Utafiti Wa Synovate: CCM Hoi Zanzibar

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
BAADHI ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) wameshtushwa na ripoti za utafiti zilizotolewa na Kampuni ya Synovate ambayo imempa nafasi kubwa ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2010 Maalim Seif Sharif Hamad na kufuatiwa na Dk Mohammed Gharib Bilal na kusema kuwa hawakubaliani na utafiti huo.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliowajumuisha na kuwahoji wananchi 2000 Tanzania nzima juu ya viongozi waliopo madarakani na wengine wanaotarajiwa kuingia katika kinyanganyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao imetoa matokeo kwamba kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad anaongoza katika kinyanganyiro hicho kwa kupata asilimia 28

Pia utafiti huo umempa nafasi ya pili Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal kwa kupata asilimia 24 Wakati Waziri Kiongozi wa sasa Shamsi Vuai Nahodha akipata asilimia 10 na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein akipata asilimia 2.
Wakizungumza nje ya ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui jana wajumbe hao kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini wamesema utafiti uliofanywa haukuzingatia vigezo halisi vinavyohitajika na hivyo hawawezi kuuamini.

Wamesema utafiti uliofanywa ni wa uongo ‘feki’na hauna sifa ya kuitwa utafiti kwani baadhi ya wasomi hutafuta njia ya kuwafurahisha wagombea jambo ambalo wamesema hawakubaliani na utafiti huo kwa kuwa jambo la uchaguzi linahitaji uwanja mpana wa kisiasa na sio kwenye karatasi katika ilivyofanywa kwa kuulizwa watu wachache kwa vigezo visivyojulikana.
Wamesema kwamba utafiti huo huenda haukuzingatia vigezo sahihi na ndio maana ukawa na upungufu kwani haiwezekani utafiti wa nchi nzima ukafanywa kwa kuwauliza watu 2000 pekee wakati tanzania ina wananchi zaidi ya milioni 30.

“Mimi sidhani kama huo utafiti upo sawa kwa sababu kwanza utafiti huo umefanywa wapi, katika mazingira gani na akina nani waliohojiwa maana inawezekana ukenda sehemu moja ukawauliza watu 1,000 kuhusiana na mtu mmoja ambaye ni kwao na ana nafasi kubwa unategemea watu hao wakwambie nini hawamtaki?” alihoji Mjumbe huyo wa NEC.

Wajumbe hao wamesema kwamba haiwezekani Chama Cha Wananchi (CUF) kikapewa kuendesha serikali hata kama kitashinda kwa kuwa Zanzibar lazima iendelee serikali ya Mapinduzi na iwapo CUF itapewa kuendesha serikali Mapinduzi yatakufa ambapo lengo la mapinduzi ni kutaendeleza.

“Hatutaki kusikia tafiti za kijinga kama hizo hapa eti nini? Seif awe rais wa Zanzibar wapi labda aende kuwa rais wa Pemba huko lakini hapa sisi hatuwezi hata siku moja kumpa nafasi ya kuwa yeye rais kwani wana mapinduzi wapo wapi hata Seif atawale? Hilo haliwezekani kabisa kabisa” nenda kaandike hivyo hebu nenda nenda kule …alaaa hii ni nchi ya kimapinduzi hakuna mambo ya kura hapa kura ni utaratibu tu lakini nchi hii itaendelea kuongozwa kimapinduzi na sio kwa karatasi”

Hata hivyo wajumbe wengi wameoneshwa kukerwa na utafiti huo ambao umempa nafasi ya pili Dk Bilali ambapo Mjumbe mwengine amesema kutokana na vigezo vilivyotumika haoni kama Dk. Bilal anaweza kupewa nafasi kubwa kiasi hicho.

Amesema nafasi aliyopewa Dk Bilali haimsatahikii kutokana na kuwa hana umaarufu mkubwa unaofikiriwa na watu wengi ambapo alisema licha ya kuwa Dk. Bilali ni mjumbe wa NEC na pia aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar lakini uzoefu wake katika siasa ni mdogo na pia hana jambo kubwa ambalo amelifanya katika Chama Cha Mapinduzi.

“Mimi ni maarufu kuliko yeye kwa sababu mimi nimeshawahi kushika nyadhifa mbali mbali katika chama chetu nikianzia chini hadi juu taifa na nimeanza siasa tokea nikiwa mdogo lakini tumuulize yeye anatoka wapi na amefanya nini katika chama?” amehoji Mjumbe huyo ambaye yeye pia anatajwa kutaka kuwania nafasi ya urais Zanzibar.

Akizungumza na gazeti hili Mjumbe mwengine wa NEC Zanzibar ambaye ni Waziri wa Serikali ya Muungano amesema utafiti uliofanywa ulikuwa wa kujifurahisha nafsi zao wenye kufnaya tafiti hizo pamoja na wakubwa waliowatuma kufnaya tafiti hizo ambapo haiwezekani utafiti umpe nafasi kubwa Dk. Bilal.

“Ahhh mimi hizi tafiti huwa siziamini kwa kikubwa kipi cha kupewa nafasi ya pili huyo Dk. Bilali mimi kwa kweli nadhani huyo Dk. Bilali amewatuma hao wanaojiita wasomi wamfanyie utafiti lakini ni bure tu wewe ngoja huo uchaguzi uje utashangaa kitakachotokea” alisema.

Mjumbe huyo amewakumbusha wasomi wenye kufanya tafiti mbali mbali katika mambo ya siasa kuacha kutumia kigezo cha umaarufu kwani suala la umaarufu halina nafasi katika siasa za Tanzania kwa kuwa huko nyuma imeshawahi kutokea mtu asiyekuwa maafuru kushinda na kuchaguliwa kuwa rais kuliko aliyekuwa maarufu.

“Ngoja nikwambie unakumbuka mgombea wa urais wa Zanzibar mwaka 2000 alikuwa nani? Unakumbuka kama Dk. Bilali si ndio alikuwa maarufu jee kapata? Na jee nani alitarajia kama Amani Karume atakuwa rais yeye si aliangushwa kwa kura nyingi sasa na watu pia hawakumtaka lakini jee hakuwa rais? Kwa hivyo kigezo cha kuwa maarufu kisitumike kabisa? Alikumbusha Mjumbe huyo ambaye ni waziri katika serikali ya Muungano na anatajwa kuwa na nafasi katika kinyanganyiro cha urais Zanzibar.

Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Hamad Masauni Yussuf amesema kwanza hajui vigezo gani vilivyotumika katika utafiti huo lakini wananchi wengi bado wana kasumba kwamba Chama Cha Wananchi (CUF) bado kina ngome yake kubwa huko Pemba jambo ambalo amesema kwa sasa ni kinyume.

Amesema sio kweli kwamba CUF wana nafasi kubwa ya kushinda urais kwa Zanzibar na pia huko Pemba hali hivi sasa imebadilika ambapo CUF wana nafasi ndogo sana ya kushinda kwa kuwa wananchi wengi wa kisiawa hicho wamekata tamaa na viongozi wao na chama chao hivyo CCM ina nafasi kubwa ya kushinda katika kisiwa hicho.

“Hizi kasumba kuwa labda CUF wana ngome yao kubwa huko Pemba
Nadahani hivi sasa zinapaswa kuachwa kwanza kwa sababu mimi nimetoka hivi karibuni huko Pemba na hali ilivyo sasa sivyo hivyo ilivyo kabisa” amesema Masauni.

Masauni hakutaka kuongelea utafiti uliofanywa na Kampuni ya Synovate ambao umempa nafasi ya pili katika kinyanyanyiro cha uchaguzi wa 2010 Dk. Bilali kwa madai kwamba bado hajafanya utafiti katika chama chake kuona nani anafaa katika kinyanganyiro hicho cha urais wa 2010.

Amesema kwamba chama chake hakiwezi kumteuwa mtu asiyekuwa safi
hivyo kwa vyovyote vile lazima mgombea atakayeteuliwa atakuwa na vigezo na sifa zinazokubalika kuwa ni mgombea urais na hakuna sababu ya kuwepo utafiti wa sasa kwani CCM haijawahi kumsimamisha mgombea ambaye sio safi.

“Mimi sijafanya research ndani ya CCM kwa sababu najua chama changu hakifanyi makosa sisi tunachagua mgombea safi wakati ukifika mie nipo na kura yangu na nitampa kura mgombea atakayeteuliwa na chama changu kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na chama changu” amesema Masauni.
Hata hivyo amesema amekuwa akifanya na tathimini ya kukipima Chama Cha Wananchi (CUF) na amegundua kwamba kuna udhaifu mkubwa na huenda udhaifu huo ukawakosesha nafasi na uongozi viongozi kadhaa wakiwemo wabunge, wawakilishi na madiwani kwa kuwa CUF haina muelekeo.
“Mie sijafanya research katika CCM lakini research yangu nimefanya kwa CUF ni nimeona hawana nafasi katika uchaguzi mkuu ujao” amesisitiza Kiongozi huyo wa vijana ambaye anasema CCM ina nafasi kubwa ya kushinda bara na Zanzibar katika ngazi zote za uongozi.

Kwa upande wake Waziri Mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye anatajwa sana katika kinyanyanyiro cha urais wa 2010 amesema hana sababu ya kujilabu wala kuwatuma watu wamfanyie utafiti kwa kuwa anaamini nafasi ya kuwa mgombea anayo na anatarajia kupata nafasi ya kwanza kuliko aliyoipata Dk. Bilali katika utafiti huo uliofanywa ambapo kimsingi alisema hakubaliani nao.

“ Mie pia nina nafasi kubwa ya kushinda katika kinyanganyiro cha uraia wa 2010 lakini naona kama ni mambo ya kitoto kufnaywa utafiti hivi sasa kwani tuna haraka ya nini mimi nakwambia chaguzi zetu wewe ngoja utaona maajabu hapa yule mtu aliyekuwa anasemwa ni maarufu basi ataangushwa kichwa chini miguu juu” amesema mjumbe huyo.

Aliyekuwa Afisa katika balozi la Tanzania nchini Geneva, Mohammed Yussuf amesema tafiti zinazofanywa katika nchi za Afrika huwa zinatumia vigezo vya nchi za magharibi (Europe) jambo mbalo halileti picha halisi ya nchi za kiafrika kwa kuwa wazungu wanapojiandikisha aktika daftari la kupiga kura tayari huwa wanajulikana watapigia chama gani kitendo ambacho ni tofauti katika nchi za kiafrika.

“Wanapofanya hizi tafiti wasitumie vigezo vya Europe kwa sababu kule wenzetu wao wanapofanya registrations wanaweka details zao kabisa na wanajulikana kabisa kwamba fulani atakipigia chama fulani kama ni republican au chama chengine lakini sisi utamjuane kama mtu huyu atyakipigia chama hiki au kile?” alihoji.

Kwa upande wa wananchi wengi wamefurahishwa na utafiti uliofanywa na wamesema tafiti kama hizo zinaonesha hali halisi ya ukweli ambapo wananchi wengi wamesema wakizitarajia kufaywa na wasomi lakini kinachosikitisha katika matokeo huwa hayaendani kabisa na tafiti hizo kwa kuwa kuna uibaji wa kura katika chaguzi zinazofanyika nchini.

“Tatizo kubwa hapa hizi tafiti zinakwenda sawa sawa na matokeo ya uchaguzi kwa kuwa walitemtaja kashinda ndio huyo kipenzi cha umma unamjua? Ni maalim Seif lakini anayeshinda hapewi hiyo haki yake hapa kuna uporaji wa kura uibaji wa maboxi ya kura na hivi sasa kuna hili la kuwakatalia watu kuwaandika katika daftari hilo pia ni lengo la kuiba kura tu” amesema Mmoja wa vijana Ali Hamad Mohammed ambaye alizongewa na vijana wenzake katika eneo la darajani alipokuwa akisoma gazeti la Mwananchi huku umma mkubwa wa vijana ukiwa nyuma yake wakimshangiria,
amesema mjumbe mmoja kwa ghadhabu kubwa huku akimsukuma mwandishi wa habari hizi.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi
 
Last edited:
Kwanza nimpe pole mwandishi wa habari hizi kwa kusukumwa sukumwa na "wakereketwa" utafikiri yeye ndiye aliyefanya utafiti huo, halafu kama hawa CCM(madhalimu) wanakuwa vegeugeu, si hawa hawa synovate(zamani steadman Grp.) walifanya utafiti kama huo mwaka 2000 na kumpa "advantage" rais Karume, nawao wakapita wakijitapa na kujinadi kuwa maoni hayo yanaonyesha kuwa mgombea wao anakubalika,leo hii imekuwaje tena hawakubaliani na utafiti huu.
 
Salma Said, Zanzibar

BAADHI ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Zanzibar, wameshtushwa na matokeo ya utafiti wa masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanayoonyesha kuwa katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha urais wa visiwa hivyo mwakani.

Ripoti hiyo iliyotolewa juzi na kampuni ya Synovate, pia inaonyesha kuwa waziri kiongozi wa zamani wa Zanzibar, Gharib Mohammed Bilal wa CCM ndiye anayefuatia kwa karibu Maalim Seif kumrithi Rais Amani Abeid Karume, ambaye anamalizia muda wake wa miaka 10.

Ingawa kamati hiyo kuu ya CCM upande wa Zanzibar ilikuwa ikiendelea na kikao chake cha kawaida jana, ripoti ya matokeo ya utafiti huo haikujadiliwa, lakini wajumbe walioongea na Mwananchi nje ya ukumbi wa mkutano wa ofisi kuu ya CCM Kisiwandui, walionekana kutofautiana.

Wengi walionyesha kushtushwa na matokeo yanayompa nafasi kubwa Bilal kwa upande wa CCM, wakisema chama hicho hakiwezi kumteua mtu kwa sababu ya umaarufu wake.

"Kwanza mimi ni maarufu kuliko yeye kwa sababu mimi nimeshawahi kushika nyadhifa mbalimbali katika chama chetu nikianzia chini hadi juu," alisema mjumbe mmoja nje ya ukumbi wa mikutano wa chama hicho ulio Kisiwandui.

"Nimeanza siasa tangu nikiwa mdogo. Tumuulize yeye (Bilal) anatoka wapi na amefanya nini katika chama," alihoji mjumbe huyo ambaye yeye pia anatajwa kutaka kuwania urais Zanzibar.

Alisema licha ya Bilal kuwahi kuwa waziri kiongozi na kwa sasa kuwa mjumbe wa NEC, uzoefu wake katika siasa ni mdogo na pia hana jambo kubwa aliloifanyia CCM.

Mjumbe mwingine wa NEC ambaye ni waziri katika Serikali ya Muungano alisema haiwezekani utafiti umpe nafasi kubwa Dk. Bilal, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

"Wewe ngoja huo uchaguzi uje utashangaa kitakachotokea," alisema waziri huyo ambaye kama wengine aliomba jina lake lihifadhiwe.

Katika utafiti huo, Synovate walihoji ni kiongozi gani ambaye wananchi wa Zanzibar wanampa nafasi ya urais baada ya Karume kustaafu mwakani na asilimia 28 ilionyesha kuwa ni Maalim Seif, wakati asilimia 24 ilionyesha ni Bilal. Waziri kiongozi wa sasa, Shamsi Vuai Nahodha alipata asilimia 10 na Makamu wa Rais Mohamed Shein alipata asilimia 2.

"Sidhani kama huo utafiti upo sawa kwa sababu kwanza umefanywa wapi, katika mazingira gani na akina nani waliohojiwa maana inawezekana ukaenda sehemu moja; ukawauliza watu 1,000 kuhusu mtu mmoja ambaye ni wa kwao na ana nafasi kubwa. Unategemea watu hao wakuambie nini, hawamtaki," alihoji mmoja wa wajumbe wa NEC Zanzibar.

Mjumbe mwingine alisema kuwa, suala la umaarufu halina nafasi katika siasa za Tanzania kwa kuwa huko nyuma imeshawahi kutokea mtu asiyekuwa maarufu kushinda na kuchaguliwa kuwa rais kuliko aliyekuwa maarufu.

"Ngoja nikuambie unakumbuka mgombea wa urais wa Zanzibar mwaka 2000 alikuwa nani? Unakumbuka kama Dk Bilal ndiye alikuwa maarufu, je, alipata?" alihoji mjumbe huyo.

"Na je, nani alitarajia kama Amani Karume atakuwa rais? Yeye si aliangushwa kwa kura nyingi sana na watu pia hawakumtaka, lakini je, hakuwa rais? Kwa hivyo kigezo cha kuwa maarufu kisitumike kabisa!"

Bilal pia alichukua fomu za kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, lakini alienguliwa katika uteuzi wa mwisho mjini Dodoma kutokana na utamaduni wa chama hicho wa kumwachia mshindi wa kiti cha urais amalizie kipindi chake cha miaka 10.

Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Hamad Masauni Yusuf alisema ingawa hajui vigezo vilivyotumika katika utafiti, anaamini kuwa wananchi wengi bado wana kasumba kwamba CUF bado ina ngome kubwa kisiwani Pemba wakati hali sasa ni kinyume.

Alisema sio kweli kwamba, CUF wana nafasi kubwa ya kushinda urais kwa Zanzibar na pia huko Pemba na kwamba hali imebadilika kwa sasa akidai kuwa, wananchi wengi wamekata tamaa na viongozi wao na hivyo, CCM ina nafasi kubwa ya kushinda.

"Nimetoka Pemba hivi karibuni na hali ilivyo sasa sivyo kama ilivyokuwa awali," alisema Masauni.

Hata hivyo, Masauni alisema CCM haiwezi kumteua mtu asiyekuwa safi na kwamba lazima awe na sifa zinazokubalika.

Aliyekuwa Afisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Geneva, Mohammed Yusuf alisema tafiti zinazofanywa katika nchi za Afrika huwa zinatumia vigezo vya nchi za Magharibi, jambo ambalo alisema halitoi picha halisi ya kile kinachokusudiwa.

Jijini Dar es salaam, wasomi na wanasiasa walikuwa na maoni tofauti kuhusu utafiti huo wakizungumzia sababu za Rais Jakaya Kikwete kukubalika huku watendaji wake wakionekana hawafai.

"Katika siasa, hili ni tatizo kubwa na linatakiwa litafutiwe ufumbuzi kwani hatuwezi kuangalia uzuri wa mtu mmoja katika taasisi nzima. Taasisi ni muhimu kuliko mtu mmoja kwani mtu huyo anaweza kuondoka na kuiacha taasisi," alisema mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Audax Kweyamba.

Lakini alisema inashangaza kuwa mfumo mzima wa uongozi kuanzia bunge na baraza la mawaziri wanakabana koo, isipokuwa pale inapofikia suala linalomhusu rais ambalo hufanya pande zote kumtetea, jambo linalomfanya awe maarufu.

"Haiwezekani wabunge na mawaziri wakabane koo, lakini inapofikia suala linalomhusu rais, wanamlinda na kumfanya kama malaika wakiwa na lengo maalumu na sio kufichua uovu wake," alisema Kweyamba.

Mhadhiri mwingine wa UDSM, John Jingu alisema matokeo ya utafiti huo yanategemeana na watu waliohojiwa.

Hata hivyo, utafiti huo katika kipengele cha viongozi wa kisiasa uliangalia umaarufu wa viongozi na ulihoji watu 2,000 walio Bara na Visiwani, wakati katika kipengele cha urais wa Zanzibar uliangalia nani mwenye nafasi kubwa ya kumrithi Rais Karume.

Aidha, baadhi ya wahadhiri ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema upande wa upinzani, hasa Chadema, umepata asilimia kubwa kutokana na kuibua kashfa nyingi za mikataba mibovu bungeni na kuwataja mafisadi.

Nao viongozi waandamizi wa vyama vya CCM, Chadema, TLP na CUF wameeleza wazi kwamba, hawakubaliani na mfumo uliotumika katika kupata matokeo ya utafiti huo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM- Itikadi na Uenezi, John Chiligati alisema anakubaliana na utafiti huo kuonyesha kwamba, Rais Kikwete anaongoza kwa umaarufu, lakini akasema watafiti wamepotoka upande wa Zanzibar, ambako katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ameonekana ndiye anayeweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2010.

Chiligati, ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema ni sahihi kwa utafiti huo kuonyesha kuwa Rais Kikwete anaongoza kwa kukubalika, lakini akapingana na kipengele cha mrithi wa Rais Karume akisema CCM imefanya makubwa visiwani humo.

"CCM imefanya mengi mazuri Unguja na Pemba na ukienda kumuuliza Mzanzibari yeyote, atakueleza safari hii CCM wameleta mabadiliko," alisema Chiligati ambaye ni mbunge wa Manyoni Mashariki.

Alitaja miongoni mwa mambo ambayo anafikiri yanampa nafasi kubwa ya ushindi mgombea yeyote watakayemsimamisha kuwa ni ujenzi wa barabara, usambazaji wa maji safi na umeme.

Mwenyekiti wa vijana Chadema, John Mnyika, alisema utafiti huo haukuzingatia suala la ufisadi wala rushwa na kwamba kama ungezingatia masuala hayo, CCM isingepata kura za juu.

"Hii taasisi haikutenda haki kwani maswali mengi katika utafiti wao yalikuwa yanahusu elimu, jambo ambalo lazima CCM ipate kura nyingi, lakini ingegusia masuala ya rushwa na ufisadi, hali ingekuwa nzuri zaidi kwa vyama vya upinzani na haki ingeonekana kutendeka pia," alisema.

Alisema taasisi zinatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kufanya utafiti wa kina wa kura za maoni, na sio kutegemea zile zinazotumiwa na serikali ambazo zinaipandisha juu bila ya kuzingatia ukweli uliopo.

Mkurugenzi wa uenezi na mawasiliano wa CUF, Ashura Mustafa alisema matokeo hayo yanalenga kuifanya jamii ya Kitanzania iamini kuwa, CUF ina nguvu upande wa Zanzibar pekee na pia kuwafanya wananchi wa visiwa hivyo wasiwe na imani na Prof Lipumba.

"Wameonyesha kuwa, Maalim Seif ndiye anayekubalika kwa upande wa Zanzibar ili wananchi wasiwe na imani na rais wetu mtarajiwa Lipumba, lakini pia wanataka kuonyesha kuwa CUF inakubalika Zanzibar tu ili hata wananchi wasimchangue mgombea wetu kwa upande wa urais," alisema Mustafa.

Alisema CUF ina nguvu kubwa ya kisiasa kwa upande wa Tanzania Bara kutokana na kuwa na uongozi kuanzia ngazi ya mtaa mpaka taifa tofauti na Chadema ambayo alisema haina uwakilishi kuanzia ngazi za chini.

Pia alipinga ripoti hiyo akidai kuwa idadi ya watu 2,000 waliohojiwa haiwezi kuwakilisha idadi ya Watanzania zaidi ya milioni 40.

Naye mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alichukulia matokeo hayo ya umaarufu kuwa ni kielelezo cha wanasiasa watakaogombea urais mwaka 2010 na hivyo kuielezea kampuni hiyo ya utafiti kuwa si wakweli kwa kuwa ameshatangaza kuwa hatagombea urais mwakani.

"Kwanza wamenidhalilisha kwa kuwa nimeshatangaza kutokugombea tena urais na hata chama changu kinajua hilo, sasa inakuwaje tena leo utafiti umhusishe Mrema?" alisema na kuunga mkono asilimia za Kikwete akisema kuwa amejitahidi kupambana na ufisadi


Source: Mwananchi 12.08.2009
 
Indirectly CCM wameanza kampeni za uchaguzi 2010. Ndiyo maana wanajenga mazingira ya Kikwete kukubalika na hata huko Zanzibar 24% kwa Bilali na 28% kwa Seif siyo gap kubwa ukiangalia idadi ya watu waliohojiwa Vs wapiga kura watarajiwa.

Ndiyo maana CCM wameamua kuwapa Bendi ya Vijana Kipanya(Hiace) kwa ajili ya kuwapigia kampeni. Ukiona harakati hizi ujue kumekucha.
 
Kwa maoni ya Mh. Cpt. John Chiligati amenukuliwa akisema kuwa amefurahishwa na utafiti huu,unaonesha kuwa Kikwete bado anapendwa na ana nafasi ya kushinda uchaguzi ujao, kwa maana hiyo Cpt. anakubaliana na takwimu za utafiti huo kwa upande wa visiwani, kuwa Maalim ndiye "jogoo" huko.
 
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Hamad Masauni Yusuf alisema ingawa hajui vigezo vilivyotumika katika utafiti, anaamini kuwa wananchi wengi bado wana kasumba kwamba CUF bado ina ngome kubwa kisiwani Pemba wakati hali sasa ni kinyume.

Alisema sio kweli kwamba, CUF wana nafasi kubwa ya kushinda urais kwa Zanzibar na pia huko Pemba na kwamba hali imebadilika kwa sasa akidai kuwa, wananchi wengi wamekata tamaa na viongozi wao na hivyo, CCM ina nafasi kubwa ya kushinda.
Masauni,
Hayo mabomu yanayolipuka huko Pemba si yanatoa picha halisi ya kutokubalika kwa SMZ na CCM yake?

Kauli yako angalia isije ikakusuta hapo mwakani!
 
Hapa ni siasa tu kwani huyu Chiligati kukubali kikwete na kumkataa Seif alitumia vigezo gani? CCM inaweza onekana imefanya mengi kisiasa lakini kiukweli hawajafanya kitu. Maana kama mpaka sasa bado wana hubiri kujikongoja wakati wana jumla ya miaka zaidi ya 40 hiyo ni failure. Hivyo hao wakina Chiligati waache watu watoe maoni yao then wao wayafanyie kazi siyo kukurupuka tu kujibu vitu visivyo na msingi.
 
kwani wana mapinduzi wapo wapi hata Seif atawale? Hilo haliwezekani kabisa kabisa" nenda kaandike hivyo hebu nenda nenda kule …alaaa hii ni nchi ya kimapinduzi hakuna mambo ya kura hapa kura ni utaratibu tu lakini nchi hii itaendelea kuongozwa kimapinduzi na sio kwa karatasi"

Junius, habari ndio hiyo :D Then kichwa cha bandiko lako kimekaa ndivyo sivyo... CCM inaweza kuwa hoi PBA tu!
 
Junius, habari ndio hiyo :D Then kichwa cha bandiko lako kimekaa ndivyo sivyo... CCM inaweza kuwa hoi PBA tu!
Kibs,
Yaaani umenichekesha mpaka nimetoka machozi,sasa kama unakubali PBA mpo hoi bin taaban, kwanini una kubaliana na kauli ya Masauni?
Halafu usisahau kuwa CUF ina ufuasi mkubwa Unguja(kwa maana kila uchaguzi inashinda jimbo walau moja) na PBA ndo ushindi bila ya jasho, CCM haijawahi kushinda kiti PBA, labda kwa "mbinu za hali ya juu" za kushinda uchaguzi alizosema Mzee Malecela.
 
Junius, habari ndio hiyo :D Then kichwa cha bandiko lako kimekaa ndivyo sivyo... CCM inaweza kuwa hoi PBA tu!
Yale ya Asha Bakari Makame, eti nchi haitolewi kwa vikaratasi, sasa kama mnasubiri mtolewe kwa nguvu ngojeni dawa ipo jikoni, nguvu ya umma, mtauwa Zanzibar nzima lakini mtaondoka.
 
Kibs,
Yaaani umenichekesha mpaka nimetoka machozi,sasa kama unakubali PBA mpo hoi bin taaban, kwanini una kubaliana na kauli ya Masauni?
Halafu usisahau kuwa CUF ina ufuasi mkubwa Unguja(kwa maana kila uchaguzi inashinda jimbo walau moja) na PBA ndo ushindi bila ya jasho, CCM haijawahi kushinda kiti PBA, labda kwa "mbinu za hali ya juu" za kushinda uchaguzi alizosema Mzee Malecela.

Nina hakika Masauni hapendi kusema ukweli kuhusu PBA, ndio maana namshangaa kwa kauli yake hiyo ambayo itamrudi mara baada ya uchaguzi. Zaidi inafaa awekeze nguvu za kutosha katika Jimbo la Mji Mkongwe na ili nae awe na cha kusema mara baada ya uchaguzi.

Mbinu za Malecela ambazo bado kuwa wazi ni ngumu kuzitabiri, ingawa jamaa zangu tayali wanadai kuzijua! Hata hivyo sidhani kama zinaweza kubadili chochote kwa upande wa Visiwani.

Tatizo kubwa la CUF ni kukebehi Mapinduzi, hii inawafanya wengi wapendao mageuzi kusita kujiunga nao, na kupelekea kuwepo na maneno ya nchi kutotolewa kwa karatasi.

CUF wataendelea kushindwa kwenye chaguzi hadi pale watakapokubali kuwepo kwa Mapinduzi.
 
Mbinu za Malecela ambazo bado kuwa wazi ni ngumu kuzitabiri, ingawa jamaa zangu tayali wanadai kuzijua! Hata hivyo sidhani kama zinaweza kubadili chochote kwa upande wa Visiwani.

Tatizo kubwa la CUF ni kukebehi Mapinduzi, hii inawafanya wengi wapendao mageuzi kusita kujiunga nao, na kupelekea kuwepo na maneno ya nchi kutotolewa kwa karatasi.

CUF wataendelea kushindwa kwenye chaguzi hadi pale watakapokubali kuwepo kwa Mapinduzi.
Hizi si mbinu tu za CCM kuwapa jina baya, na CUF hakuna Pahala rasmi waliposema kuwa hawayatambuwi Mapinduzi na ndiyo maana uliwasikia wawakishi wa CUF (BLW) walivyosimama kidete kupinga kauli ya PM Pinda iliyoashiria kutaka kuifuta SMZ(Serikali ya Mapinduzi), walipinga kwa nguvu zote. Kasumba za kuwa CUF wanapinga mapinduzi ni sawa na kauli zile za zamani tukiambiwa kuwa CUF wakipata serikali watamrejesha Sultani, msomi kama ww na wengine kauli hii ukiipima utaona kuwa ni kauli ya kipuuzi tu, haina maana yoyote, lakini ilisemwa, kwa makusudi ya kuichonganisha CUF na wananchi wa kawaida, kuwapoteza malengo bure na kuwaendeleza umasikini. Nakubaliana na ww kuwa CUF wataendelea kuporwa ushindi,lkn si kwa kuwa wanadaiwa kupinga Mapinduzi bali kwa kuwa SMT, wanahofia vugu vugu la mabadiliko ya visiwani kuhamia bara.
 
Kwa maoni ya Mh. Cpt. John Chiligati amenukuliwa akisema kuwa amefurahishwa na utafiti huu,unaonesha kuwa Kikwete bado anapendwa na ana nafasi ya kushinda uchaguzi ujao, kwa maana hiyo Cpt. anakubaliana na takwimu za utafiti huo kwa upande wa visiwani, kuwa Maalim ndiye "jogoo" huko.
Angalia, wajanja sana hao. Huyo bwana mkubwa anasema hivyo kwa sababu anajua hata maalim akishinda, lakini hatotangazwa mshindi, kwa hiyo hilo la umaarufu wala haliwaumizi kichwa
 
CUF wakishinda hapata kuwepo na SMZ, watakuja na serikali mpya, kama ile ya kabla ya Mapinduzi.
Kibunango 'asa unamambo ya Kisonge!!!
Serikali kabla ya Mapinduzi iliitwa "serikali ya Zanzibar".
Na CUF wakipewa serikali itaendelea kuitwa SMZ kwa kuwa neno "serikali" kwa mjibu wa katiba ya Zanzibar, lina maana ya "serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar" na Seif Shariff atakuwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kuwa katiba ya Zanzibar inatoa tafsiri ya neno "rais" kuwa ni "Rais wa Zanzibar na Mw'kiti wa Baraza la Mapinduzi"(ambalo katika mfumo wa vyama vingi baraza hilo hatujuwi limempindua nani).
 
Nini cha ajabu katika utafiti huo, kwani nani alishinda chaguzi za Zanzibar 1995, 2000 na hatimaye 2005? Hakuna siri, masauni n wengine wote wanafahamu fika kuwa ushindi wa CCM kwa Komandoo na Karume ni ushindi wa mezani. Sasa iweje taarifa hizo ziwe geni kwao

CM imeitahidi kwa nguvu zote ikiwa ni pamoja na kuingiza wapiga kurabandia na kugushi kura ili kuwapachika vibaraka wao madarakani. Kiongozi mna gongo hawezi kamwe kuchaguliwa kuiongoza Zanziba r hhata akishindana na jiwe.

Vizuri kama hizo taarifa haziwavytii basi waandae utafiti wao, au wajaribu kufanya uchaguzi wa haki na huru ZANZIBAR 2010. Hata hivyo kwa mwenye akili yeyote hujiuliza kwanini CCM wliukimbia muafaka 2007?
 
Kiufupi CCm wanatapatapa na wanaonesha kuna mpasuko ndani yo wenyewe kwa wenyewe tungewaelewa kama wangemtetea mwenzao kuwa kaonewa kupewa nafasi ya pili. Lakini pia wanaona kapendelewa kwa maana kuna ambao ni bora kuliko yeye. Wanaposema kuna wanamapinduzi ina maana Bilali hayumo.
Kama Masauni anasema hali ya pemba ni shwari kwanini sisiem wanawabania wapemba kuandikishwa si wawaache wajiandikishe kwa wingi ili wapate hayo majimbo. kiufupi hawa jamaa wazenji wameshafulia ni wabara tu ndio wanawabeba.
 
si wawaache wajiandikishe kwa wingi ili wapate hayo majimbo.
Wapemba hawakataliwi kujiandikisha kwa wingi. Zan ID zinakataza kuaandikishwa Wabara wanaovalishwa ngozi ya Upemba, Au wale wa Mombasa wanaovalishwa ngozi ya Upemba. msipotoshe mambo jamani. Ilikuwa ni CUF iliyopigia debe kwa nguvu zote Zan ID- ili kupinga askari watokao Bara wasiandikishwe uchaguzi Pemba, sasa na tuende nayo hiyo. This is a fair deal.
 
Back
Top Bottom