Utafiti - UKIMWI una tiba? fuata maelezo hapa chini

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Jambo kubwa baya linaloendelea duniani ni kuwa matatizo ya wengine ndo njia za kujipatia utajiri kwa wengine.

Viwanda vikubwa vya madawa vinafaidika kwa kuuza madawa yasiyoponya magonjwa kikamilifu. Matokeo yake ni kuwa magonjwa huzidi kuwa sugu hivyo wao kuendelea kutengeneza dawa na kutajirika. Mifano halisi ni metakelfin za Italy.

-Malaria
-typhoid (homa ya matumbo)
-Cancer
-ARV (Ukimwi)

Utafiti unaonyesha kuwa zile Research Organisation zinazofanya utafiti, kadri matokeo mazuri yanapopatikana, na kutangazwa Hivyo viwanda vya dawa hutoa pesa nyingi ili hao watafiti wasitangaze au kusabotage.

Kwa hiyo wanafaidika kwa kuuza ARVS, n.k

Pia Kuna Tetesi kuwa Limao na aloe Vera zikitumika kila siku basi virusi wanapungua katika mwili wa binadamu na pia anaweza kupona kabisa. Pia Watafiti wa Australia wanatengeneza Jelly kwa ajili ya wanawake kujipaka ukeni ambapo ni kinga ya ukimwi. Hiyo jelly inatengenezwa kwa malimao.

Naomba wana Jf mfuatilie hizo website na mtoe maoni yenu hapa.

Kuna haja ya watanzania kufanya utafiti wa kitibabu na kuja na madawa ya kitanzania bila kuingiliwa na WHO au pharmacies.
 
Hawa (alternative medicine) nao wanataka kutajirika.

Wajinga ndio waliwao kwa hiyo watakuja na ma-conspiracy theories yao, na ma-articles marefu (kama emails za wa-Nigeria) ili kukuingiza mkenge.

Hata Dar, kuna tetesi waganga wa kienyeji wana-make kinoma juu ya ignorance ya wagonjwa.

Dawa wanavyozipata utachoka, mara kaoteshwa na mizimu ya babu!! Ngoja wawe fit kwenye mtandao na technolojia watakuja na research kama hizi.

Kila la kheir.
 
Kimsingi, hapa Tanzania utafiti wa Dawa za Asili unakuwa discouraged kishenzi...Sometimes hata kabla dawa hizo hazijafanyiwa Tests na mamlaka husika, tayari wanasiasa wanaingilia kati na kuziponda, kisa wana hisa kwenye makampuni ya ARVs. Mimi nadhani ni wakati sahihi sasa kuacha kila taasisi na watu binafsi wenye fani za utafiti wa madawa, wafanye kwa uhuru kazi hiyo, na wapimwe kwa matokeo. Vinginevyo, tutaendelea kuwatajirisha hawa machinga wa ARVs.

Tanzania ilibarikiwa na Mungu kuwa na rasilimali zote muhimu kabisa, na hivyo naamini hata dawa ya UKIMWI ipo Tanzania, ni matter ya muda tu na utafiti sahihi!.
 
Hili pia dawa ya Ukimwi, mie nilisikia na kweli kuna mtu alishuhudia kapona.
Vundika mkojo wako na unywe kila siku. Sasa sijui nayo ni mambo ya kienyeji au vp, lkn dawa ndio hiyo.
 
Hili pia dawa ya Ukimwi, mie nilisikia na kweli kuna mtu alishuhudia kapona.
Vundika mkojo wako na unywe kila siku. Sasa sijui nayo ni mambo ya kienyeji au vp, lkn dawa ndio hiyo.

Dada Pretty,
Mimi siupondi utafiti wa kiasili, lakini kwa taarifa uliyotoa

hapo juu, nina mashaka kwa sababu ulisikia tu, na mtu

kashuhudia kapona!!.. Tafuta uhakika wa taarifa zako.

Pia,uuvundike huo mkojo kwa siku ngapi? We unaonekana

una taarifa nzuri, lakini ndo hivyo, una sita kiaina kuitoa. -

Lete mambo bana!!
 
mkojo kwenye uponyaji wa ukimwi unatakiwa kuuvundika siku 3, ila kwenye magojwa kama vidonda vya tumbo unaweza kunywa mkojo wako kila siku ule wa asubuhi unapokojoa.
Hii ni kweli ni tiba, sio nilisikia tu na kushuhudia bali nilimuona mgonjwa na cheti chake alikuwa HIV +positive na baada ya hiyo dawa ya mkojo akawa HIV -negative.
 
kwa kweli tiba za asili zikifanyiwa utafiti vizuri zinaponyesha ugonjwa huu ila watu wanaogopa kujitokeza na hawa wakijitokeza hawapewi sapoti.

mimi nina ushuhuda kuna mtu namfahamu tangu 2004 ni hiv positive ametumia dawa hizi ya kunywa kwa muda wa miezi mitatu na amepona kabisa ameenda kupiwa yuko negative alishakuwa ICU zaidi ya mara tatu alienda kukaa kwa huyo mtengeneza dawa kwa miezi mitatu unanywea dawa hapohapo na dawa zake hakupi kama hujapima CD4 ili ajue utatumia dawa kwa muda gani na utumie kipimo gani.

Huyo mtu kwa sasa yuko nje ya dar akija nitamuuliza vizuri anipe details then nitawaletea hapa maana amemaliza kunywa dawa mwezi wa tatu lakini ni mzima.
 
atarudi dar lini ssa? hana simu? unatucheleweshea nyuzi kichizi.
 
atarudi dar lini ssa? hana simu? unatucheleweshea nyuzi kichizi.

tangu ametoka huko kwenye dawa hajaj dar, niliongea naye kwenye simu akaniambia ameishafanya vipimo kuanzi KCMC , angaza na ameenda kwao Mwanza akapima Bugando yuko negative ameniambia ni habari ndefu tunatakiwa tuongee uso kwa uso atakuja soon nitawaambi usijali.
 
Namsupport Joycelin, tiba za asili mie nimesikia pia kuna watu wamepona hapo hapo Dar. Sema wenye kujua tiba, definetly wanakatishwa na taratibu za kufuata hadi dawa zao zikubalike.

Kuna binti namfahamu nae alikuwa +ve, majuzi majuzi katika story na ndugu zangu wa karibu wakaniambia huwezi amini binti ameenda kupima sasa mara tatu..hospitali tofauti na yuko -ve. Yeye wanadai ametibiwa na tiba ya asili na wakat anapata hiyo tiba walivyomwona akiwa anatumia hizo dose....Binti mwenyewe mpaka leo nasikia haamini km amepona.
Ametibiwa na mtu aliyetumia tiba ya asili ana asili ya DRC.

Pia kuna wengine pia wakadai kuna tiba inatolewa na watu wa asili ya DRC if not mistaken walisema wako tabata sijui ni tegeta..nasikia nao wanatumia tiba za asili na watu wanapona.....
Ila malipo yanatofautiana..huyo binti anadai huyo mwenye tiba anatoza million 3/4 kwa dose nzima wakati hao wa tabata nikikumbuka vizuri walisema milioni haifiki na unakuwa umemaliza dose.
ila tiba inavyoanza nasikia kwanza inakupelekesha hoi sana.....asiyemvumilivu anaweza kata tamaa..ila wanadai mwishoni inatibu.
Labda wadau mlioko Dar mdodose hii tetesi kufuatilia lazima wanajulikana wanaotoa tiba za asili
 
Wakuu tusipotezeane muda hapa....HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEWAHI KUWA NA HIV akatibiwa akapona duniani.....if tested positive with HIV antibodies and viral load confirmed...mtu huyo hata akitumia ARV ataweza kuzuia replication ya HIV viruses...CD4 zitaongezeka lakini always atakuwa positive with HIV antibodies....

Akina Hawa Nyamicho, na Dr Ezekiel walikuwa wanamitishamba inayotibu magonjwa nyemelezi....na kumpatia mgonjwa hamu ya kula....ndiyo sababu walikuwa na tiba kwao walionekana kupata nafuu. Kosa walilofanya ni kutembea na wagonjwa wao baada ya kupata nafuu UKIMWI ulimuua Hawa Nyamicho na hata Dr Ezekiel.

Ukimwi hauna kinga tumia kondom na acha ngono zembe......dawa zilizopo ni kupunguza makali tu .....eti alipima akawa positive sasa hizi -ve acheni hizo hadithi....kuna descrapancies sana kwenye vipimo hasa bongo...unaweza ambiwa unangoma kumbe laaa ama huna ngoma kumbe umeathirika.

Masa
 
Jambo kubwa baya linaloendelea duniani ni kuwa matatizo ya wengine ndo njia za kujipatia utajiri kwa wengine.

Viwanda vikubwa vya madawa vinafaidika kwa kuuza madawa yasiyoponya magonjwa kikamilifu. Matokeo yake ni kuwa magonjwa huzidi kuwa sugu hivyo wao kuendelea kutengeneza dawa na kutajirika. Mifano halisi ni metakelfin za Italy.

-Malaria
-typhoid (homa ya matumbo)
-Cancer
-ARV (Ukimwi)

Utafiti unaonyesha kuwa zile Research Organisation zinazofanya utafiti, kadri matokeo mazuri yanapopatikana, na kutangazwa Hivyo viwanda vya dawa hutoa pesa nyingi ili hao watafiti wasitangaze au kusabotage.

Kwa hiyo wanafaidika kwa kuuza ARVS, n.k

Soma hapa:: Alternative Cancer Treatments Home Page (the Cancer Tutor Website)
Research - Articles - Journals | Find research fast at HighBeam Research
J.Crow's®,Herbs,Spices,Essential Oils,Fragrances,Tibetan,Incense,Stamps,Folk Medicine,Organic,Apple,Cider,Vinegar,buckwheat,hulls,pillows,Ethnobotany,Ethnobotanical,Beeswax,Absolutes,Mark Twain,Lugol's Solution of Iodine,iodine,lugol,lugol's solution

Pia Kuna Tetesi kuwa Limao na aloe Vera zikitumika kila siku basi virusi wanapungua katika mwili wa binadamu na pia anaweza kupona kabisa. Pia Watafiti wa Australia wanatengeneza Jelly kwa ajili ya wanawake kujipaka ukeni ambapo ni kinga ya ukimwi. Hiyo jelly inatengenezwa kwa malimao.

Soma Hapa:: Herbs To Herbs
Middle Path Organic Natural Health Retreat Naturopathy Detox Depression Colon Cleanse
eHow | How To Do Just About Everything!

Naomba wana Jf mfuatilie hizo website na mtoe maoni yenu hapa.

Kuna haja ya watanzania kufanya utafiti wa kitibabu na kuja na madawa ya kitanzania bila kuingiliwa na WHO au pharmacies.
Mimi nafikiri ushauri wako wa mwisho "Kuna haja ya watanzania kufanya utafiti wa kitibabu na kuja na madawa ya kitanzania bila kuingiliwa na WHO au pharmacies." ni wa muhimu sana kwakuwa kuna madawa ya kitanzania ambayo yanatibu vizuri kuliko dawa za kisasa kwa mfano kuna tiba ya mtu aliyevunjika mfupa inapatikana huko same, ukweli ni kwamba mahali palipovunjika panaunga kwa muda wa siku 16 tu.! wengi wametibiwa na hata mguu uliopondeka mifupa badala ya kuukata unaungika..

Utafiti wetu wenyewe utatupeleka mbali si kwenye tiba tu bali hata na mambo mengine
 
Kama ulichooandika kina ukweli wasiliana na Institute of Traditional Medicine pale Muhimbili kwa Dr Mbwambo huyo kwenye picha! http://www.muhas.ac.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=39&Itemid=57

Unataka kusema tukifanyia tafiti zile nyungo za kupaa usiku Sumbawanga na wale fisi wanaotumika na walozi mikoa ya kati tutafika mbali? I doubt....
 
Hatukatai kuwa watu waendelee kujikinga na Ukimwi kwa njia tatu zinazofahamika. Ila pia tunatoa maoni kwa kile tulichosikia. Inawezekana tiba ipo? sio kukana ati tu kwa sababu inatoka kwa mganga wa asili tena Africa.
Leo likitoka tangazo, UK wamepata dawa si mtaamini? Je utakuja na point kuwa waache hadithi hakuna tiba ya ukimwi? Ina maana tiba haiwezi patikana?
Sawa na malaria, bahati ina tibu za asili na za kisayansi. lakini pamoja na hivyo watu bado tunashauriwa tujikinge na malaria, kwa kutumia net n.k
Vile vile na ukimwi...watu wasizembee ..waendelee kujikinga na waachane na ngono zembe...Ila kama kuna tetesi kuna tiba za asili..zi mbaya zikifuatiliwa regardless of source country. Huwezi jua tiba hizo za asili, zinaezwa kuja kugeuzwa na kuwa tiba ya kisayansi. Hata hivyo mbona dawa za mahospitali ..zote source ni mimea ya asili...
Huwezi jua ufuatiliaji wa haya masuala yanaweza kuja kuokoa maisha ya watu wa ngapia???
 
Dawa mpaka kutumika huwa zinapitia majaribio mengi sana (clinical trial phases) kuangalia toxicity, torelability, efficacy mpaka kuja establish IC50 etc etc....ukisikia dawa mpya ujue ilikuwa kwenye majaribio zaidi ya miaka 10 maabala.
Dawa nyingine za mitishamba kufikia dosage inayotakiwa wakati mwingine inabidi unywe ndoo nzima....sizidharau kuna zinazotibu ama kupungaza hata magonjwa yasiyo na tiba mbadala ie cancer kisukari etc etc.....

Waganga walio wengi ni wajasiliamali...uongo mtupu....kuna kituo pale muhimbili kina shirikiana na big phamaceutical companies duniani kuchunguza hizo tiba za asili...lakini matokeo yake ndo hivyo hayaridhishi na waganga hawatoi ushirikiano. Kuhusu HIV najua kuna jamaa wanafanyia tafiti dawa hizo asili zaidi ya 15 yrs na hakuna dalili nyingi ya mizizi pori ina antibacterial, antiprotozoan na hata antiviral activities kwa kiwango kidogo....dawa ya ukimwi ama chanjo viko mbali sana

Masa
 
mimi hayo ninayoeleza ni kweli nitajaribu kumshawishi huyo mtu ajiunge hapa awape ushuhuda mwenyewe halafu huyo mtu, aliyemtibu ni mwanamke na hatozi kitu chochote ni bure tu anamuhudumia kwa dawa , chakula , malazi mpaka apone na huyu ni mtu wake wa tano hana tangazo wala haambii mtu labda watu wake wa karibu wakwambie na wakuombee kwake ndo akupe dawa hivihivi hapana.
 
Back
Top Bottom