Utafiti wa RAI: CCM kushinda Arumeru kwa asilimia 61%

nafikiri ni mapema mno kutoa tafiti wakati hata kutangazwa wagombea kulikuwa bado, lets wait and see what will happen Arumeru East.
 
Kwa kuwa ni utabiri hauna tatizo hata Shr. Yahaya alitabiri mengi mwisho wake akafariki yeye hata Rai itatabiri mengi mwisho wa siku hatutaliona tena sokoni(natural death).
 
WanaJF
Gazeti la RAI linalomilikiwa na kampuni ya Habari Cooperation limeubuka na kile kinachodai ni kura ya maoni ya nani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki
Katika kile wanachodai ni utafiti wao katika kata 17 ni kwamba mgombea wa CCM Siyoi Sumari anatarajiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 61% huku mgombea wa CDM Joshua Nassari akitarajiwa kuambulia asilimia 38.5%. RAI wanadai Siyoi Sumari anaungwa mkono na makundi yote ya wananchi jimboni humo na pia ndiye anaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi

My take:Nadhani ufike wakati vyombo vya habari viache propaganda chafu kwa ajili ya kukatisha wananchi tamaa.Bado hatujasahau gazeti hilihili lilitoa tathmini kama hii wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambapo walidai katika utafiti wao mgombea wa CCM angepata ushindi wa asilimia 70%.Lakini nadhani wote tunayajua matokeo ya Igunga yalivyokuwa.Pia tafiti za kipropaganda kama hizi zimekuwa zikitumiwa na maafisa wa tume ya uchaguzi wasio waaminifu kuchakachua matokeo.

kwa hiyo unamaanisha zile kura nyingi alizopata Dr.Slaa hapa JF zilikuwa propaganda? Au ndo zile tume 'imezichakachua?'
 
Hahahaha Nimeipenda hii! Kumbe wanapodai CDM/Slaa alishinda urais wanamaanisha kulingana na kura zilizokuwa zinapigwa hapa JF?
Pathetic Losers!
 
Rai inamilikiwa na raia wa Iran ,na Mbunge wa zamani asiye raia wa Tanzania

Basi nimepata jibu la tafiti hii,lazima kuna shinikizo toka kwa Hussein Bashe juu ya chapisho ili,maana ni mmoja ya wakurugenzi wa Habari corp,pia ni mmoja ya wapambe wa Naoa Sumari
 
CCM itashinda kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanakubaliana na sera zake na mfumo wake wa kiutawala vyama vingine havieleweki watu wanaamini ni vyama kwa ajili ya viongozi kujinufahisha wao wenyewe tumeona kwa NCCR-MAGEUZI,CUF na bado tutaona kwa wengine haiwezekani chama kikawa na viongozi hao hao toka kimeanzishwa kana kwamba hamna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza ukichunguza na kufuatlia vizuri utajua kwamba hivi ni vyama vya watu fulani wao,marafiki zao na koo zao vimeanzishwa kwa masilahi ya watu binafsi na wala si kwa masilahi ya taifa sasa hivi watanzania wameshtuka wanaona bora waichague CCM kuliko upinzani,jimbo la Arumeru Mashariki CCM itashinda kwa kuwa wananchi wana imani nayo sana!

Nakubaliana na wewe kuwa siku ambayo watanzania wataichoka CCM haitaweza kushinda hata kwa kuchakachua. Kuhusu maslahi binafsi ya viongozi wa vyama na ndugu zao hili ni tatizo la vyama vyote ikiwemo CCM. Ndiyo maana amekufa mheshimiwa SOLOMON SUMARI na sasa amepitishwa SIYOI SOLOMON SUMARI kugombea nafasi hiyo.
 
Mkuu siongezi neno.Umempa vidonge vya sawasawa
 
Wapenzi wa CDM ni wengi, lakini wenye shahada za kupigia kura siyo wengi kama CCM.

nakumbuka hata arusha mjini mliwaita mashabiki wa chadema ni wahuni na hawana shahada.si mlijionea,NAWASILISHA TOKA TIBET
 
WanaJF
Gazeti la RAI linalomilikiwa na kampuni ya Habari Cooperation limeubuka na kile kinachodai ni kura ya maoni ya nani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki
Katika kile wanachodai ni utafiti wao katika kata 17 ni kwamba mgombea wa CCM Siyoi Sumari anatarajiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 61% huku mgombea wa CDM Joshua Nassari akitarajiwa kuambulia asilimia 38.5%. RAI wanadai Siyoi Sumari anaungwa mkono na makundi yote ya wananchi jimboni humo na pia ndiye anaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi

My take:Nadhani ufike wakati vyombo vya habari viache propaganda chafu kwa ajili ya kukatisha wananchi tamaa.Bado hatujasahau gazeti hilihili lilitoa tathmini kama hii wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambapo walidai katika utafiti wao mgombea wa CCM angepata ushindi wa asilimia 70%.Lakini nadhani wote tunayajua matokeo ya Igunga yalivyokuwa.Pia tafiti za kipropaganda kama hizi zimekuwa zikitumiwa na maafisa wa tume ya uchaguzi wasio waaminifu kuchakachua matokeo.

Mh! Bora ungesema Ijumaa kuliko RAI, RAI yenyewe si ya akina Rostam na akina Bashe? unategemea busara toka ktk kinya cha Mpumbavu? unakumbuka kauli ya Saddam Hussein kuwa Marekani huwa wanaigiza picha za kijeshi ili kuwatisha nchi zingine lakini uhalisia ni kwamba hawana huo uwezo? Muulize kilichomkuta hatakuambia kuwa ni maigizo tena! Sisi ndio Wameru na CDM itapita kwa 75% na utafiti tumeufanya mijini na vijijini, Waulize Rai wanajua vijiji vya ndani kama Ngabobo, Kisimiri,Ngereiyani? huo ni utabiri wa akina Sheikh Ubwabwa na Washili wawili wa Meru
 
Jamani vyombo vya habari pamoja na waandishi acheni kuamisha uongo kwa Wanarumeru waacheni wachague kiongozi wanaye mtaka basi,acheni propaganda za uongo.
 
WanaJF
Gazeti la RAI linalomilikiwa na kampuni ya Habari Cooperation limeubuka na kile kinachodai ni kura ya maoni ya nani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki
Katika kile wanachodai ni utafiti wao katika kata 17 ni kwamba mgombea wa CCM Siyoi Sumari anatarajiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 61% huku mgombea wa CDM Joshua Nassari akitarajiwa kuambulia asilimia 38.5%. RAI wanadai Siyoi Sumari anaungwa mkono na makundi yote ya wananchi jimboni humo na pia ndiye anaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi

My take:Nadhani ufike wakati vyombo vya habari viache propaganda chafu kwa ajili ya kukatisha wananchi tamaa.Bado hatujasahau gazeti hilihili lilitoa tathmini kama hii wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambapo walidai katika utafiti wao mgombea wa CCM angepata ushindi wa asilimia 70%.Lakini nadhani wote tunayajua matokeo ya Igunga yalivyokuwa.Pia tafiti za kipropaganda kama hizi zimekuwa zikitumiwa na maafisa wa tume ya uchaguzi wasio waaminifu kuchakachua matokeo.
RAI=Rost tamu
 
CCM itashinda kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanakubaliana na sera zake na mfumo wake wa kiutawala vyama vingine havieleweki watu wanaamini ni vyama kwa ajili ya viongozi kujinufahisha wao wenyewe tumeona kwa NCCR-MAGEUZI,CUF na bado tutaona kwa wengine haiwezekani chama kikawa na viongozi hao hao toka kimeanzishwa kana kwamba hamna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza ukichunguza na kufuatlia vizuri utajua kwamba hivi ni vyama vya watu fulani wao,marafiki zao na koo zao vimeanzishwa kwa masilahi ya watu binafsi na wala si kwa masilahi ya taifa sasa hivi watanzania wameshtuka wanaona bora waichague CCM kuliko upinzani,jimbo la Arumeru Mashariki CCM itashinda kwa kuwa wananchi wana imani nayo sana!

utakuwa unaliwa huogi kenge we laiti ningekujua ...,
 
WanaJF
Gazeti la RAI linalomilikiwa na kampuni ya Habari Cooperation limeubuka na kile kinachodai ni kura ya maoni ya nani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki
Katika kile wanachodai ni utafiti wao katika kata 17 ni kwamba mgombea wa CCM Siyoi Sumari anatarajiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 61% huku mgombea wa CDM Joshua Nassari akitarajiwa kuambulia asilimia 38.5%. RAI wanadai Siyoi Sumari anaungwa mkono na makundi yote ya wananchi jimboni humo na pia ndiye anaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi

My take:Nadhani ufike wakati vyombo vya habari viache propaganda chafu kwa ajili ya kukatisha wananchi tamaa.Bado hatujasahau gazeti hilihili lilitoa tathmini kama hii wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambapo walidai katika utafiti wao mgombea wa CCM angepata ushindi wa asilimia 70%.Lakini nadhani wote tunayajua matokeo ya Igunga yalivyokuwa.Pia tafiti za kipropaganda kama hizi zimekuwa zikitumiwa na maafisa wa tume ya uchaguzi wasio waaminifu kuchakachua matokeo.
sioni tofauti na hawa wanaoleta thread hapa na kusema sinyari atashinda kwa 85%. what is the difference. au kwa sababu ni mkuki kwa nguruwe.
 
Back
Top Bottom