababu gani haswa!!