Greater thinker!!!!Kwa kweli hawa watu wanatuabisha watafiti wa Tanzania. Huwezi fanya kitu cha kuangalia ni chama gani kinaandikwa na kutangazwa zaidi na vyombo vya habari, kisha akaita huo kuwa ni Utafiti!!! What a rubbish.... Alafu wakaja waandishi njaa wa gazeti la uhuru wakasema chama kilichoongoza kwa kuandikwa zaidi eti 'kina mvuto'!!!! Mbona watu wanapenda kujifanya wajinga?
Yes, CCM inaandikwa zaidi kwa sababu yapo ya kuandikwa; Mwenyekiti wao kaanguka jukwaani, wanachama wake wamesingiziwa sio raia, wanachama wake wanakihama chama, wanachama wake wanakamatwa na Takukuru kwa rushwa, wagombea wake wanabembeleza watu waende kwenye mikutano, makada wake wanapeleka watu mikutanoni kwa malori, mipasuko na makundi chungu nzima nk nk alafu unasema inaandikwa kwa sababu ina mvuto!!!
Mi naomba hao synovate waipublish report nzima (kwenye gazeti of coz kwa sababu hakuna journal itakayopokea takataka kama hiyo), ili tuone objectives, methodology na result zilizopatikana.... swine...
Aise kweli lakini ni media ndio inasikitisha aise. Nasikia clouds waliongea zaidi kuhusu chadema. :welcome:Tetesi nilizopata ni kuwa wale watafiti wa Synovate Tanzania (ambayo inaongozwa na Wakenya) wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu media ya Tanzania ambao unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya habari kwenye vyombo hivi ni kuhusu chama tawala CCM.
Pengine hii inaashiria kuwa zile posho za CCM kwa waandishi wa habari kwenye kampeni ya Kikwete za shilingi laki moja kwa siku (100,000/-) zinafanya kazi. Utafiti unadhihirisha kuwa waandishi wa Tanzania wamenunuliwa na CCM na sasa wanalipa fadhila kwa kutoa habari za kukipamba chama tawala.
Haya ni matokeo:
1. Zaidi ya asilimia 50 ya habari kwenye media ni kuhusu CCM
2. Chadema inapata coverage ya kama 20%
3. Vyama vilivyobaki, CUF, NCCR, TLP, etc vinagawana asilimia iliyobaki.
Binafsi sijaiona hii taarifa ya utafiti, ila nina fahamu kuwa magazeti ya kesho ya kila siku yatatupa taarifa.
Pia, utafiti umeonyesha kuwa gazeti la serikali la DAILY NEWS ndiyo linaongoza kwa kuipendelea CCM. Kaimu mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali (Daily News, Sunday News na Habari Leo), Mkumbwa Ally, anasifika hapa mjini kwa kujipendekeza kwa Kikwete ili ateuliwe yeye kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali.
Utafiti huo umetoa marks/grades kwa magazeti na televisheni mbalimbali kuhusu coverage yao kwa vyama vya siasa, ikiwemo Habari Leo, Uhuru, Mwananchi, The Citizen, na magazeti mengine.
* ANGALIZO: Utafiti haujaeleza lolote kuhusu mgombea gani kati ya Dk. Willibrod Slaa, Kikwete au Lipumba anakubalika zaidi na wananchi, umeangalia mwenendo wa media tu.
Katika kile kinachoendelea kutokea na kuaminika ya kwamba watanzania wengi wamekuwa na imani na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imedhihirika baada ya kampuni moja ya hapa nchi inayofanya tathimini zake kuibuka na tathimini iliyo kuwa inasema ni chama gani kinacho kubalika kwasasa kutokana na muelekeo wa taifa katika uchaguzi mkuu ujao.
katika tarifa hiyo ilionyesha ya kuwa chama cha CHADEMA kinaongoza kwa asilimia 44% kikifuatiwa na chama cha CCM kwa asilimia 41% na asilimia zilizo salia kugawanyika kwa vyama vingine,
kutokana na ushabiki uliopo kwasasa taarifa hiyo ikapindishwa na kuandikwa visivyo baada ya kuonekanika ya kuwa CHADEMA inaongoza, ndipo ikaamuliwa taarifa hiyo iachwe isomwe ile ya ya vyombo vya habari, katika hili makada waliyo ingia ubia na chama cha ccm kukikampenia ambao ni wamiliki wa kituo kimoja cha radio station alipo pata taarifa hiyo aliamua kupiga simu kwa boss wa kampuni hiyo ya utafiti ya SYNOVATE kwakuwa ni rafiki yake na kumuamuru taarifa hiyo isitoke
boss huyo ndipo akaamua kupinndisha taarifa hiyo nyeti iliyo kuwa ikiwahusisha wananchi mbali mbali na sekta mbalimbali hapa nchini, MUNGU ENDELA KUIBARIKI CHADEMA
Kama kweli hawa watafiti wa SYNOVATE hii ilikuwa ni taarifa ya kwamba CHADEMA inaoongoza kuliko CCM halafu wao wakapewa maelekezo kuficha ukweli. Kama mtu ana taarifa ya awali angetupa ili tuisambaze katika vyombo vya habari vya nchii vyenye mapenzi mema na nchii hii ambao watatoa taarifa yao wakiwaumbua kwa kuficha ukweli; mtafiti anapaswa kuwa mkweli ili aweze kuaminika.
Wasijaribu kuisukuma nchi yetu kwenye uwanja wa maangamizi kwa sababu ya taarifa yao wapuuzi sana waliojaa tamaa mbaya
Haya ni matokeo:
1. Zaidi ya asilimia 50 ya habari kwenye media ni kuhusu CCM
2. Chadema inapata coverage ya kama 20%
3. Vyama vilivyobaki, CUF, NCCR, TLP, etc vinagawana asilimia iliyobaki.
As a research student,nadhani wa kulaumiwa zaidi pindi matokeo ya utafiti ambayo yanapokinzana na hali halisi ni mtafiti na wala sio waliohojiwa katika utafiti husika.Tunaweza kuwalaumu "Watanzania" lakini ni vema lawama hizo zikabainisha "Watanzania wa aina gani" wanaopaswa kulaumiwa.Tatizo la opinion polls za Synovate na REDET lipo zaidi kwenye subjectivity ambapo taasisi hizo zinakuwa na pre-conceptions za matokeo,na maswali yao yanakuwa leading to specific responses.
Hata kama mindsets za respondents ziko against ufisadi lakini kama researcher atakwepa kuuliza maswali ya kuchonoa hoja husika kwa undani ni dhahiri majibu yataonyesha ufisadi si kero kwa Watanzania.
Tukumbuke kuwa wahojiwa sio wanaotengeneza maswali.Ikumbukwe pia kuwa wahojiwa hawahusiki katika kuchambua na kutafsiri findings.Tatizo kubwa la pollsters wetu ni kutaka findings zao ziendane na matarajio ya watawala.Bila kuwa na independent pollsters (kwa maana ya kutofungamana na upande wowote) na wanaojibidiisha kupunguza subjectivity (kuindoa completely ni kitu kigumu) matokeo ya polls hizo yatatoa majibu yasiyoendana na hali halisi.
Kwa kweli binafsi sintakuwa hata na muda wa kufuatilia matokeo ya opinion polls za Synovate au REDET kwa vile hawa hawana tofauti na TBC,Daily News/Sunday News na Habari Leo au Uhuru na Mzalendo (including hao wanaojikomba akina Rai,etc).Sanasana watakachofanya ni kuonyesha kukubalika kwa CCM na Kikwete ni pungufu kidogo ya ilivyokuwa kwenye previous poll lakini si kwa kiwango cha kushindwa uchaguzi.
Huyu jamaa kasema kweli. Utafiti ni tofauti na monitoring. WAKE UP!!! Alafu hawa majamaa wamesema kwamba ni bora waandishi wawe wanaandika bila upendeleo. Mi sijui watu wanaelewa vipi hio statement.:confused2:Kwa kweli tuwe tunaongea kwa uhakika humu ndani, ninavyofahamu synovate ilikuwa ikidhaniwa kukibeba chama tawala hii ni SAWA.
Synovate imepata kazi kutoka shirika la kimataifa kufuatilia vyombo vya habari vinavyoripoti uchaguzi hii pia sawa
Waandishi wa habari wakaanza kulalamika kwa nini synovate wanachelewa kutoa matokeo hayo ya election media monitoring
Hatimaye juzi likawekwa tangazo pale habari maelezo kwamba watatoa report hiyo ya jinsi media inavyoripoti habari za uchaguzi kama ni fairly or not, na jana wakatoa habari hiyo na kusema wazi kuwa vyombo vingi vya habari vimeipendelea CCM hasa vyombo vya umma kwa kuipa muda mwingi tofauti na vyama vingine na wakaweka wazi kuwa hiyo ni kinyume na maadili ya uandishi pale habari maelezo.
Nashindwa kuelewa kama kweli wanapendelea CCM Wangetoaje ripoti kama hiyo inayoonyesha wazi CCM WAMEPENDELEWA.
Ndugu zangu wapenda maendeleo tuache kuipigia kelelele Synovate tunapoteza muda wa kampeni, na tuvipigie kelele vyombo vya habari vya umaa vinavyopendelea chama kimoja viache mara moja kwani viko hapo kwa ajili ya kodi zetu, Synovate wamefanya kazi yao ipasavyo this time, tungoje matokeo yao ya utafiti wa kura ya maoni